Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Bwana Tuliponga,
Kuku wa kienyeji ni wastahimilivu sana dhidi ya magonjwa. Mara nyingi kuku wakienyeji wanaofugwa na watu wa vijijini hawawajali sana katika mtibabu na ndio maana unakuta mfugaji kwa muda fulani anakuwa na kuku wengi lakini baada ya muda tena kuku wote wanakufa kutokana na magonjwa.

Hata hivyo wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji wanazingatia sana chanjo sana sana ya ugonjwa wa mdondo/kideri /kipetupetu kama ambavyo unavyojulikana kwa majina mengi na wafugaji wengi katika maeneo tofauti tofauti. Kifupi ugonjwa ni mmoja lakini majina ni mengi.

Kuku wa kienyeji wanahitaji huduma zote wanazopatiwa kuku wa kisasa kwakuwa magonjwa anayopata kuku wa kisasa hata kuku wa kienyeje naye anayapata. Kimsingi magonjwa ambayo yanawatesa sana kuku wa kienyeji ni pamoja ugonjwa mdondo, ugonjwa mafua, minyoo, Vidudu visumbufu mfano viroboto, utitiri, na chawa, ugonjwa ndui, taifodi, kipindupindi pamoja na ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis)

Kama mfugaji atafuata ratiba kamili ya chanjo pamoja na kinga kwa kuku hawa wa asili, hakutakuwa na vifo vyovyote vitakavyotokea kwa kuku wake hata kama wakifugwa katika mazingira ya kuachiwa huru wakijitafutia chakula chao wao wenyewe. Kitu kimoja cha msingi cha kuzingatia ni kwamba eneo ambalo wanaachiwa huru lazima liwe limezungushiwa senyenge ili kuku wasiende mbali sana wakapata kuliwa na wanyama waharibifu mfano vicheche, paka, mbwa nk.

Dawa kwa ajili ya chanjo na kinga zinapatika madukani.
 

Itafaa tangazo likajitegemea na uzi wake ili wengi waweze kusoma, bila shaka mtatumia na media nyingine kuwafikia wengi. Kila la kheri
 
Itafaa tangazo likajitegemea na uzi wake ili wengi waweze kusoma, bila shaka mtatumia na media nyingine kuwafikia wengi. Kila la kheri

Sawa kaka nimekuelewa nitafanya hivyo mkuu, pia litatangazwa kwenye midia soon
 
wakuu naombeni kupata ramani au muundo wa banda la kufugia kuku wa kienyeji namna gani linavyotakiwa kujengwa vyumba vingapi na kazi ya kila chumba
 
wakuu naombeni kupata ramani au muundo wa banda la kufugia kuku wa kienyeji namna gani linavyotakiwa kujengwa vyumba vingapi na kazi ya kila chumba

Ndugu yangu donMramba,
Sisi wataalam mara nyingi ushauri wetu una base zaidi kwenye kukupa wewe specification kwa maana eneo kiasi gani linahitajika kwa kuku kadhaa, lakini pia tunakupa sifa za banda bora la kuku, liweje ili kuku wako waweze kuishi na kukua vizuri.

Ramani ya mabanda itategemea na wewe mwenyewe preference yako ni kama ujenzi wa nyumba ya kuishi kila mtu anakuwa na ramani yake. Kitu cha msingi lazima uangalie hilo banda unataka kulijenga sehemu gani, maana kila mahali kunatofautiana hali ya hewa, kuna maeneo mengine yana baridi kali mfano Iringa na kilimanjaro wakati mengine yana joto mfano, maeneo ya Pwani. Ujenzi wa mabanda katika maeneo hayo lazima utatofautiana.

Lakini unapojenga mabanda kitu cha msingi lazima uwe na chumba cha stoo, uwe na brooder ambacho chumba maaalum cha kutunzia vifaranga, na pia uwe na vyumba vingine vya kufugia kuku.

Unapaswa kuzingatia kwamba, lazima kabla ya kuanza kujenga mabanda yako ya kuku, ujue unataka kufuga kuku wangapi. Kujua idadi ya kuku itakupa itakupa uelewa wa ukubwa wa mabanda utakayoyajenga na eneo linalohitajika kujenga mabanda hayo.
 

mkuu asante kwa ushauri wako mzuri.mimi banda langu nataka kulijenga kilimanjaro wilaya ya rombo pia nataka kuanza na kuku 50 na lengo langu ni kufikia kuku 1000.pia hiyo brooder inatakiwa kuwa vipi mkuu kwa kuzingatia hali ya baridi kule rombo
 
Jamani mi bado natafuta mayai ya kuku wa kienyeji wenye uwezo wa kuatamia wenyewe. Nahitaji tray 4 kuweka kwenye incubator mwenye nayo. Napatikana Dar es salaam.
Au waweza nisaidia pia kwa kuniambia wenye nayo
 
de Marco,
Mimi binafsi nilikuwa nakushauri hebu concentrate kwanza kwenye kitabu ufugaji ufuate kwa sasa wewe endelea tu kujifunza zaidi kuhusu kuku ili utakapoanza ufugaji utakuwa na elimu ya kutosha kukuwezesha ufuge kwa ustadi.

Je naweza pata hicho kitabu cha ufugaji
 
mi naitaji kufuga kuku wa nyama chotara 200 na wamayai 100 kwa kuanzia.Nina shilingi laki tano naitajika niongeze kiasi gani katika huendeshaji ukiacha gharama za banda include chakula cha kuku wote na dawa zingine
 
Jamani mi bado natafuta mayai ya kuku wa kienyeji wenye uwezo wa kuatamia wenyewe. Nahitaji tray 4 kuweka kwenye incubator mwenye nayo. Napatikana Dar es salaam.
Au waweza nisaidia pia kwa kuniambia wenye nayo

Mheshimiwa andybird314,
Kama utapata shida sana namna ya kuyapata mayai hayo ya kutotolesha unaweza ukanunua kuku wako kama 50 na ukawafanya kama kuku wazazi watakaokupatia mayai kwa ajili ya kuyaatamisha.
 
Mmh njopino mkuu hapo bado sana kwa kuku wa nyama 200 tu bei take 1,400@1 sasa piga MWENYEWE hata hapo mayai 1,300@1+ kwa wengine 1,400@1 SSA piga kwa idadi unayotaka mmh hapana chagua moja kama unataja bei yako kuwa makini kwani nahii unataka kufahamu ...jipange mkuu halafu mtafute mtaalamuuu...
 
Usajili kwa ajili ya semina ya kuku Dar es salaam katika ukumbi wa Landmark hotel unaendelea karibu sana.
 
Mkuu nitumie namba kwani nahitaji semina hiyo kwakuwa nilianza na kuku 100 mwaka huu mwanzoni ila sasa nina fuga mpaka 800 tena nafuga kwa i - i naona maendeleo mazuri wala sihitaji ajira kwani nimeweza nimeanza kuona mafanikio lakini nahitaji kujifunza kutoka kwa wengine pia kufahamu na kutoa huduma nzuri kwa wateja /nitumie namba ya kujisajili na gharama zake pia tafadhali sana....
 
Heshima mbele wadau ,

Naomba muongozo wa cage za kuku wa Mayai na possible bei zake; Nipo Dar

Asante sana
 

nataka nianze kufuga kuku..naomba nijue kati ya kuku wa nyama na mayai bora ipi ,na mtaji wake sh ngapi..masaada please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…