Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 961
- 533
Bwana Tuliponga,Kwa kuku wa kienyeji kabisa ambao siyo chotara na ambao wanafugwa kienyeji kama vile ambavyo wananchi wengi na hasa wa kijijini wanavyo wafuga kwa kuwaachia wakijitafutia chakula wenyewe.Je ni mtiririko gani wa kimatibabu unatakiwa ufuatwe ili kuwa kinga kuku na magonjwa tangu wakiwa vifaranga?.Je ufugaji wa aina hii unaweza ukatumika kwa kuku wa kienyeji ambao ni chotara endapo taratibu zote za kimatibabu zitafuatwa?.
Kuku wa kienyeji ni wastahimilivu sana dhidi ya magonjwa. Mara nyingi kuku wakienyeji wanaofugwa na watu wa vijijini hawawajali sana katika mtibabu na ndio maana unakuta mfugaji kwa muda fulani anakuwa na kuku wengi lakini baada ya muda tena kuku wote wanakufa kutokana na magonjwa.
Hata hivyo wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji wanazingatia sana chanjo sana sana ya ugonjwa wa mdondo/kideri /kipetupetu kama ambavyo unavyojulikana kwa majina mengi na wafugaji wengi katika maeneo tofauti tofauti. Kifupi ugonjwa ni mmoja lakini majina ni mengi.
Kuku wa kienyeji wanahitaji huduma zote wanazopatiwa kuku wa kisasa kwakuwa magonjwa anayopata kuku wa kisasa hata kuku wa kienyeje naye anayapata. Kimsingi magonjwa ambayo yanawatesa sana kuku wa kienyeji ni pamoja ugonjwa mdondo, ugonjwa mafua, minyoo, Vidudu visumbufu mfano viroboto, utitiri, na chawa, ugonjwa ndui, taifodi, kipindupindi pamoja na ugonjwa wa kuharisha damu (coccidiosis)
Kama mfugaji atafuata ratiba kamili ya chanjo pamoja na kinga kwa kuku hawa wa asili, hakutakuwa na vifo vyovyote vitakavyotokea kwa kuku wake hata kama wakifugwa katika mazingira ya kuachiwa huru wakijitafutia chakula chao wao wenyewe. Kitu kimoja cha msingi cha kuzingatia ni kwamba eneo ambalo wanaachiwa huru lazima liwe limezungushiwa senyenge ili kuku wasiende mbali sana wakapata kuliwa na wanyama waharibifu mfano vicheche, paka, mbwa nk.
Dawa kwa ajili ya chanjo na kinga zinapatika madukani.
