Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Jamani wana jamii jama nilikuwa mmojawapo wa watu tuliohudhuria semina iliofanyika landmark hotel, kwakweli tumejifunza mengi sana kwenye biashara hii, nashauri ziwe zinafanyika after miezi mitatu mitatu ili kupata uelewa zaidi, big bip kwako AMAN na waandaaji kwakweli tumefaidika na semina! yani nimegundua kumbe mahitaji ya kuku ni makubwa lakini ni sie WATZ ni kutokujipanga, tunafanya mambo yetu
kilocal sana, tukiwa serious especially kwa kuunganisha mitaji kama wenzetu Kenya etc nahisi tutafika mbali sana basi tu, natumai wengi wamejifunza kitu fulani..

 
Habarini wana JF,
Napenda kuwashakuru wadau wote waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya ufugaji wa kuku, masoka na mitaji. Kwa kweli ilikuwa ni semina ya aina yake kuwahi kufanyika mkoani DSM. Katika semina hiyo tulipata pia fursa ya kufhamiana nje ya jamii forum. Shukrani za pekee ziende kwa shirika la Communication Solution kwa kuweza kuandaa tukio kubwa kama lile.

Masomo yaliyofundishwa ni mengi na yenye tija kubwa kwa wafugaji. Katika semina hiyo, kitabu cha mwongozo wa ufugaji bora wa kuku kiliuzwa kwa ofa ya sh elfu 20 tu badala ya sh elfu 60 bei yake ya halisi. Formula mbalimbali za kutengeneza chakula cha kuku na namna ya utumiaji wake, malighafi zilizotumika, uandaaji wake na upatikanaji ziligaiwa kwa wanasemina. Ilisisitizwa kuwa inalipa kutengeneza chakula mwenyewe. Gharama ya chakula inakuwa ndogo ukilinginisha na chakula cha kununua.

Kwa ambaye hakupata fursa ya kuhudhuri mafunzo hayo Communication Solution waliweza kulirecord tukio lote kwa kutumia wapiga picha wa Benchmark Production kusudi kuwanufaisha wote ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo. DVD hizo zinapatikana kwa shilingi elfu 10 tu. Kwa yeyote ambaye atahitaji DVD Hiyo basi awasiliane na Communication Solution kwa simu namba 0655663900.


Elimu ina thamani katika ufugaji wa kuku wenye tija.
 
nimeona wafugaji kuku wa mayai wanalalamika msiba wa kuingia mayai kutoka nje ya nchi. wafugaji wa kuku wa nyama mtuambie je soko liko salama kwa sisi wafugaji watarajiwa??
 
Kama ni kweli kuwa soko la mayai limevamiwa na mayai toka nje basi ni fedheha na aibu kubwa. Ina maana hapa serikali imelala, vyombo vya usalama na TRA mipakani vimelala au ndio athari za rushwa na kuweka watendaji wasiojua wajibu wao. Ni fedheha na aibu kubwa , sasa mzungu akisema hatuwezi kujitawala tutasema anatutukana?.
 
nawezaje kupata mawasiliano yako na hatimae kuonana na wewe ndugu ili kuweza kupata somo zaidi na hyo hard copy itakayoweza kuniongoza kufikia malengo tarajiwa na endelevu? Tizo 1

Nakushauri ufuge kuku wa kienyeji. baaaas
 
Last edited by a moderator:

hatuwezi kujitawala kabisa. ila tusiilaumu TRA inawezekana yaingia kihalali kwa kufuata taratibu zote
 

Dr. Nahitaji hiyo DVD aisee...
 
Mtaji sio tatizo, sehem sio tatizo, tatizo ni mtu wa kumkabidhi shughuli hy mnk sina muda wa kukaa huko shamba, unao vijana wazuri?
 
Mtaji sio tatizo, sehem sio tatizo, tatizo ni mtu wa kumkabidhi shughuli hy mnk sina muda wa kukaa huko shamba, unao vijana wazuri?

Ngosha,
Kwa kushirikiana na shirika la Ndurumo, tunaendesha mafunzo kwa vijana wa kitanzania wenye ari ya kufanya kazi kwa weredi na kujituma. Hawahitaji kusukumwa katika kutekeleza majukumu yao, ni waaminifu, wachapakazi na wanaojua wajibu wao. Tunawafundisha namna ya kuwahudumia kuku hatua kwa hatua, udhibiti wa magonjwa na kuyajua magonjwa hatari ya kuku dalili zake, kuenea kwake na namna ya kuyazuia. Pia huwa tunawapeleka kwenye mafunzo kwa vitendo katika mashamba mbalimbali ya watu ambao tunawasimamia miradi yao kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi.

Vijana hawa kwakweli wanaopenda kazi, siyo wavivu, wapo wanaotoka kigoma, ambao huwa wao hupenda kufanya kazi kwa mkataba, kwamba wanaweza wakakufanyia kazi kwa muda wa mwaka mzima bila kudai malipo yoyote kisha mwisho wa mwaka ukawlipa mishahara yao yote kama lump sum. Wengine kutoka Songea, Iringa na dodoma nk.

Kwa kuwa tunawafanyia training, kila ambaye atawahitaji atawalipia laki 2.5 kwa kila kijana mmoja kama gharama za mafunzo.

Ikiwa una kijana/vijana wako, na ungependa wawe weredi katika kusimamia na kuhudumia kuku unaweza kumlete/kuwaleta kwetu na tukawapatia mafunzo ya ufugaji bora wa kuku, mafunzo hayo hufanyika kwa muda wa wiki 4, wiki moja darasani na wiki tatu nyingine wanakuwa field/ mafunzo kwa vitendo.

Kijana mmoja anauwezo wa kuwahudumia kuku 1000 kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kudhibiti. Wako tayari kufanya kazi kwa mshahara wa laki moja wa kuanzia

Kama utahitaji pia vijana wenye certificate za afya ya wanyama na uzalishaji unaweza ukawasiliana nami na utawapata vijana hao ambao ni weledi katika tasnia ya mifugo. Siku zote rahisi ni ya ghali.
 
Ok... mafunzo yanaaza lini? Na hiyo ada uliyotaja hapo juu inajumuosha kila kitu, kwa maana ya malazi na chakula kwa wanaotoka mbali?
Malazi na chakula ni juu yako. Ikumbukwe kuwa haya ni mafunzo tu ya kukujengea uwezo kijana ambaye ungependa pindi ukiajiliwa au kujiajiri mwenyewe uweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Mara nyingi mafunzo haya huwa tunayafanya kwa mahitaji maalum.
 
Mkuu Aman, je ninaweza kuchanganya kuku chotara na wale wa kienyeji pure kwenye banda moja? Kuna hasara yoyote kufuga kuku wa kienyeji na bata kwenye eneo moja. Asante kwa ushirikiano
 
Mkuu Aman, je ninaweza kuchanganya kuku chotara na wale wa kienyeji pure kwenye banda moja? Kuna hasara yoyote kufuga kuku wa kienyeji na bata kwenye eneo moja. Asante kwa ushirikiano

Kitaalamu hatushauri kuchanganya kuku wa breed tofauti. Kuku wa kienyeji wafugwe kwenye banda lao na kuku chotara kadhalika. Kuku wa kienyeji ni wastahimilivu zaidi katika magonjwa ukilinganisha na kuku chotara. Pia kuku wa kienyeji wakati mwingine wanakuwa carrier wa magonjwa bila wao kuathirika.

Inapendeza bata wakafugwa kama mita 30 kutoka kwenye banda la kuku
 

Asante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…