Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Coaster mzee mfuko mdogo! hapo parefu kidogo mzee!!! 40m kwa mwajiriwa ni parefu kidogo

Kijana kama uko serious na kuku unafanikiwa haraka sanaa;

Mfano kwa experience yangu,with CP Broiler chicks (CPF DOC) 500,unakuja kupata profit kati ya 500K to 700K iff mgt yako itakuwa nzuri sanaa,mortality ikiwa ndogo sanaa. For CP Layers chicks,na ukawapa chakula cha CP watataga vizuri sanaa,week ya 22 utaanza kurudisha cost zako,per month kwa kuku wa mayai 500,utakusanya c chini ya milion moja (income b4 deduct feeds cost of that month),so its like 50% of income ndio profit yako.

Unaweza nicheck kwenye deograts@gmail.com tuongee kiundani zaidi
 

Attachments

Wadau nimefurahishwa na nimenufaika sana na hii topic.
Nami nitaomba kuwasiliana nawe Mr Aman ili unipe mwanga zaid.
 
Naomba kufahamu ,nimeona Jogoo kubwa la kuku wa kienyeji ana mdomo mfupi, hawa wanapatikana wapi, wanaitwaje? .
 
Naomba kufahamu ,nimeona Jogoo kubwa la kuku wa kienyeji ana mdomo mfupi, hawa wanapatikana wapi, wanaitwaje? .

Nadhani hao watakuwa ni majogoo wa kuchi ambao wanapatikana zaidi katika mikoa ya Singida na Tabora.
 
Wadau heshima kwenu! Nina kuku wa kienyeji kama 50 hivi, majuzi nimeongeza wengine kama kumi hivi kumbe miongoni mwao wana uambukizo wa ndui,naomba ushauri nitumie dawa/chanjo gani,pili wachache macho yamepata uambukizo mpaka yameziba hawaoni kabisa, please naomba msaada kutatua matatizo haya,natanguliza shukrani
 

Mkuu pole sana kwa tatizo hilo. Kosa la kwanza kubwa ulilolifanya ni kuchanganya kuku wageni na hao wa zamani. Ukinunua wakati mwingine watenge kwanza hao wapya peke yao ikiwezekana kwa wiki 2 huku ukihakikisha wanapata chanjo zote zinazostahili. Hii itakusaidia kupunguza uwezekano wa kuku wageni kuwaletea ugonjwa kuku wako wa zamani.

Kwa ugonjwa wa ndui nijuavyo mimi ni kwamba hauna tiba kwa sababu unatokana na virus. Kilichopo ni chanjo ya sindano ambayo huchomwa kwenye mabawa lakini hii inapaswa kufanyika kabla kuku hawajapata ugonjwa. Kwa hao ambao wameshaugua tayari unapaswa tu kuwasaidia kwa kusafisha hivyo vidonda vyao na unaweza kuwapakia mafuta mazito kwa mfano samli kwenye hivyo vidonda baada ya kuvisafisha. Waweza wapa pia antibiotics kama OTC 20% kwa ajili ya kusaidia uponeshaji wa hivyo vidonda.
 

nashukuru kiongozi kwa ushauri huu muhimu,asante sana
 

Mkuu inaonekana una uzoefu..nimependa..unafugia wapi Mkuu nipate kujifunza..
 
Mkuu inaonekana una uzoefu..nimependa..unafugia wapi Mkuu nipate kujifunza..

Hapa hapa Dar es Salaam,maeneo ya kitunda,unaweza nipata kwenye no 0717332652.Ufugaji wa kisasa hapa Tanzania umekuwa sana,kuja kwa CPF COMPANY kumefanya mapinduzi makubwa sana,kuanzia chakula bora mpaka vifaranga bora ambavyo ni rahisi kufuga,havishambuliwi na magonjwa coz wanakushauri jinsi ya management,pamoja na ubora wa chakula pia is the major factor
 

Attachments

  • 1421466662044.jpg
    89.4 KB · Views: 656
  • 1421466683943.jpg
    80.7 KB · Views: 630
  • 1421466697432.jpg
    74.9 KB · Views: 618
Kwa sehemu za temeke wapi kuna vifaranga wazuri(broiler)????
 
Naomba kama kuna mtaalamu wa ufugaji kuku wa kienyeji na kisasa aniambie ni kuku yupi anatumia gharama kubwa katika matunzo na yupi anaongpza kwa faida.
 
Naomba kama kuna mtaalamu wa ufugaji kuku wa kienyeji na kisasa aniambie ni kuku yupi anatumia gharama kubwa katika matunzo na yupi anaongpza kwa faida

Kwenye Red hapo, ukianza na haya mawazo jaindae kuacha ndani ya miezi michache sana, nini kitatokea endapo hutapata hiyo faida unayo itegemea?
 
Mkuu Chasha Poultry Farm. Pamoja na kuuliza kwa namna isiyopendeza, hicho pekee ndicho ulichoweza kumjibu? Naamini una majibu mazuri zaidi ya hayo (nimesoma michango yako mingi; inadhirisha uwezo wako mzuri katika mijadala).

Juu ya yote, nami pia ningependa kujua masuala ya ufugaji kuku. Natarajia karibuni kuanza kufuga kuku wa kienyeji kisasa. Kama hautajali ukatuhabarisha ndugu zako nitakushukuru sana.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu boy future na Baba Mkali, angalieni hapo juu kwenye hizo nyuzi ambazo zimewekwa sticky kwenye jukwaa hili la ujasiriamali. Kuna habari nyingi sana hapo za ufugaji wa kuku kama mtaweza kupitia michango yote iliyomo humo ndani.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…