Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Wapendwa nahitaji kufuga kuku wa kienyeji na ninao kama kuku 10 sasa nahitaji wawe na banda imara na la kisasa sasa sijajua ni vifaa vp vinahitajika ktk banda na ni chakula kipi chenye kufaha
 
 
Songea muna branch au mutakuja lini kwenye semina?
 
Songea muna branch au mutafika Lin kwa ajili ya Mafunzo?
 
Tufuge wa kienyeji best na madawa yao ya kienyeji, naamini ni rahisi kuwafuga
waeleze jamani
 
Kwa uzoefu wako kuku 200 wa mayai wanaweza kula mifuko mingapi ya chakula kwa siku moja?? Msaada kwa yeyeto anaefahamu maana nataka nianze shughuli ya ufugaji
 
Tufuge wa kienyeji best na madawa yao ya kienyeji, naamini ni rahisi kuwafuga
Uko sawa kabisa ila inachukua muda kutoboa.

Ukiwa na mahali pa kufugia, ukatenga laki tano tu kwa ajili ya kununua kuku na chakula cha kuanzia ndo utaweza kutoka ndani ya mda mfupi. vinginevyo safari ni ngumu.
 
wapendwa habari! Naitaji mayai ya kienyeji naitaji tray 20 kwa ajili ya kutotolesha
 
UFUGAJI WA KUKU KIBIASHARA

Ili Mfugaji aweze kufanikiwa katika ufugaji wake wa kuku ni lazima kwanza ahakikishe kuwa gharama za ufugaji zinazipungua. Kuna gharama nyingi ambazo kimsingi mfugaji anaziingia pasipo na sababu zozote za msingi. Gharama za ufugaji zinapokuwa kubwa zinapunguza tija ambayo mfugaji angeweza kuipata

Ili kuweza kupunguza gharama, hakikisha kuwa unapata feeding program ya kuku wako ili isaidie kukuongoza katika ulishaji wao. Vile vile punguza matumizi yasiyo ya lazima ya madawa. Ni kawaida kukuta mfugaji wa kuku emekithirisha matumizi ya madawa kwa kuku wake. kila siku madawa na kuku kuku na madawa matokoe yake madawa hayo hugeuka kuwa sumu katika mwili wa kuku kutokana yale mabaki ya madawa. Wakati mwingine madawa hayo yanakuwa makali na kuwaathiri viungo vyao muhimu vya ndani mfano Maini, mapafu na moyo. Utumiaji wa madawa uliokokithiri licha ya kuleta hasara katika ufugaji lakini pia kunapunguza umri wa maisha ya kuku ambao angeweza kuishi. Sasa kama kuku ni mtagaji huwezi iona ile faida ya utagaji wake kwa kuwa kuku watakuwa wamekufa kabla ya kumaliza muda wao wa utagaji.

Lakini vile vile kwenye chakula, mfugaji anaweza kupunguza gharama kwa kujitengenezea mwenyewe chakula cha kuku wake. Ni muhimu kuhakikisha kuwa inapatikana formula nzuri itakayotumika kutengenezea chakula hicho. Ili kuhakikisha kuwa gharama za utengenezaji wa chakula hicho kinakuwa chini zaidi ni lzima mfugaji akanunua malighafi au viwambajengo vya kutengenezea chakula hicho wakati wa msimu wa mavuno. Kama tujuavyo wakati wa msimu wa mavuno, malighafi za kutengenezea chakula cha kuku, hasa nafaka ambazo ndiyo zinazotumika kwa kiwango kikubwa, zinakuwa ziko chini. Chakula kikitengenezwa kwa gharama nafuu husaidia kuongeza faida katika ufugaji.

Mwisho hakikisha kuwa udhibiti wa vifo vya kuku unafanyika kwa kufuata kanuni bora za ufugaji. Vifo vinaongeza gharama za ufugaji kutokana na kutumia madawa mengi ya kutibu. Kuku anapokufa tafsiri yake ni kuwa, huenda akawa anaumwa au vinginevyo, lakini ikiwa kufa kwao kunatokana na mlipuko wa ugonjwa hapo ndipo mfugaji atakapotumia gharama kubwa ya madawa ili kuwanusuru kuku wake wasiendelee kufa. Vifo vya kuku vinapunguza faida katika ufugaji wa kuku.

Kwa ajili ya kupata Feeding, Vaccination and Prophylaxis programs, Formula za utengezaji wa chakula bora cha kuku, Processing za malighafi za kutengezea chakula cha kuku, Namna ya kuanzisha na kuendesha mradi wa utotoleshaji wa vifaranga, utibuji wa mayai kabla ya kutotoleshwa na faida zake, changamoto katika ufugaji wa kuku na namna ya kuzitatua na mambo mengine mengi, tunakukaribisha katika Semina ya Ufugaji wa Kuku Kibiashara, ufugaji wa kuku kama kazi, Kuku ni pesa unahitaji kuweza katika ukumbi wa THE AFRICAN DREAMS HOTEL DODoMA maeneo ya AREA D jirani na Royal Village Hotel siku ya Tarehe 16/07/2016

Imeandaliwa na:

AMAN NG'OMA
KINASORU EAST AFRICA (T) LTD
SIMU NA. 0767989713, 0786989713,0715989713
NDUKA STREET, CHAMWINO BONANZA
DODOMA MJINI.

PIA UNAWEZA KUWASILIANA NA
SUFIANI MAKANDO
KILIMO COMMUNICATION SERVICES CO. LTD
SIMU NA.0755436412
MOROGORO
 
Nimetuga kuku wa kienyeji wamefika 60 sasa at first it was fun lakini sasa nataka kujikita kama biashara, lakini nisilolijua ni kuondoa hayo mayai pindi wanapotaga, maana kila siku nakuta mayai.

Je hayo mayai yanakaa mda gani bila kuharibika? Nihifadhi vipi kama siku zinapishana za mayai?
Hapo ndio nakuta mengine yamekuwa yai vinza.
Swali la pili nikihitaji mayai kwenu mnitumie yatakuwa Salama kwa mda gani kabla ya kuwawekea kuku watotoleshe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…