Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

chanjo na tiba ni vitu vi2 tofauti kuku hungingwa na maradhi kwa njia kuu 5

1.usafi wa banda na vyombo vya chakula

2.chakula bora chenye
virutubisho vyote vinavyo stahili

3.maji ya kutosha yaliyo saf na salama tibu maji kwa (water gurd) au chemsha

4.kuzingatia chanjo tena kwa wakati maana magonjwa meng ya kuku ni vigum kutibika

5.banda lenye nafasi na hewa ya kutosha
 
Msaada naombeni mniunge makundi ya Whatsapp simu iliibiwa kwa namba +255712227885na telegram +255654444064
 
jamani habari zenu!hivi eka moja kwa ufugaji huria kitaalamu inachukua kuku wangapi?maana nataka niexpand mradi wangu wa kuku
 
Teknolojia mpya ya ukweli na nafuu sana ya kutunzia vifaranga
 
Attachments

  • 1470993303524.jpg
    93.2 KB · Views: 252
Nahitaji kupata mawazo ya msingi juu ya ufugaji serious wa kuku wa kienyej kwa ajili ya biashara, I mean nataka kumiliki kampuni ya kuku wa kienyej, namba yangu ya whatsaap Ni 0712093626. Please mdau ameniambia niandae proporsal.
 
Jamani hii thread nimefatilia kwa mda kiongozi Aman Ngoma
Naomba tuwasiliane na kama kuna magroup ya whatsapp kuhusu hili swala ntashukuru kujumuishwa
Number yangu ni 0654908122
 
Jaman kama kuna mijadala mbali mbali ya whatsaap em na mimi nawaombeni mniadd, namba zangu Ni 0712093626.
 
Bei ya kifaranga wa broiler ikoje ss hv jamani?
1800
2000
2500

hizi ni bei za kifaranga cha cku moja tofauti ya being hizi ina fatana na wapi unapo nunua na aina ya vifaranga na ubora wake
 
Wakati wa kufuga ni muhimu kuku wapate sehemu ya wazi wanayoweza kutembea kwa uhuru. mfugaji mwenye lengo la kufuga kuku wengi wenye umri mmoja na kupata mayai mengi au aweze kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja wenye umri unaolingana inabidi uwe na vifaranga wengi wa umri mmoja.

Kuwa na vifaranga wengi wa umri mmoja kuna faida nyingi ikiwa ni pamoja, kupunguza gharama za ufugaji kwa mfano chanjo na tiba, kutunza kuku kitaalamu kwa urahisi, kupata mayai mengi kwa wakati mmoja, kuuza kuku wengi kwa wakati mmoja, na kuwapa uhakika wateja.

kuna njia kuu mbili za upatikanaji wa vifaranga wengi kwa wakati mmoja nazo ni;
Kwa kuwaatamisha kuku wengi kwa wakati mmoja Kwa njia ya mashine ya kuangulia (incubator) Njia hizo zinaweza kumwezesha mfugaji apate vifaranga bora. Uchaguzi wa njia ipi itumike utatokana na mtaji wa mfugaji na mahali alipo. Njia ya kuatamisha inatumika kwa tetea wengi kuatamishwa kwa wakati mmoja hivyo mfugaji anatakiwa achague mitetea, mayai, aandae viota, maji na chakula bora.
Sifa za tetea wa kuatamia
Kuku mwenye umbo kubwa Mwenye uwezo na historia nzuri ya kuatamia na hatimaye kutotoa vifaranga.
Sifa za mayai ya kuatamisha
Mayai ya siku ya mwisho kutagwa ndio yawe ya kwanza kuwekwa yafuatiwe na ya siku zinazofuata yasizidi wiki mbili tangu kutagwa. Lisiwe kubwa sana au la duara, lisiwe na uvimbe. Yasiwe machafu wala yasiwe na nyufa.

Sifa za kiota na chumba cha kuatamia Kuku wanaoatamia watengwe katika chumba ili kuondoa tatizo la kutagiana. Mlango na dirisha viwekwe wavu ili muda wa mchana mwanga na hewa viweze kuingia.

Chumba kiwe na nafasi ya kutosha kuweka viota, chakula na maji. Ili kutumia eneo vizuri viota vinaweza kutengenezwa ukutani kama mashelfu. Viota viundwe vizuri kwa nyasi, maranda makavu ya mbao, au nguo ya pamba lakini isiyo tetroni. Viota visiwe sehemu yenye unyevunyevu.

Idadi ya viota vilingane na idadi ya tetea waliochaguliwa kuatamia. Vinyunyiziwe dawa ya kuuwa wadudu { Akher powder} ukiwemo utitiri kwa kuwa ni wasumbufu hivyo husababisha kuku kutokatoka nje na kupunguza uwezekano wa mayai kuanguliwa yote.

Kuku wanaoatamia wapewe chakula cha kutosha cha kuku wakubwa wanaotaga. Majani, mboga na maji ya kunywa ni muhimu kwa kuku hao. Vyote hivyo viwekwe kwenye chumba kinachotumika kuatamia kuku asiende umbali mrefu kutafuta chakula na kuyaacha mayai kwa muda mrefu.
Hatua za kuatamisha kuku
Kuandaa viota, uchaguzi wa tetea bora na kuandaa mayai. Tetea wa kwanza akianza kuatamia muweke mayai yasio na mbegu ama viza( nakumbuka nilisha zungumziaga hili hapa hapa jf) . Rudia zoezi hilo mpaka itakapofikia idadi ya kuku unaowahitaji. Baada ya kupata idadi ya kuku wawekee mayai yenye mbegu. Kuku wote waliochaguliwa kwa ajili ya kuatamia wawekwe wakati wa usiku kwa sababu ya utulivu uliopo. Kwa kupitia njia hiyo kuku mmoja anaweza kuatamia hadi mayai 20 kwa kuzingatia sifa zake.

Baada ya kutotoa hatua ya awali ni uleaji wa vifaranga. Kuku wazazi hutengwa na vifaranga. Vifaranga hupewa joto na mwanga kwa kutumia taa ya umeme, jiko au kandili. Maji yenye glucose kwa ajili ya kuongeza nguvu, na chakula ni muhimu kwa vifaranga hao.
Changamoto Huhitaji sehemu kubwa kwa sababu ili upate vifaranga wengi unahitaji kuku wengi wanaoatamia. Kuwepo kwa wadudu kama utitiri na kutopatikana kwa chakula cha kutosha husababisha kuku kutoka toka nje na kusababisha mayai kuharibika.

Kuku kupata magonjwa wakati wanapoatamia.
Kutokuwa na kipimo cha kupimia mayai yaliyo na mbegu Jambo lingine muhimu kuzingatia ni chanjo. Wakati wa kutayarisha mpango wa kuchanja kuku kwa ajili ya kinga dhidi ya magonjwa kuna vipengele sita vya kuzingatiwa.

1. Vifaranga vinavyoanguliwa kwa pamoja:
Iwapo kuna kundi zaidi ya moja la vifaranga wanaoanguliwa, mfugaji aweke utaratibu wa chanjo utakaopunguza uwezekano wa kuenea magonjwa.

2. Umri wa kuchanja kuku:
Kwa kuku ambao wanatarajiwa kutaga mayai au kuwa kuku wazazi, chanjo nyingi hutolewa si zaidi ya mwezi mmoja kabla ya kuku kuanza kutaga.

3. Magonjwa makuu katika eneo husika:
Ni muhimu sana kuelewa magonjwa ya kuku yaliyopo katika eneo lako kabla ya kuandaa programu ya uchanjaji, kwa magonjwa ambayo chanjo zenye vimelea hai hutumika.

4. Hali ya kiafya ya kuku watakaochanjwa: Usiwape chanjo kuku ambao wanaonesha dalili za kuathirika kwa mfumo wa hewa au wanaonesha kuwa na minyoo au wadudu wengine. Kwa kuku walio na dalili hizo chanjo zinaweza kuleta madhara.

5. Aina ya kuku watakaochanjwa: Kuku wanaofugwa kwa ajili ya nyama wanahitaji kinga ya muda mfupi, hivyo chanjo moja inaweza kutosha. Kuku wa mayai na kuku wazazi wanahitaji mpango wa chanjo itakayowakinga na magonjwa kwa kipindi chote wanapokua na kutaga.

Historia ya magonjwa katika banda Kabla ya kuandaa mpango wa chanjo, lazima ufahamu ni magonjwa gani yaliyoenea katika shamba. Kama unataka kuingiza kuku wapya kutoka mahali ambako ugonjwa umeshawahi kutokea, kuku hao wachanjwe wiki 3 kabla ya kuwaingiza bandani. Iwapo utatumia chanjo yenye vimelea hai, hakikisha kwamba magonjwa hayo yameshawahi kutokea katika banda husika.

Usitumie chanjo hizo katika shamba ambalo ugonjwa huo haujawahi kutokea au kutambuliwa. Wasiliana na wafugaji jirani kufahamu iwapo wanatumia chanjo zenye vimelea hai.

• Hakikisha unazingatia kwa makini masharti ya mtengenezaji wa chanjo: Jinsi ya kuhifadhi, kutayarisha na njia inayotumika kumchanja kuku. Wakati wote zingatia masharti ya mtengenezaji kuhusu uhifadhi wa chanjo ili isipoteze nguvu.

• Fuata ushauri wa daktari wa mifugo unapoandaa mpango wa chanjo

•Watumie wataalamu waliopatiwa mafunzo ya utoaji chanjo

• Chagua aina ya chanjo kulingana na umri na hali ya kiafya ya kuku

• Fanya usafi wa mara kwa mara katika mabanda ili kupunguza wingi wa vimelea kwenye mazingira

• Tumia maji ambayo hayajawekwa dawa au kemikali kwa ajili ya kuchanganyia chanjo, kwa mfano maji ya kisima, mvua na kadhalika. Maji ya kuchanganyia chanjo yawe na ubaridi, yasiwe moto.

• Changanya chanjo kabla ya kutumia na iwekwe mbali na kuku.

• Pata ushauri wa daktari wa mifugo kabla ya kuchanja kuku wagonjwa au wale ambao hawako katika muonekano mzuri.

• Siku ya chanjo, usiwape kuku maji kwa saa 3 – 4 ili waweze kunywa maji yaliyowekwa chanjo kwa haraka. • Zoezi la uchanjaji lifanyike haraka ili kupunguza usumbufu kwa kuku.

• Tenganisha kuku waliochanjwa na wale ambao hawajachanjwa.

• Baada ya kuchanjwa, kuku wawekwe kwenye banda linalopitisha hewa vizuri.

Lakini pia katika mfumo huu una faida na hasara. Hasara ntazielezea pia

Kwa ushauri zaidi 0673296942

Nasikia kuna chanjo ambanzo huwa zinatolewa mara baada ya kifaranga kuanguliwa,hizo chanjo zinaitwaje?na kwa mtu anayetegemea kutotolesha vifaranga kwa kutumia kuku wazazi anaweza akazipataje?.
 
Asante Mkuu Donata
Nimekuelewa Vizur Lakin Hizo points zinawafaa wa mjin zaidi kuliko sisi wa vijijin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…