Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Darasa ni zuri sana,

Wakuu nawashauri hivi, kwa wanaotaka kufanya investments (ufugaji,bustani za mboga, misitu) ni vizuri ukijenga utamaduni wa kutembelea kwa wenzio walioanza na wanaoendelea ili uone kwa vitendo. Wakati mwingine unaweza ukajenga hofu bure kumbe mambo yanawezekana kabisa. Vitendo hufundisha zaidi.

Kuku wanalipa ndugu zangu.
 
kaka el-nino mie pia huwa na interest na ufugaji nikiamini kwa kutumia kijishamba changu hapo bagamoyo nitakuwa na reason ya kila weekend kwenda shamba na familia

sema nimekuwa na kiu sana ya kuwa na mashine ya kuangulia vifaranga na nyingi zinatumia umeme sasa ulivyosema ipo ya mafuta ya taa nimetamani kutimiza kiu yangu ili niinunue...inauzwaje na inauwezo wa kuangua mayai mangapi kwa muda gani...nisaidie mkuu information hizo ili nirudi kwenye mchanganuo wangu wa biashara ....DOKEZO...kuku wa kienyeji aina ya kuchi au wale vishingo wakubwa ni biashara tosha na wana soko kubwa sanaa...tuchangamkie aina hiyo ya kuku..wanapatikana singida na manyara

Nitapita ktk mikoa hiyo karibuni... nitajaribu kudodosa nipate cha kuleta humu:thinking:
 
kaka el-nino mie pia huwa na interest na ufugaji nikiamini kwa kutumia kijishamba changu hapo bagamoyo nitakuwa na reason ya kila weekend kwenda shamba na familia

sema nimekuwa na kiu sana ya kuwa na mashine ya kuangulia vifaranga na nyingi zinatumia umeme sasa ulivyosema ipo ya mafuta ya taa nimetamani kutimiza kiu yangu ili niinunue, inauzwaje na inauwezo wa kuangua mayai mangapi kwa muda gani...nisaidie mkuu information hizo ili nirudi kwenye mchanganuo wangu wa biashara. DOKEZO: kuku wa kienyeji aina ya kuchi au wale vishingo wakubwa ni biashara tosha na wana soko kubwa sanaa...tuchangamkie aina hiyo ya kuku..wanapatikana singida na manyara

REDS: Nitapita katika mikoa hiyo karibuni. Nitajaribu kudodosa nipate cha kuleta humu:thinking:
 
Habari wakuu:

Bila shaka kuna watu ambao wanafuga kuku au walishawahi kufuga kuku. Naomba watu wenye uzoefu na maarifa kuhusu kufuga kuku,,wanipe mawazo,,,maana nataka kuanza kufuga kuku na sijawahi kufanya hivyo. Hivyo nahitaji mawazo yenu wakuu.

Natanguliza shukrani zangu wakuu:

At the end of the day pamoja na maelekezo mazuri utakayopewa akili kumkichwa - angalia soko, fanya cost benefit na risks analysis.

Mfanya biashara wa Singida au Dodoma anaweza kufanikiwa vizuri kwenye hii biashara wakati yule wa Tanga au Kigoma wasifanikiwe sababu zikawa ni pamoja na gharama za kuwafikisha vifaranga pale walipo ni juu, pengine by the time wanawapata % fulani wamekufa, na pia soko lisiwe zuri kwa vile wenyeji wanaprefer samaki na bei ya samaki pengine ni ahueni zaidi ya kuku.

All the best
 
Nimeanza majaribio ya ufugaji kuku wa kienyeji na vijogoo, lakini tatizo kubwa ninalolipata ni huu ugonjwa wa kushusha mabawa (kuvaa koti)Coccidiosis! Ninaweza kupata ushauri wa nini kinga na matibabu yake. Nawasilisha wakuu.
 
Wana-jamvi mimi nina kitabu, cha kufuga kuku wa kienyeji, nimeshindwa kukiweka hapa, mwenye haja ani PM, tafadhali, espescially wewe FIRST LADY, wataka kufuga wa kienyeji!
 
Wana-jamvi mimi nina kitabu, cha kufuga kuku wa kienyeji, nimeshindwa kukiweka hapa, mwenye haja ani PM, tafadhali , espescially wewe FIRST LADY, wataka kufuga wa kienyeji!!!!!!

Ubaguzi mkuu, kama ni special kwa FL basi ungem-PM wewe, wengi tunaoshiriki mjadala huu tuna haja na maarifa zaidi.
 
Kwanza nimkaribishe bwana Bathrm ambaye amesema amejiunga na JF hivi karibuni, karibu sana na waalike na wenzako pia,

Kuhusu kuku, mimi niko kwenye pilot project ambayo imeanza kama miezi miwili hivi iliyopita, kwa ufupi naweza kusema kwamba ni Biashara nzuri kwani mwelekeo nimeanza kuuona.
 
Habari gani wakuu?

Kuna vifaranga wa kienyeji sasa hivi wanauzwa. Je, hao nao wana matatizo gani katika ufugaji?
 
Habari gani wakuu? Kuna vifaranga wa kienyeji sasa hivi wanauzwa, je hao nao wana matatizo gani ktk ufugaji ?

Kama una uhakika na matetea yaliyotaga mayai hapo no problem, lakini kama hujui anayekuuzia katoa wapi mayai,ni kasheshe tupu. Inawezekana mimi ndio sijui maana ya kuku wa kienyeji, nijuavyo mimi(mtanisaidia),kuku wa kienyeji ni yule aliyetokana na jogoo/mtetea wa asili ambaye sio hybrid (pure kwa jogoo na mtetea).

Siku hizi tuna cross breed nyingi sana za kuku wa Kienyeji. Na muda si mrefu tutapoteza kuku wetu, kama tulivyo poteza vile vikuku short chases vya uluguruni,vinataga mayai hadi vinashindwa kuatamia kwa sababu ya uwingi, vinaangua mayai yote na vinatunza vifaranga wote kama hakuna predators.
 
Nafahamu katika JF kuna thread mbili ambazo zimejikita katika ufugaji wa kuku ambapo wafugaji na wale wanaotaka kuanza kufuga wamejadili mambo mengi..

nimeona ni vema niwashirikishe link hii titled
KUKU WA AMADORI utapata mambo mengi ya ufugaji wa kuku..
Kuku wa Amadori « simbadeo2000


Thread nyingine za ufugaji wa kuku zilizowahi kujadiliwa hapa JF ni hizi hapa. nimeziweka hapa kwa sababu kuna watu wengi humu wanakuwa wanazitafuta lakini hawajui jinsi ya kuzipata:


  1. Insha: YAH: Kuku wa kienyeji na kuku wa kizungu https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-lugha/35473-insha-yah-kuku-wa-kienyeji-na-kuku-wa-kizungu.html
  2. Ufugaji wa kuku https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/70693-ufugaji-wa-kuku.html
  3. Kuku wa mayai https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/86289-kuku-wa-mayai.html
  4. Nimeanza kufuga kuku wa Kienyeji -Soko likoje? https://www.jamiiforums.com/busines...anza-kufuga-kuku-wa-kienyeji-soko-likoje.html
  5. Mbegu za kuku wa kienyeji https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/88299-mbegu-za-kuku-wa-kienyeji.html
Nawasilisha kwa uperuzi na reference!!!

Next time nita-compile mada za ardhi ya kilimo ili watu waweze kuziona na kufanya reference pale wanapohitaji!!
 
Ukifanikiwa ku-compile thread za ardhi ya kilimo kama ulivyo kusanya thread za kuku utakuwa umesaidia sana. Thanks mkuu.
 
Nataka kufuga kuku wa nyama ila sina uzoefu naufugaji wa kuku mtaji wangu ni 5000,000/= kwa pesa hiyo naweza kufuga kuku wangapi, pia nataka kujua soko la kuku wa nyama Dar-es-Salaam liko.
 
nataka kufuga kuku wa nyama ila sina uzoefu naufugaji wa kuku mtaji wangu ni 5000,000/= kwa pesa hiyo naweza kufuga kuku wangapi, pia nataka kujua soko la kuku wa nyama Dar-es-salaam liko

Mkuu una mtaji wa milioni tano kwa ajili ya kuku au?
 
Una Banda tayari, au inabidi ulijenge kwa hela hiyo hiyo? Ushauri wa awali kuhusu banda la broiler; kuku 10 kwa meta ya mraba. Mfano ukitaka kufuga kuku 1000 banda liwe na angalu 100m2.
 
Tafuta jamaa yako yeyote aliyesoma mambo ya Animal Health au Animal Production. Hao watakupa mpaka michoro ya banda pamoja na kukuandikia "business plan" Kwenye hilo andiko kutakuwa na kila kitu kinachohitajika kwenye ufugaji wa kuku. Tafuta namna ya kuweka namba zako za simu ili hao wadau wakutwangie mweze kupanga vizuri naamini watakushauri vizuri sana. Hapo Dar mbona hao jamaa wamejazana tu!
 
Nashukuru hata mimi nimejifunza kitu licha ya kuwa sijawahi kufuga kuku nitazingatia ushauri wenu wana JF
 
Kweli hii ni nzuri. Je, ni vifanga wa kampuni gani ni bora zaidi?
Nasikia wengine hawakui kwa kiwango kinachotarajiwa na wanaugua sana.
 
Back
Top Bottom