Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

kichwa mbovu na wengine,

Nafikiria kufanya mradi mkubwa kiasi wa kuku wa mayai na/au wa nyama (layers na broilers) - nafikiria cycles za kuku elfu 5 mpaka 10 hivi. Ninalo eneo (shamba) kubwa tayari kwa shughuli hiyo. Lakini kwanza natafuta mtu mwenye uzoefu (wa ufugaji wa kibiashara) na ambaye anaweza kunisaidia kufanya feasibility study ya mradi huo. Je, unaweza kunisaidia kazi hiyo? Unahitaji taarifa gani kutoka kwangu ili kufanya kazi hiyo kwa ufanisi? Au kuna mtu/kampuni unafahamu wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi? Eneo la mradi lipo Dar, lakini nipo flexible kama mtaalamu atashauri nitafute eneo jingine - ili mradi prospects za kupata faida na sustainability ziwe za uahakika wa kuridhisha.

NDUGU SMU, kazi yako iko ndani ya uwezo wetu.Tuna uzoefu na hiyo kazi. Kuna wapo ambao tayari tumekwisha waanzishia mradi kama wako na wamefanikiwa, kwa mfano kuna mteja ambaye tumemwanzishia mradi na kwa sasa,kila mwezi anatoa kuku 5000 na kuwapeleka sokoni. Yeye anatotoresha na kufuga kuku wa kienyeji. Kila kuku anauzwa kwa shs.10,000 kwa bei ya jumla,ebu imagine kuku 5000 ni sh. ngapi anatengeza, ukipiga hesabu hapo utaona kila mwezi anatengeneza milioni 50.Akitoa gharama, let say milioni 20,je kuna kuna kazi gani ambayo unaweza ukaearn milioni 30 kwa mwezi!

Kwa hiyo kama utahitaji ufafanuzi zaidi nitumie namba yako kwenye private message nitakutumia yangu.
 
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.

Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajilikiwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi.

Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

Mimi nataka kufuga kuku,ila nahitaji kujua kati ya wale wa nyama,na mayai..wapi wanalipa zaidi?soko langu litakua Moshi na arusha zaidi. Halafu kama ni wa nyama au mayai,wazuri ni chotara,ama kienyeji ama kisasa? Ukishanijibu maswali mengine yataendelea hapo.
 
Mimi nataka kufuga kuku,ila nahitaji kujua kati ya wale wa nyama,na mayai..wapi wanalipa zaidi?soko langu litakua Moshi na arusha zaidi.
Halafu kama ni wa nyama au mayai,wazuri ni chotara,ama kienyeji ama kisasa? Ukishanijibu maswali mengine yataendelea hapo.

Kimsingi kuku wote wanalipa katika ufugaji,mfano kuku wa nyama broilers, kila wiki ukaingiza let say vifaranga 300 ,ukawafuga kwa kufuata kanuni, ukawafuga kwa wiki 8 ili uwauze kwa Tshs. 6000/=.Kama kila wiki utaingiza vifaranga ina maana bechi ya kwanza watakapofikia wiki 8,tayari utakuwa na bechi nyingine 7 zinafuata. Chukulia vifo ni 50 katika kuku 300 ingawa inaweza ikawa chini ya hapo. Kwa hiyo katika kila bechi kila wiki utakuwa na kuku 250.

Kimahesababu kuku 250 ukizidisha mara tshs.6000/=,utapata tshs. 1500,000/= kwa wiki na kwa mwezi utapata tshs 6000,000/=.Mapato ya broilers yanaanza baada ya miezi 2 yaani wk 8 ingawa unaweza ukawauza chini ya hapo lkn kwa uzito wa chini kidogo ndio maana inashauriwa wauzwe wk ya nane.

Kuku wa mayai pia nao wanalipa sana tatizo inatakiwa uwe na mtaji mkubwa kwa ajili ya gharama ya kuwanunua na chakula, mathalani kwa sasa baadhi ya makampuni ya kutotoresha vifaranga wanauza kila kifaranga tshs.2500.Kila kifaranga mpaka atakapoanza kutaga atahitaji kilo 8 za chakula, ukiongeza na madawa, mfanyakazi nk utajikuta unatakiwa uwe na mtaji mkubwa kweli. Mapato ya kuku wa mayai utaanza kupata kwa wastani kuanzia mwezi wa 5 katikati. Baada ya hapo utakuwa na kazi kuuza mayai tu mpaka watakapo choka wiki ya 80 kama umewatunza kwa kufuata misingi na kanuni boro za ufugaji.

Kama ni kuku wa mayai,wakisasa ni wazuri zaidi kwa kuwa wanataga kwa wingi.Kama ni wa nyama ukiweza kufaga machotara ni wazuri zaidi kutokana na kuwa na soko la uhakika. Watu wengi sasa hivi wanapenda kuku wa kienyeji hivyo machota, nyama yake haina tofauti na kuku wa kienyeji,pia ukiweza kuwafuga kwa miezi 6 utaweza kuwauza kila kuku kwa tsh.10000/= bila mteja anayenunua kulalamika. Kuku pure wa kienyeji wana ukuaji hafifu.
 
Leo niuzungumzie ugonjwa wa mafua (Infectious coryza)

Mafua ni ugonjwa mojawapo unaoshambulia mfumo wa upumuaji wenye tabia ya kumfanya kuku kutoa kamasi puani,kupiga chafya,kichwa kujaa maji na kuvimba.Ugonjwa huu huwaathiri kuku,bata mzinga na kanga.
Mafua ni ugonjwa unaowapata jamii ya ndege wa umri wote lakini zaidi ni kwa wakubwa.Ueneaji wake ni kwa njia ya hewa na chanzo chake ni ndege wanaougua au waliougua.

KISABABISHI

Mafua ya kuku husabibwa na Kimelea (Bacteria) kiitwacho Haemophilus paragallinum

DALILI ZA MAFUA
Dalili za mafua huanza kuonekana kuanzia siku ya 3-10 toka kuambukizwa.Sehemu zinazodhihirika zaidi ni pua,macho,mapafu,koo na koromeo.
  1. Kuku kuzubaa na kuto makamasi wakati mwingine yenye damu.
  2. Kubadilika rangi ya mapanga(Comb and wattle) na kuwa ya rangi ya bluu
  3. Huvimba macho,hali inayosabababisha kuku kuziba jicho moja na wakati mwingine yote mawili
  4. Kuvimba mapanga na uso
  5. kukosa hamu ya kula na kupunguza utagaji
  6. Kuku kukoroma wakati wa kupumua
  7. Kuhara uharo wenye harufu mbaya hasa kama kuna maambukizi mengine ya vimelea
  8. Vifo ni vichache na kuku hupona baada ya wiki

NAMNA YA KUZUIA
  • Usafi wa mazingira na kuhakikisha hakuna vimelea wanaosababisha ugonjwa huu
  • Kuku wagonjwa watengwe mbali na kuku wazima
  • Hakikisha vifaranga wanaagizwa kutoka kwenye makampuni yanayofuata kanuni bora za ufugaji
TIBA
Mafua ni ugonjwa unaotibika mfugaji unaweza kumwona afisa mifugo aliye karibu nawe ili akuandikie dawa sahihi ya kutumia.
 
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi kwani kazi ndio msingi wa maisha yetu.Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajilikiwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

salaam.
Ningependa unifahamishe kwa kuku hao wa kienyeji au mchanganyiko/machotara unahitaji eneo lakiasi gani kwa kuku 1000? Ukubwa wa mabanda? Na ukubwa wa eneo watakao shinga kwa mchana/nje?
Na utagaji wao unakuaje, ni kila siku au? Nia yangu ni kuwauza kwanza majogoo kwa ajili ya nyama pale watakapofikia umri na uzito wa kutosha, na hao majike watage msimu mmoja au miwili ndio niwauze. Na je ninaweza kuwasialana na wewe kwa njia gani zaidi ya hapa JF?
Ahsante
 
salaam.
Ningependa unifahamishe kwa kuku hao wa kienyeji au mchanganyiko/machotara unahitaji eneo lakiasi gani kwa kuku 1000? Ukubwa wa mabanda? Na ukubwa wa eneo watakao shinga kwa mchana/nje?
Na utagaji wao unakuaje, ni kila siku au? Nia yangu ni kuwauza kwanza majogoo kwa ajili ya nyama pale watakapofikia umri na uzito wa kutosha, na hao majike watage msimu mmoja au miwili ndio niwauze. Na je ninaweza kuwasialana na wewe kwa njia gani zaidi ya hapa JF?
Ahsante

NAFASI INAYOHITAJIKA KWA KUKU 1000 WENYE RIKA TOFAUTI (MABANDA YA KUKU)

[TABLE="class: grid, width: 500, align: center"]
[TR]
[TD]RIKA[/TD]
[TD]CHICKS

VIFARANGA[/TD]
[TD]
GROWERS

KUKU
WANAOKUWA
[/TD]
[TD]LAYERS

KUKU
WANAOTAGA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]UMRI
KTK
WIKI
[/TD]
[TD]0-6[/TD]
[TD]7-20[/TD]
[TD]20-80[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KUKU/ENEO LA
M[SUP]2 [/SUP]MOJA ZA MRABA

[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]M[SUP]2 [/SUP]ZINAZOHITAJIKA
/KUKU 1000


[/TD]
[TD]83.7M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]111.2M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]166.6M[SUP]2[/SUP][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Eneo watakaloshinda kuku 1000 wakati wa mchana, ambao hufugwa ktk mfumo wa nusu huria ni mita za mraba 10,000 .Hii inamaana kwamba ,kuku mmoja anahitaji eneo lenye mita za mraba 10.Kuhusu utagaji kuku wa kienji hana sifa ya utagaji wa mayai mengi.Kuku wa kienyeji hutaga kwa mzunguko.Kila mzunguko mmoja hutaga hutaga wastani wa mayai 15 na kuanza kuatamia,kutotoa na kulea vifaranga.Mzunguko huo huchukua wastani wa kipindi cha miezi 4 hadi 6 .Hali hiyo hiyo humfanya atage mayai machache kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kisasa ambao hutaga mayai 270 hadi 300.

Kuku wa kienyeji ukitaka watage mayai mengi wasiruhusiwa kuatamia,kila mayai yanayotagwa yaokotwe na kuhifadhiwa na kama mfugaji atahitaji kutotoresha, kama kuna kuku wengi ,ni vyema ikatumika machine ili kuzalisha vifaranga wengi zaidi.Kuku wa kienyeji anapokuwa kwenye mzunguko wa utagaji,kila siku hutaga yai moja.

Mawasiliano yangu nimekutumia kwenye private message yako ya jf,nenda kwenye notification yako fungua utaona.
 
salaam.
Ningependa unifahamishe kwa kuku hao wa kienyeji au mchanganyiko/machotara unahitaji eneo lakiasi gani kwa kuku 1000? Ukubwa wa mabanda? Na ukubwa wa eneo watakao shinga kwa mchana/nje?
Na utagaji wao unakuaje, ni kila siku au? Nia yangu ni kuwauza kwanza majogoo kwa ajili ya nyama pale watakapofikia umri na uzito wa kutosha, na hao majike watage msimu mmoja au miwili ndio niwauze. Na je ninaweza kuwasialana na wewe kwa njia gani zaidi ya hapa JF?
Ahsante

NAFASI INAYOHITAJIKA KWA KUKU 1000 WENYE RIKA TOFAUTI (MABANDA YA KUKU)

[TABLE="class: grid, width: 500, align: center"]
[TR]
[TD]RIKA[/TD]
[TD]CHICKS

VIFARANGA[/TD]
[TD]
GROWERS

KUKU
WANAOKUWA
[/TD]
[TD]LAYERS

KUKU
WANAOTAGA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]UMRI
KTK
WIKI
[/TD]
[TD]0-6[/TD]
[TD]7-20[/TD]
[TD]20-80[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]KUKU/ENEO LA
M[SUP]2 [/SUP]MOJA ZA MRABA

[/TD]
[TD]12[/TD]
[TD]9[/TD]
[TD]6[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]M[SUP]2 [/SUP]ZINAZOHITAJIKA
/KUKU 1000


[/TD]
[TD]83.7M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]111.2M[SUP]2[/SUP][/TD]
[TD]166.6M[SUP]2[/SUP][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Eneo watakaloshinda kuku 1000 wakati wa mchana, ambao hufugwa ktk mfumo wa nusu huria ni mita za mraba 10,000 .Hii inamaana kwamba ,kuku mmoja anahitaji eneo lenye mita za mraba 10.Kuhusu utagaji kuku wa kienji hana sifa ya utagaji wa mayai mengi.Kuku wa kienyeji hutaga kwa mzunguko.Kila mzunguko mmoja hutaga wastani wa mayai 15 na kuanza kuatamia,kutotoa na kulea vifaranga.Mzunguko huo huchukua wastani wa kipindi cha miezi 4 hadi 6 .Hali hiyo humfanya atage mayai machache kati ya mayai 30 hadi 60 kwa mwaka ukilinganisha na kuku wa kisasa ambao hutaga mayai 270 hadi 300.

Kuku wa kienyeji ukitaka watage mayai mengi wasiruhusiwa kuatamia,kila mayai yanayotagwa yaokotwe na kuhifadhiwa na kama mfugaji atahitaji kutotoresha, kama kuna kuku wengi ,ni vyema ikatumika machine ili kuzalisha vifaranga wengi zaidi.Kuku wa kienyeji anapokuwa kwenye mzunguko wa utagaji,kila siku hutaga yai moja.

Kuku chotara angalau utagaji wao unakuwa mzuri ukilinganisha na kuku wa kiaenyeji.

Ukihitaji contact zangu nitumie namba yako kwenye jf private message then nitakupatia yakwangu.
 
Kimsingi kuku wote wanalipa katika ufugaji,mfano kuku wa nyama broilers,kila wiki ukaingiza let say vifaranga 300 ,ukawafuga kwa kufuata kanuni,ukawafuga kwa wiki 8 ili uwauze kwa tshs. 6000/=.Kama kila wiki utaingiza vifaranga ina maana bechi ya kwanza watakapofikia wiki 8,tayari utakuwa na bechi nyingine 7 zinafuata.Chukulia vifo ni 50 katika kuku 300 ingawa inaweza ikawa chini ya hapo.Kwa hiyo katika kila bechi kila wiki utakuwa na kuku 250.

Kimahesababu kuku 250 ukizidisha mara tshs.6000/=,utapata tshs. 1500,000/= kwa wiki na kwa mwezi utapata tshs 6000,000/=.Mapato ya broilers yanaanza baada ya miezi 2 yaani wk 8 ingawa unaweza ukawauza chini ya hapo lkn kwa uzito wa chini kidogo ndio maana inashauriwa wauzwe wk ya nane.

Kuku wa mayai pia nao wanalipa sana tatizo inatakiwa uwe na mtaji mkubwa kwa ajili ya gharama ya kuwanunua na chakula ,mathalani kwa sasa baadhi ya makampuni ya kutotoresha vifaranga wanauza kila kifaranga tshs.2500.Kila kifaranga mpaka atakapoanza kutaga atahitaji kilo 8 za chakula,ukiongeza na madawa,mfanyakazi nk utajikuta unatakiwa uwe na mtaji mkubwa kweli.Mapato ya kuku wa mayai utaanza kupata kwa wastani kuanzia mwezi wa 5 katikati .Baada ya hapo utakuwa na kazi kuuza mayai tu mpaka watakapo choka wiki ya 80 kama umewatunza kwa kufuata misingi na kanuni boro za ufugaji.

Kama ni kuku wa mayai,wakisasa ni wazuri zaidi kwa kuwa wanataga kwa wingi.Kama ni wa nyama ukiweza kufaga machotara ni wazuri zaidi kutokana na kuwa na soko la uhakika.Watu wengi sasa hivi wanapenda kuku wa kienyeji hivyo machota, nyama yake haina tofauti na kuku wa kienyeji,pia ukiweza kuwafuga kwa miezi 6 utaweza kuwauza kila kuku kwa tsh.10000/= bila mteja anayenunua kulalamika.Kuku pure wa kienyeji wana ukuaji hafifu.

Okay nashukuru sana.
kwa maelezo yako nadhani kuku wa nyama watanifaa kufuga, kama naanza na vifaranga say 250,gharama ya utunzaji hadi kufikia kuuza itakua roughly how much?chotara au wa kisasa.
 
Mzoefu naomba anielekeze namna ya kufanya attachment ya document nizidi kutupia vitu
 
Okay nashukuru sana.
kwa maelezo yako nadhani kuku wa nyama watanifaa kufuga, kama naanza na vifaranga say 250,gharama ya utunzaji hadi kufikia kuuza itakua roughly how much?chotara au wa kisasa.

Badae nitakuji kazi zikipungua kidogo ofisini.
 
Hakika mwezi huu wa 12 lazima nianze, nitafuga kuku wa Malawi au aina nyingine ya machotara.JKT RUVU wanauza vifaranga bei nzuri.
 
Nimerudi tena na sasa naanda majibu ya Selmah,Kama kuna mtu still ana swali tutalijadili kwa pamoja.
 
Hakika mwezi huu wa 12 lazima nianze, nitafuga kuku wa Malawi au aina nyingine ya machotara.JKT RUVU wanauza vifaranga bei nzuri.

Try Singo,inalipa sana,ni kama masihara unaweza ukawa boss kwenye kampuni yako mwenyewe kama ambavyo wasemavyo Sokoine university of Agriculture Graduates entrepreneurs cooperative(SUGEKO),kwenye slogan yao kwamba "SUGEKO...!!!,BE YOUR OWN BOSS.Ni katika kuhamasishana vijana na hasa graduates kujiajili.Pia wanasema be a job creator and not job seeker kwani kutafuta kazi ni kazi.
So vijana lazima tukomae,si lazima ufugaji wa kuku hata mifugo mingine,tutaingolea siku za mbele Inshallah.
 
Okay nashukuru sana.
kwa maelezo yako nadhani kuku wa nyama watanifaa kufuga, kama naanza na vifaranga say 250,gharama ya utunzaji hadi kufikia kuuza itakua roughly how much?chotara au wa kisasa.

Swali lako nitalijibu kwa option mbili.Wewe utachagua option moja kati ya hizo utakayoona inafaida kwako.Kwanza tuangalie bei ya mfuko mmoja wa kg 50 huku kwetu unauzwa tsh.38000.

OPTION 1
Vifaranga watafugwa kwa wiki 8
Gharama ya kuku mmoja kama ifuatavyo;
Bei ya kifaranga kimoja ni tshs. 1500/=

Chakula cha broiler 1 ni tshs. 3300/=
Mshahara wa mfanyakazi tshs. 100/=
Dawa na gharama ya afisa mifugo tshs. 800/=
Usafiri wa kifaranga1 ni tshs. 150/=
Gharama ya umeme ni tshs. 5o/=
Gharama ya vifo kwa kifaranga ni tshs. 150/=

Gharama za kumfuga kuku mmoja ni tshs. 6050/=

MAUZO
Kuku mmoja aliyefugwa kwa wiki 8 atauzwa kwa bei ambayo ni ya wastani ya tsh 6500.Ukitoa gharama,faida halisi kwa kuku itakuwa tshs. 450/=hii ni kwa wiki.Kwa kuku 250 faida itakuwa tshs.112500 kwa wiki na kama kila wiki utaingiza vifaranga,ina maana kila wiki utakuwa unauza vifaranga 250 hivyo kwa mwenzi utatengeneza faida halisi ya tshs.450,000/=Je faida itakuwaje kwa miezi 2,3,4,5,6........na 12.Hapo hatujajumlisha mauzo ya samadi.

Kwa hii option 1,exactly, gharama ya kuwafuga kuku 250 itakuwa tshs.1,512,500/=


OPTION 2
Vifaranga watafugwa kwa wiki 6
Gharama ya kuku mmoja kama ifuatavyo;

Bei ya kifaranga kimoja ni tshs. 1500/=
Chakula cha broiler 1ni tshs 2050/=
Mshahara wa mfanyakazi ni tshs. 100/=
Dawa na gharama ya afisa mifugo ni tshs. 600/=
Usafiri wa kifaranga ni tshs. 150/=
Gharama ya umeme ni tshs. 5o/=
Gharama ya vifo kwa kifaranga ni tshs.150/=

Gharama za kumfuga kuku mmoja ni tshs. 4600/=

MAUZO
Kuku mmoja aliyefugwa kwa wiki 6 atauzwa kwa bei ambayo ni ya wastani ya tshs. 5500/=ingawa inaweza ikazidi kulingana na soko.Ukitoa gharama,faida halisi kwa kuku itakuwa tsh 900/=hii ni kwa wiki.Kwa kuku 250 faida itakuwa tshs.225000/= kwa wiki na kama kila wiki utaingiza vifaranga,ina maana kila wiki utakuwa unauza vifaranga 250 hivyo kwa mwenzi utatengeneza faida halisi ya tshs.900,000/=Je faida itakuwaje kwa miezi 2,3,4,5,6........na 12.Hapo hatujajumlisha mauzo ya samadi.

Kwa hii option 2,exactly,gharama ya ku niwafuga kuku 250 itakuwa tshs.1,150,000/=

USHAURI
  • Mfugaji/mjasiriamali anashauliwa kuchagua mradi ambao unatumia gharama ndogo ila unatoa faida kubwa.
  • Kutokana na ughali wa chakula cha kuku,mfugaji anashariwa wakati wa msimu wa mazao,kununua malighafi mfano mahindi,pumba,mashudu nk.kwani kipindi hicho bei huwa chini,ili mfugaji aweze kutengeneza chakula chake mwenyewe.
 
u

Kama ni PDF inakuwaje?Au ufupi minimum page ngapi ili iwe copy and paste

Hata pdf unaweza kuikopi na kupesti, ebu jaribu ukishindwa uliza. Fungua sehemu ya post kisha ipestie umo baada ya kuikopi.
 
Back
Top Bottom