Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 961
- 533
kichwa mbovu na wengine,
Nafikiria kufanya mradi mkubwa kiasi wa kuku wa mayai na/au wa nyama (layers na broilers) - nafikiria cycles za kuku elfu 5 mpaka 10 hivi. Ninalo eneo (shamba) kubwa tayari kwa shughuli hiyo. Lakini kwanza natafuta mtu mwenye uzoefu (wa ufugaji wa kibiashara) na ambaye anaweza kunisaidia kufanya feasibility study ya mradi huo. Je, unaweza kunisaidia kazi hiyo? Unahitaji taarifa gani kutoka kwangu ili kufanya kazi hiyo kwa ufanisi? Au kuna mtu/kampuni unafahamu wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi? Eneo la mradi lipo Dar, lakini nipo flexible kama mtaalamu atashauri nitafute eneo jingine - ili mradi prospects za kupata faida na sustainability ziwe za uahakika wa kuridhisha.
NDUGU SMU, kazi yako iko ndani ya uwezo wetu.Tuna uzoefu na hiyo kazi. Kuna wapo ambao tayari tumekwisha waanzishia mradi kama wako na wamefanikiwa, kwa mfano kuna mteja ambaye tumemwanzishia mradi na kwa sasa,kila mwezi anatoa kuku 5000 na kuwapeleka sokoni. Yeye anatotoresha na kufuga kuku wa kienyeji. Kila kuku anauzwa kwa shs.10,000 kwa bei ya jumla,ebu imagine kuku 5000 ni sh. ngapi anatengeza, ukipiga hesabu hapo utaona kila mwezi anatengeneza milioni 50.Akitoa gharama, let say milioni 20,je kuna kuna kazi gani ambayo unaweza ukaearn milioni 30 kwa mwezi!
Kwa hiyo kama utahitaji ufafanuzi zaidi nitumie namba yako kwenye private message nitakutumia yangu.