Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuwasiliane mkuu,nanavyo.Ni pamphlects zinazotoa mwongozo wa ufugaji bora wa kuku wa kienyeji,chotara na wa kisasa.
Mkuu kichwa nina swali kwenye swala la Kutotoresha, Ulisema unaweza gawa Incubators ya mayi 1000 mara mbili yaani ukaweka mayai 500 baada ya wili mbili ukaweka mengine 500, Ia ninavyo jua mimi Joto na Humidity ndani ya Incubators inatakiwa kubadilika pale inapo fikia kuanguliwa yaani siku ya 18 inatakiwa Humidity ipande juu kidogo na unaacha au unachomo Eggs turining susteam make siku ya 18 ndo inatakiwa wisho kugeuza mayai, so ukifanya hivyo inakuwa vipi katika swala la kugeuza mayai na humidity? kwa sbabau mayai yanatakiwa kugeuzwa angalau mara Tatu kwa siku,
Mkuu nimekupata vyema kabisa, Kuna sehemu nilisoma huwa inawezekana kutotoresha Vifaranga kabla ya siku 21 yaani unaweza ongeza joto na hivyo kufanya mayai yatotorewe yakiwa na hata siku 19, hii vipi?
King kingo,Mkuu kichwa mbovu
Hivi kwa hapa Tanzania ni wapi naweza kupata kuku wazazi kwa ajili ya broilers?
Mkuu kichwa, vipi kuhusu kusafirisha Fertlized eggs, yaani ni njia zipi nzuri za kusafirisha mayai ya kwenda kuatamisha? mfano umepata mayai Mbeya na unataka kuyapeleka Arusha, je utatumia Tray kama kawaida au kuna njia nyingine ya kuyabeba,
Mkuu kwenye kutibu Mayai, ni lazima utibu yote kabla ya kuweka kwenye mashine/Incubators? na ukisha changanya hayo madawa unaosha kama unavyo osha vyombo vya chakula? au kuna mtambo mwingie wa kutibu?
Na je kama source ya mayai ni wewe mwenyewe means kutoka kwenye kuku wako ni lazima kuyatibu?
King kingo,
Kwa hapa Tanzania huwezi kuwapata kuku wazazi wa Broilers.Kwa afrika mashariki kuku hawa wanapatikana nchini Kenya ambako kuna kituo cha kuzalisha na kuuza kuku wazazi wa Broilers kinachomilikiwa na Aviagen ya uingereza ambao ni wazalishaji wakubwa wa Hybro parent stock.
Chasha,
Ni muhimu kuyatibu mayai yote kabla ya kuingizwa kwenye Incubators kwa kuwa mayai toka yatagwa na kuku huchukua siku 7 hadi 10 mpaka kuingizwa kwenye Incubator.
Yai linapotagwa linakuwa limejiweka kwenye mazingira rahisi kuingiwa na wadudu ambao huenda kuharibu kiini cha yai matokeo yake husababisha yai kushindwa kutotolewa na hivyo kupunguza percentage of harcherbility.
Hata kama mayai unazalisha mwenyewe lazima uyatibu.Utibuji wa mayai husaidia kuzuia pia manjwa ya kuambukiza toka kwa mama kwenda kwa vifaranga.Ndio maana wakati mwingine unakuta vifaranga wanazaliwa baada ya muda mfupi wanakufa wote.Hali hii inatoka na mayai kutotibiwa.
Dawa ya kutibu mayai ni ya kuunguza na mvuke wake ndio unaotibu mayai.Mayai yote hutibiwa kwa pamoja.Wakati mwingine unaweza ukailamu Incubator yako kuwa sio nzuri kumbe mayai yako hukuyatibu hivyo yanakuwa yameharibiwa na wadudu.Wadudu hawa ni wadogowadogo sana ambao hawana uwezo wa kuonekana kwa macho na wana uwezo mkubwa sana wa kupenya hadi kwenye kiini cha yai na kukiharibu.
Dawa zinazotumika kwa ajili ya utibuji wa mayai ni dawa mbili ambazo hutumika zote kwa pamoja kwa ya fumigation.Dawa hizo ni Potassium parmananate pamoja na fomalin 40%.