Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 961
- 533
Nganu,Mkuu,kuku wangu(matetea)hayatotoleshi vifanga vingi tatizo ni nini? au uwingi wa majogoo linaweza kuwa tatizo.ahsante.
Inawezekana kuku wako unawawekea mayai mengi kuliko uwezo wake matokeo yake kuku anashindwa kuyamudu kuyaatamia mayai yote,hivyo kushindwa kutoa joto linalostahili ambalo ni muhimu kwa utotorewaji wa vifaranga.
Kuku wa kienyeji ana uwezo wa kuatamia vizuri mayai kati ya 10-15 kwa wakati moja,vinginevyo hataweza kuyaatamia vyema.
Sababu nyingine ni uwingi wa majogoo unasababisha matetea washindwa kutotoa vizuri kwa kuwa jogoo mmoja anapoenda kumpanda tetea, majogoo wengine wanaenda kumfurumua yule jogoo anayeenda kumpanda tetea matokeo yake yai linakosa kurutubishwa na mbegu ya jogoo.
Yai lisiporutubishwa haliwezi kutotolewa.
Uwiano sahihi kati ya jogoo na tetea ni 1:10 yaani, jogoo mmoja kwa jike kumi.
Mayai yasiyotibiwa pia hupunguza asilimia ya utotorewaji kwa kuwa,wakati mwingine yanaingiwa na wadudu ambao hupenya hadi kwenye kiini cha yai na kukiharibu.Kiini cha yai kikiharibiwa yai haliwezi kutotolewa.