Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chasha,
Mama Joe na Sabayi wako sahihi kabisa, mchanga husaidia kwenye usagaji wa chakula ili digestion symstem iweze kufanya kazi yake vizuri. Pia mchanga ni dawa ya kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis) kwa kuwa husaga mayai yasababishayo ugonjwa huo.
Ni muhimu kwa wafugaji kuwawekea kuku mchanga kwenye moja ya chombo cha chakula kisichokuwa na chakula.
Nianze nawe ndugu yangu Zion Daughter,kwanza umeuliza uzoefu wangu kwa ufupi hasa changamoto na masoko.Kwa upande wa changamoto ni kwamba wafugaji wengi wa kuku hushindwa kuyatambua magonjwa mbalimbali ya kuku pale yanapotokea hali inayopelekea kuku wengi kufa kwa magonjwa.Kujua ugonjwa inamsaidia mfugaji kuchagua dawa sahihi.Endapo kuku watapatiwa dawa sahihi hupona haraka kama walipata maambukizo ya ugonjwa.Changamoto nyingine ni ughali wa chakula cha kuku hasa kutokana na kucompete na binaadamu.Na kuhusu masoko,kiukweli soko la kuku sio tatizo.Demand ya kuku pamoja na mayai ni kubwa sana kuliko uzalisha uliopo.Kuhusu kukushauri uanze na kuku wangapi au mtaji shilingi ngapi hapo itabidi kwanza uniambie unahitaji kufaga kuku wa aina gani,maana kuna kuku wa nyama wa kisasa (Broilers),kuna kuku wa mayai wa kisasa(Layers),pia kuna kuku machotara na kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama na mayai.Na kwa wale wanaotaka kuanzishisha mradi wa utotoreshaji wa kuku watahitaji kuwa na kuku wazazi yaani Parent stock.Pia uniambie aina ya ufugaji mfano ufugaji huria,nusu kuria au wa ndani bila kuku kutoka.
Suala la ufagaji wa kuku kuchanganya na mifugo mingine kama ulivyo ainisha kwy swali lako inaruhusiwa ilaa ni kwa kuku wa kienyeji hasa wanaofugwa huria.Kinyesi cha mifugo mfano mbuzi,ng'ombe nk husaidia kutengeneza funza ambao ni chakula kizuri kwa kuku .
Mkuu asante sana kwa ufafanuzi wako
Ukiwaweka wataula? sio ni lazima uchnganwe kenyechakula chao?
kwangu mimi nina mbwa..na sometimes mbwa hupata viroboto..je si tishio kwa kuku?au ni kuku wa ina gani naweza kufuga ikiwa banda liko karibu na la mbwa?
Chasha,Mkuu kicwa, asante kwa Majibu, ukwelini upi kuhusu muda wa mayai kukaa kabla ya kuwekwa kwenye kuanguliwa, baadhi wanadai yaizdi siku saba au 8 tangu yatagwe, na wngine wanadai isizidi siku 14, vipihapo?
Asante Tanzanite klm, mayai ya kuatamiwa yanatakiwa yasikae zaidi ya siku 10,kama unaweza kupata mayai yaliyotagwa ndani ya siku saba ni vizuri zaidi. Kuhusu kutotoa mayai machache,nadhani ni kwa sababu ya kutotibu mayai yako. Kuku ana uwezo wa kuatamia mpaka mayai 15 na kutotoa vifaranga 12-13 kati ya mayai yote.Ni jinsi gani ya kutibu mayayi,naomba nifungue hapa, cz huwa napoteza vifaranga sana.
Mkuu habari ya kazi Kichwa,
Nina kuku wekundu wa mayai kutoka Malawi.Tatizo lao ni kwamba kila wakati wanaacha midomo wazi iwe mchana au usiku na wanatoa sauti kama vile kuna kitu kwenye koo kinawabana na wanapungua uzito.Je watakuwa wanasumbuliwa na nini? kwani nimewapa dose ya minyoo(oral kepromec,coryza(tylodox)lakini bado hali ni tete kwani walikuwa wanataga kwa 95%lakini kwasasa wapo 80% na nawapa amintotal kama vitamini.Swali jingine kwa hapa Tanzania, chanjo ya coryza na chronic respiratory disease zinapatikana?Nipo Gongo la mboto Dar es Salaam.
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako,usituchoke.Anania,
Mimi ni mzima kabisa.Hizo dalili unazosema ni kama za chronic respiratory disease(CRD) au kama siyo ni mafua yaani infectious coryza,ila zaidi zaidi nionavyo mimi na kwa dalili hizo ulizotaja ni wazi kuwa ugonjwa huo utakuwa CRD,chanjo za haya magonjwa kwa Tanzania hazipatikani kwa kuwa magonjwa yote hayo ni ya bacteria,yanatibika kwa dawa za kawaida na siyo lazima chanjo lakini pia mfano Ugonjwa wa kwanza ni nadra sana kutokea nchini kwetu.Mafua ni ugonjwa ambao hutokea mara kwa mara kwenye makundi ya kuku.
Mara nyingi magonjwa ya mfumo wa upumuaji mfano CRD na infectious coryza hasa yakiwa sugu, dawa za unga hazileti matokeo mazuri.Hapo ili kupata ufanisi inabidi itumike dawa ya sindano aina ya tylosine.Kuku wako wote watapona na wataendelea vizuri.
Nakusihi kuwa makini kama dawa ya sindano itatumika,kwani kuna watu mtaani wanajiita madactari na kwamba wanaweza kuchoma kuku sindano matokeo yake wanaua kuku.
Mwisho nikupongeza kwa kuweza kufikisha 95% ya utagaji wa kuku wako,natumai wewe ni miongoni mwa wafugaji bora kabisa wa kuku unaezingatia vyema kanuni na misingi ya ufugaji bora wa kuku .