Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ni kweli ukimchinja kuku utakuta mchanga kwenye firigisi. Huu unasaidia kuyeyusha/kusaga chakula. Wenzetu majuu unauzwa wenye texture maalumu kwa lkazi iyo.
 
Ni kweli ukimchinja kuku utakuta mchanga kwenye firigisi. Huu unasaidia kuyeyusha/kusaga chakula. Wenzetu majuu unauzwa wenye texture maalumu kwa kazi iyo.
 
Chasha,

Mama Joe na Sabayi wako sahihi kabisa,mchanga husaidia kwenye usagaji wa chakula ili digestion symstem iweze kufanya kazi yake vizuri. Pia mchanga ni dawa ya kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu(Coccidiosis) kwa kuwa husaga mayai yasababishayo ugonjwa huo.

Ni muhimu kwa wafugaji kuwawekea kuku mchanga kwenye moja ya chombo cha chakula kisichokuwa na chakula.
 
Chasha,

Mama Joe na Sabayi wako sahihi kabisa, mchanga husaidia kwenye usagaji wa chakula ili digestion symstem iweze kufanya kazi yake vizuri. Pia mchanga ni dawa ya kuzuia ugonjwa wa kuharisha damu (Coccidiosis) kwa kuwa husaga mayai yasababishayo ugonjwa huo.

Ni muhimu kwa wafugaji kuwawekea kuku mchanga kwenye moja ya chombo cha chakula kisichokuwa na chakula.

Mkuu asante sana kwa ufafanuzi wako Ukiwaweka wataula? sio ni lazima uchnganwe kenyechakula chao?
 
Nianze nawe ndugu yangu Zion Daughter,kwanza umeuliza uzoefu wangu kwa ufupi hasa changamoto na masoko.Kwa upande wa changamoto ni kwamba wafugaji wengi wa kuku hushindwa kuyatambua magonjwa mbalimbali ya kuku pale yanapotokea hali inayopelekea kuku wengi kufa kwa magonjwa.Kujua ugonjwa inamsaidia mfugaji kuchagua dawa sahihi.Endapo kuku watapatiwa dawa sahihi hupona haraka kama walipata maambukizo ya ugonjwa.Changamoto nyingine ni ughali wa chakula cha kuku hasa kutokana na kucompete na binaadamu.Na kuhusu masoko,kiukweli soko la kuku sio tatizo.Demand ya kuku pamoja na mayai ni kubwa sana kuliko uzalisha uliopo.Kuhusu kukushauri uanze na kuku wangapi au mtaji shilingi ngapi hapo itabidi kwanza uniambie unahitaji kufaga kuku wa aina gani,maana kuna kuku wa nyama wa kisasa (Broilers),kuna kuku wa mayai wa kisasa(Layers),pia kuna kuku machotara na kuku wa kienyeji kwa ajili ya nyama na mayai.Na kwa wale wanaotaka kuanzishisha mradi wa utotoreshaji wa kuku watahitaji kuwa na kuku wazazi yaani Parent stock.Pia uniambie aina ya ufugaji mfano ufugaji huria,nusu kuria au wa ndani bila kuku kutoka.

Suala la ufagaji wa kuku kuchanganya na mifugo mingine kama ulivyo ainisha kwy swali lako inaruhusiwa ilaa ni kwa kuku wa kienyeji hasa wanaofugwa huria.Kinyesi cha mifugo mfano mbuzi,ng'ombe nk husaidia kutengeneza funza ambao ni chakula kizuri kwa kuku .

Kwangu mimi nina mbwa..na sometimes mbwa hupata viroboto. Je, si tishio kwa kuku?au ni kuku wa ina gani naweza kufuga ikiwa banda liko karibu na la mbwa?
 
Mkuu asante sana kwa ufafanuzi wako
Ukiwaweka wataula? sio ni lazima uchnganwe kenyechakula chao?

Ukiwawekea wanakula tu vizuri ila si kama wanavyokula chakula chao.Sio vizuri kuwachanganyia kwenye chakula kuepusha kuwazidishia kiwango kuliko kile kinachohitajika.

Kuku anahitaji kiasi kidogo sana cha mchachanga kitakacho msaidia kusaga chakula ili kurahisisha mmeng'enyo wake.Kwa mantiki hiyo,mchanga uwekwe kwenye chombo kinachojitegemea ili kuku ajikadirie kiasi anachohitaji.
 
kwangu mimi nina mbwa..na sometimes mbwa hupata viroboto..je si tishio kwa kuku?au ni kuku wa ina gani naweza kufuga ikiwa banda liko karibu na la mbwa?

Chamweli,

Ni muhimu mbwa wako wakatafutiwa sehemu nyingine mbali kidogo na banda la kuku. Mbwa ni miongoni mwa wanyama wabebao magonjwa. Magonjwa hayo huweza kuwaambukiza kuku na kusababisha vifo.

Viroboto kwa mbwa vinazuilika iwapo tu utakuwa na utaratibu wa kuwaogesha mbwa wako kila wiki. Pia ni muhimu kuhakikisaha kuwa mabanda ya mbwa na ya kuku yakasakafiwa kwa cement ili kuzuia vumbi ambalo ni makazi mazuri sana kwa viroboto.
 
Mkuu kicwa, asante kwa Majibu, ukwelini upi kuhusu muda wa mayai kukaa kabla ya kuwekwa kwenye kuanguliwa, baadhi wanadai yaizdi siku saba au 8 tangu yatagwe, na wngine wanadai isizidi siku 14, vipi hapo?
 
Mkuu kicwa, asante kwa Majibu, ukwelini upi kuhusu muda wa mayai kukaa kabla ya kuwekwa kwenye kuanguliwa, baadhi wanadai yaizdi siku saba au 8 tangu yatagwe, na wngine wanadai isizidi siku 14, vipihapo?
Chasha,

Mayai ya kutotoresha yanaweza kukaa hadi siku 14 kabla ya kuwekwa kwenye mashine,ingawa kwa matokeo mazuri kwenye uanguliwaji wa vifaranga,inashauriwa mayai yakusanywe kwa siku 7 na ile siku ya nane asubuhi yawekwe kwenye machine.

Kuanzia siku ya 7, kila siku moja inayozidi inapunguza asilimia ya utotoaji wa vifaranga.Ni muhimu kuzingatia kwamba kila baada ya siku saba za kukusanya mayai, siku inayofuata, yaani siku ya nane, mayai yaingizwe kwenye machine tayari kwa kutotolewa.

Pia kwa ajili ya kuepusha magojwa kutoka kwa kuku wazazi kwenda kwa vifaranga lazima mfugaji ahakikishe kuwa mayai yanatibiwa kabla hayajaingizwa kwenye mashine. Pia utibuji wa mayai husaisaidia kuongeza kiwango cha utotorewaji wa vifaranga kwa kuwa dawa inayotumika kwenye utibuji wa mayai ina uwezo mkubwa sana wa kupenya hadi kwenye kiini cha yai na kuwaua wadudu waliopenya ndani kaabisa ambao huharibu kiini cha yai kinachotengeza kifaranga.

Utibuji wa mayai husaidia pia kuwafanya vifaranga wanaozaliwa kuwa imara na wenye nguvu, hivyo kuepusha vifo vya mara kwa mara hasa kwa vifaranga wenye umri kati ya wiki ya kwanza hadi ya 4.
 
Ni jinsi gani ya kutibu mayayi, naomba nifungue hapa, cz huwa napoteza vifaranga sana.
 
Ni jinsi gani ya kutibu mayayi,naomba nifungue hapa,cz huwa napoteza vifaranga sana.
 
Ni jinsi gani ya kutibu mayayi,naomba nifungue hapa, cz huwa napoteza vifaranga sana.
Asante Tanzanite klm, mayai ya kuatamiwa yanatakiwa yasikae zaidi ya siku 10,kama unaweza kupata mayai yaliyotagwa ndani ya siku saba ni vizuri zaidi. Kuhusu kutotoa mayai machache,nadhani ni kwa sababu ya kutotibu mayai yako. Kuku ana uwezo wa kuatamia mpaka mayai 15 na kutotoa vifaranga 12-13 kati ya mayai yote.

Kuhusu kutibu mayai unaweza kunitafuta kupitia 0767989713 au 071599713 nikakuelekeza zaidi.

Asante sana mkuu.
 
Mkuu habari ya kazi Kichwa,

Nina kuku wekundu wa mayai kutoka Malawi. Tatizo lao ni kwamba kila wakati wanaacha midomo wazi iwe mchana au usiku na wanatoa sauti kama vile kuna kitu kwenye koo kinawabana na wanapungua uzito. Je, watakuwa wanasumbuliwa na nini? kwani nimewapa dose ya minyoo (oral kepromec,coryza (tylodox) lakini bado hali ni tete kwani walikuwa wanataga kwa 95% lakini kwasasa wapo 80% na nawapa amintotal kama vitamini.Swali jingine kwa hapa Tanzania, chanjo ya coryza na chronic respiratory disease zinapatikana?Nipo Gongo la mboto Dar es Salaam.
 
Mkuu habari ya kazi Kichwa,
Nina kuku wekundu wa mayai kutoka Malawi.Tatizo lao ni kwamba kila wakati wanaacha midomo wazi iwe mchana au usiku na wanatoa sauti kama vile kuna kitu kwenye koo kinawabana na wanapungua uzito.Je watakuwa wanasumbuliwa na nini? kwani nimewapa dose ya minyoo(oral kepromec,coryza(tylodox)lakini bado hali ni tete kwani walikuwa wanataga kwa 95%lakini kwasasa wapo 80% na nawapa amintotal kama vitamini.Swali jingine kwa hapa Tanzania, chanjo ya coryza na chronic respiratory disease zinapatikana?Nipo Gongo la mboto Dar es Salaam.

Anania,

Mimi ni mzima kabisa.Hizo dalili unazosema ni kama za chronic respiratory disease (CRD) au kama siyo ni mafua yaani infectious coryza, ila zaidi zaidi nionavyo mimi na kwa dalili hizo ulizotaja ni wazi kuwa ugonjwa huo utakuwa CRD, chanjo za haya magonjwa kwa Tanzania hazipatikani kwa kuwa magonjwa yote hayo ni ya bacteria, yanatibika kwa dawa za kawaida na siyo lazima chanjo lakini pia mfano Ugonjwa wa kwanza ni nadra sana kutokea nchini kwetu.Mafua ni ugonjwa ambao hutokea mara kwa mara kwenye makundi ya kuku.

Mara nyingi magonjwa ya mfumo wa upumuaji mfano CRD na infectious coryza hasa yakiwa sugu, dawa za unga hazileti matokeo mazuri. Hapo ili kupata ufanisi inabidi itumike dawa ya sindano aina ya tylosine. Kuku wako wote watapona na wataendelea vizuri.

Nakusihi kuwa makini kama dawa ya sindano itatumika, kwani kuna watu mtaani wanajiita madaktari na kwamba wanaweza kuchoma kuku sindano matokeo yake wanaua kuku.

Mwisho nikupongeza kwa kuweza kufikisha 95% ya utagaji wa kuku wako,natumai wewe ni miongoni mwa wafugaji bora kabisa wa kuku unaezingatia vyema kanuni na misingi ya ufugaji bora wa kuku .
 
MAYAI YAFAAYO KUTOTOLEWA

1. Yawe mayai masafi
2. Yasiwe na ufa
3. Yawe mayai yanayotokana na kuku wazazi wa kisasa au kienyeji, wenye uwiano sahihi kati ya jogoo na Temba. Uwiano wa kuku wazazi ni jogoo 1 kwa Temba 10, hii ni sawasawa na 1:10.
4. Mayai yasioshwe walakutumbukizwa kwenye maji.Yakioshwa na maji huwarahishia bacteria kuingia na kuyaharibu.
5. Yawe mayai ya wastani , yasiwe makubwa sana na wala yasiwe madogo sana. Mayai madogo au makubwa yanakua na matatizo kwenye utotolewaji. Mayai madogo mara nyingi hutotoa vifaranga wadogo ambao kwa kawaida pia huwa ni wadhaifu na mara baada ya kuzaliwa hufa. Mayai makubwa hayatotolewi kutokana na mengi ya hayo kuwa na viini viwili (double yolk)
6. Lazima yawe yaliyotibiwa kwa dawa maalam za kutibia mayai.
 
UGONJWA WA KIPINDUPINDU CHA KUKU ( FOWL CHOLERA) Ni ugonjwa unaoambukiza .Huwaathiri kuku na jamii nyingine ya ndege wafugwao na ndege pori. Kisababishi Ugonjwa huu unasababishwa na bacteria anaeitwa Pasteurell multocida Dalili

Dalili
Vifo vya ghafla hutokea, Kuku kuzubaa na kunyongea, Kulegea, Kuku kushindwa kula na kunywa, Kusinzia, Kutokwa na ute telezi mdomoni, Kuharisha mharo mweupe na baadae kubadilika na kuwa mharo wa kijani, Kujikunyata, Mapanga kuwa ya na rangi ya bluu.
 
UGONJWA WA KUHARIBU MAYAI (COLLIBACILLOSIS)

Ugonjwa huu huwapata kuku wakubwa au wadogo wenye umri kati ya wiki 1-12,pia vimelea hivi hukaa katika wanyama wengine pamoja na ndege bila kuwa na madhara yeyote isipokuwa baadhi ya vimelea ndivyo husababisha ugonjwa.

Vimelea hivi huzaliana haraka katika utumbo wa vifaranga wapya na huambukizana kati ya vifaranga kwenye mashine ya kuangulia vifaranga na maeneo ya kulele vifaranga (brooders)

Ugonjwa huu umegawanyika katika sehemu kuu nne ambazo ni:

a) Ugonjwa wa kushindwa kutembea (Coliseptisaemia)
b) Ugonjwa wa kupasua mayai tumboni(egg peritonitis)
c) Ugonjwa wa kitovu(yolk sac infection)
d) Ugonjwa wa uvimbe mgumu tumboni
 
Anania,
Mimi ni mzima kabisa.Hizo dalili unazosema ni kama za chronic respiratory disease(CRD) au kama siyo ni mafua yaani infectious coryza,ila zaidi zaidi nionavyo mimi na kwa dalili hizo ulizotaja ni wazi kuwa ugonjwa huo utakuwa CRD,chanjo za haya magonjwa kwa Tanzania hazipatikani kwa kuwa magonjwa yote hayo ni ya bacteria,yanatibika kwa dawa za kawaida na siyo lazima chanjo lakini pia mfano Ugonjwa wa kwanza ni nadra sana kutokea nchini kwetu.Mafua ni ugonjwa ambao hutokea mara kwa mara kwenye makundi ya kuku.

Mara nyingi magonjwa ya mfumo wa upumuaji mfano CRD na infectious coryza hasa yakiwa sugu, dawa za unga hazileti matokeo mazuri.Hapo ili kupata ufanisi inabidi itumike dawa ya sindano aina ya tylosine.Kuku wako wote watapona na wataendelea vizuri.

Nakusihi kuwa makini kama dawa ya sindano itatumika,kwani kuna watu mtaani wanajiita madactari na kwamba wanaweza kuchoma kuku sindano matokeo yake wanaua kuku.

Mwisho nikupongeza kwa kuweza kufikisha 95% ya utagaji wa kuku wako,natumai wewe ni miongoni mwa wafugaji bora kabisa wa kuku unaezingatia vyema kanuni na misingi ya ufugaji bora wa kuku .
Mkuu nashukuru kwa ushauri wako,usituchoke.
 
Habari njema kwa wafugaji.

Matumizi ya soya kwenye mchanganyiko wa chakula cha kuku.Soya inatumika badala ya dagaa au sangara.

Faida
  1. Ina protein nyingi ukilinganisha dagaa
  2. Bei ya soya ni rahisi tsh 1500 kwa kilo huku ikiwa imechakatuliwa tayari,kwa kukaangwa, kusagwa na kupakiwa kwenye mifuko ya kilo 100.Bei hii pia inajumuisha usafiri hadi Dar es salam kwa wale wanaoishi huko.
  3. Soya haisababishi typhoid kama ambavyo inavyosababisha dagaa/sangara.
Kwa wale wanaohitaji tuwasiliane.

Pia mwongozo wa ufugaji bora wa kuku bado naendelea kusambaza kwa wafugaji kote nchini.Pata mwongozo wako mapema ukuongoze kwenye mradi wa ufugaji wako bora wa kuku.Bei yetu ni ile ile,tsh 60,000/=
 
Mkuu kichwa, kwani kazi ya dagaa kwenye chakula cha kuku ni ipi,? Nilikuwa nazania iko kwenye kundi la kuimarisha mifupa, ok utakuja unitumie kwenye ISLAM YA MORO Ngoja nikae sawa.
 
Back
Top Bottom