King kingo,
Kuku hawa wanaanza kutaga wakiwa na umri wa wiki kumi na tisa.Kuku wazazi wa mayai wanataga sana kama utafuata masharti yao ya malezi pamoja na chakula.Kwa kawaida sio rahisi kuku wote katika kundi wakawa wanataga,isipokuwa kwa kuku wazazi wa mayai wanapokuwa kwenye kilele cha utagaji wanataga hadi asilimia 96.
Kuku wako wa mayai hawakuwa wanataga wote inategemea na aina ya management uliyokuwa unawapa.Lakini vinginevyo kuku hawa ni watagaji wazuri tu,laita ungewasiliana na mimi ningekuuzia uchawi wa dactari na kuku wako wangetaga vizuri.
Najua changamoto kubwa inayowakabili wafugaji wa kuku ni kwenye utagaji hasa kutokana na chakula wanachowalisha kutokuwa na ubora unaotakiwa,pia kuku hawa kukabiliwa na magonjwa na mfugaji kushindwa kuyatambua n.k Kuhusu suala la utagaji nishalifanyia utafiti na nimepata mafanikio makubwa sana.Kama una kuku ambao hawatagi au wameonekana wanaelekea kuchoka katika utagaji kabla ya muda wake tuwasiliane hata usiwauze,watataga vizuri sana mpaka utashangaa.
Kiukweli katika ufugaji wa kuku hakuna kubahatisha kwenye ushughulikiwaji matatizo vinginevyo hasara haiepukiki.Kwa suala la kuku kushindwa kutaga katika malengo yaliyokusudiwa siyo tatizo tena ukifanya mawasiliano nami.
Kuku wazazi wanachakula chao maalum ambacho kinatengenezwa kwa kutumia malighafi hizi hizi zinazotumika kutengenezea chakula cha kuku wa kawaida yaani Layers na Broilers.Kuku wazazi wa kuku wa mayai ni watagaji sana na ndio maana hiyo tabia wamewarisisha watoto wao yaani kuku wa mayai wa kawaida.
Kuku wazazi wa mayai au nyama ninaowaagiza ndio hao hao hata hayo makampuni makubwa ya utotoleshaji wa vifaranga ndiyo waliyokuwa nao,na wengi wao wao wanaagizia huko huko ambako mimi naagizia.