Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

hi @kichwa mbovu nimefuatilia hii mjadala nimepata elimu tosha. napenda kuuliza je kuku wa mayai wanachukua muda gani kuanza kutaga? na je kwa kuku mia mpaka watage watakuwa wametumia chakula kiasi gani? na je naweza kufuga kuku wa mayai na nyama kwa wakati mmoja au kutakuwa
na muingiliano wa magonjwa?

Little Angel,

Kuku wa mayai anaanza kutaga akiwa na miezi 5 na wiki 2 hadi tatu kama watakuwa wamefugwa kwa kufuta kanuni bora za ufugaji.Kuku mia moja hutumia kilogram 800 za chakula sawa na mifuko 16@50kg au sawa na 1.6tones mpaka watakapoanza kutaga.

Kuku wa mayai na wa nyama wanaruhusiwa kufugwa pamoja ila iwe mabanda tofauti,wasichanganywe.
 
Little angel,

Na unaweza kuwafuga kuku wazazi pamoja na wengine kama wa mayai pamoja? (Ofcourse kwenye mabanda tofauti)
 
King kingo,
Kuku hawa wanaanza kutaga wakiwa na umri wa wiki kumi na tisa.Kuku wazazi wa mayai wanataga sana kama utafuata masharti yao ya malezi pamoja na chakula.Kwa kawaida sio rahisi kuku wote katika kundi wakawa wanataga,isipokuwa kwa kuku wazazi wa mayai wanapokuwa kwenye kilele cha utagaji wanataga hadi asilimia 96.

Kuku wako wa mayai hawakuwa wanataga wote inategemea na aina ya management uliyokuwa unawapa.Lakini vinginevyo kuku hawa ni watagaji wazuri tu,laita ungewasiliana na mimi ningekuuzia uchawi wa dactari na kuku wako wangetaga vizuri.

Najua changamoto kubwa inayowakabili wafugaji wa kuku ni kwenye utagaji hasa kutokana na chakula wanachowalisha kutokuwa na ubora unaotakiwa,pia kuku hawa kukabiliwa na magonjwa na mfugaji kushindwa kuyatambua n.k Kuhusu suala la utagaji nishalifanyia utafiti na nimepata mafanikio makubwa sana.Kama una kuku ambao hawatagi au wameonekana wanaelekea kuchoka katika utagaji kabla ya muda wake tuwasiliane hata usiwauze,watataga vizuri sana mpaka utashangaa.

Kiukweli katika ufugaji wa kuku hakuna kubahatisha kwenye ushughulikiwaji matatizo vinginevyo hasara haiepukiki.Kwa suala la kuku kushindwa kutaga katika malengo yaliyokusudiwa siyo tatizo tena ukifanya mawasiliano nami.

Kuku wazazi wanachakula chao maalum ambacho kinatengenezwa kwa kutumia malighafi hizi hizi zinazotumika kutengenezea chakula cha kuku wa kawaida yaani Layers na Broilers.Kuku wazazi wa kuku wa mayai ni watagaji sana na ndio maana hiyo tabia wamewarisisha watoto wao yaani kuku wa mayai wa kawaida.

Kuku wazazi wa mayai au nyama ninaowaagiza ndio hao hao hata hayo makampuni makubwa ya utotoleshaji wa vifaranga ndiyo waliyokuwa nao,na wengi wao wao wanaagizia huko huko ambako mimi naagizia.

Mkuu kichwa
Asante nimekupata vizuri
 
Wana JF,

Nimekuwa nikifuatalia sana habari za kufuga kuku wa kienyeji. Ki ukweli mimi ndio hobby yangu ila kwa elimu niliyopata hapa nimeona inawezekana kufuga kwa kukuingizia kipato.

Katika pitapita yangu kwenye mtandao nimekutana na jarida moja la ufugaji wa kuku. Kwa kweli ki muono wangu ni jarida lililokamilika na ningependa na wengine pia wafaidi elimu iliyoko ndani yake.

Naomba kuwakilisha.
 
Attachments

Vifaranga wazazi wa kuku wa nyama n mayai wanazalishwa kwa sasa nchini Kenya, kuna kampuni moja inawazalisha na kuuza nchi mbalimbali
Juzi niliongea na mkulima/mfugaji wa Tarime ambaye nimekutana naye huko Mkulima Mbunifu kanielezea kuhusu hao kuku wa Kenya aina ya KENBRO. Wao wanawapata kutoka Kisumu na wanaletewa pale border SIRARI. Anasema kifaranga cha siku moja kinauzwa KSh.40 kama TShs. 800; anasema pale border kwa sababu ni box moja tu hamna taabu. Haya wajasiriamali changamukieni hiyo fursa! Mimi bado najipanga.
 
Achakpotosha watu, mkuu, Kifaranga gani cha Sh 800? Na Vifaranga wa Kuku wa Mayi na Nyama ni Sh ngapi? make hao wote wa nyama na mayai bei yao haiwezi fikia Kenboro, usionge usicho kijua, Hata Vifaranga wa kuku kienyeji Pure bei yake si hiyo, Hata Bei ya Kware wanao fugwa sana Huko bei si hivyo.

So acha kupotosha Kenya nzima hakuna mahali kifaranga kinauzwa bei hiyo hata kama ni Wa mayai au Nyama achilia mali hao wengine.

Kabla ya Kupost uwe unauliza kwanza
 
Wana JF,

Nimekuwa nikifuatalia sana habari za kufuga kuku wa kienyeji. Ki ukweli mimi ndio hobby yangu ila kwa elimu niliyopata hapa nimeona inawezekana kufuga kwa kukuingizia kipato.

Katika pitapita yangu kwenye mtandao nimekutana na jarida moja la ufugaji wa kuku. Kwa kweli ki muono wangu ni jarida lililokamilika na ningependa na wengine pia wafaidi elimu iliyoko ndani yake.

Naomba kuwakilisha.......

Mkuu mwenye thread akikukuta ni noma,natania tu, Ok ila ni andiko zuri nilwahi kukutana nalo make hawa Heifer nilishawai kufanya kazi zao, na huwa wana project nzuri sana za Ng,ombe wa maziwa a Mbuzi wa Maziwa
 
Nashukuru sana kichwa mbovu na wadau wote kwa michango yenu mizuri nimeipitia yote na nimeelimika vya kutosha.Nimehamasika na najua kupitia ufugaji wa kuku nitajikwamua kimaisha. Kichwa mbove na wazo la kufuga kuku wa kienyeji (wa nyama) kulingana na elimu niliyoipata nimeona chotara watanifaa zaidi.

Nauliza: Je, nisahihi nikiwatafuta hawa kuchi tetea na hawa wa kisasa jogoo nikawafuga pamoja kupata chotara au kunautaalamu maalum katika kuwapa chotara? Pia kama kuna utalaamu maalumu naweza kuwapata wapi?na kwa bei gan? Nategemea kuanza ufugaji sept. Zaidi nashukuru kwa elimu.
 
Wana JF,

Nimekuwa nikifuatalia sana habari za kufuga kuku wa kienyeji. Ki ukweli mimi ndio hobby yangu ila kwa elimu niliyopata hapa nimeona inawezekana kufuga kwa kukuingizia kipato.

Katika pitapita yangu kwenye mtandao nimekutana na jarida moja la ufugaji wa kuku. Kwa kweli ki muono wangu ni jarida lililokamilika na ningependa na wengine pia wafaidi elimu iliyoko ndani yake.

Naomba kuwakilisha.......
Mh.Alsaidy,
Kwa kweli nakupongeza sana kwa document yako uliyoipost,kimsingi iko nondo sana,haifer project huwa hawabatishi wanapofanya kazi yao.Ni kazi ya uhaika,nimeipitia yote,binafsi nimeikubali.Document hii itawasaidia sana wafugaji wa kuku wa kienyeji.
 
Mkuu hiyo Nondo hata kwa wafugji wa kuku wa Kisasa inatumika, si wa Kieyeji tu, make ufugaji wa kuku wa kisasa n kienyeji kuna vitu vingi sana vinafanana, na ni vichache sana vinatofautiana.
 
Nashukuru sana kichwa mbovu na wadau wote kwa michango yenu mizuri nimeipitia yote na nimeelimika vya kutosha.Nimehamasika na najua kupitia ufugaji wa kuku nitajikwamua kimaisha.Kichwa mbove na wazo la kufuga kuku wa kienyeji(wa nyama) kulingana na elimu niliyoipata nimeona chotara watanifaa zaidi. Nauliza je nisahihi nikiwatafuta hawa kuchi tetea na hawa wa kisasa jogoo nikawafuga pamoja kupata chotara au kunautaalamu maalum katika kuwapa chotara?Pia kama kuna utalaamu maalumu naweza kuwapata wapi?na kwa bei gan?Nategemea kuanza ufugaji sept.Zaidi nashukuru kwa elimu
Mnyalu,Sahihi kabisa kutumia tetea wa kuchi na majogoo wa kisasa kutengeneza chotara.
 
Achakpotosha watu, mkuu, Kifaranga gani cha Sh 800? Na Vifaranga wa Kuku wa Mayi na Nyama ni Sh ngapi? make hao wote wa nyama na mayai bei yao haiwezi fikia Kenboro, usionge usicho kijua, Hata Vifaranga wa kuku kienyeji Pure bei yake si hiyo, Hata Bei ya Kware wanao fugwa sana Huko bei si hivyo,

So acha kupotosha Kenya nzima hakuna mahali kifaranga kinauzwa bei hiyo hata kama ni Wa mayai au Nyama achilia mali hao wengine,
Kabla ya Kupost uwe unauliza kwanza

Chasha,
Njia unayotumia kumkosoa mtu siyo nzuri,Ni vyema kama mtu kakosea akasahihishwa kwa lugha nzuri pale alipokosea,sio kumwambia acha kupotosha,sio kauli nzuri,sidhani mzee mukaruka alikusudia kupotosha ila alisema ni kwa mujibu wa mkulima aliyefanya nae mazungumzo.

Sote hapa tupo kwa ajili ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu,ndio maana alsaidy tumempongeza kwa kuleta document nzuri ya ufugaji wa kuku wa kionyeji.
 
chasha,
njia unayotumia kumkosoa mtu siyo nzuri,ni vyema kama mtu kakosea akasahihishwa kwa lugha nzuri pale alipokosea,sio kumwambia acha kupotosha,sio kauli nzuri,sidhani mzee mukaruka alikusudia kupotosha ila alisema ni kwa mujibu wa mkulima aliyefanya nae mazungumzo.

Sote hapa tupo kwa ajili ya kujifunza kutoka kwa kila mmoja wetu,ndio maana alsaidy tumempongeza kwa kuleta document nzuri ya ufugaji wa kuku wa kionyeji.

mkuu umesema vyema
 
jama kakider kameingia bandan kwangu msaada wa haraka jaman
Kama hukuchanja,kideri haina tiba,vinginevyo hebu wasapoti tu Otc 20%.Kideri ni ugonjwa ambao kimsingi hauna tiba,ndio maana tunahamasisha kufuata ratiba za chanjo.
 
Mkuu Chasha hapo ni suala la nguvu ya soko na nguvu ya pesa yako! Ukiambiwa bei a kitu fulani USA ni dollar moja na huku kwenu kinauzwa kama dollar mia utashangaa au utakataa!? Basi hiyo ni elimu ndogo tu ya nguvu ya pesa yako (kwa maana ya exchange rate!); kwa hiyo nguvu ya soko ndiyo inaongoza kila kitu bradha Chasha.

NI ELIMU NDOGO TU. Na mtoa taarifa wangu hakuwa na sababu yoyote ya kuniongopea na alikuwa anaelezea hali halisi ilivyo huko Tarime/Sirari. Hata hivyo Chasha inawezekana usielewe hili somo kufuatana na uzoefu wako kama ulivyoelezea humu katika jamvi kuhusu bei za hawa KENBRO na wale wengine kadri ulivyopata huko Kenya, sijui ni wapi - Nairobi au Kisii au Kisumu au Migori! Kote huko bei haziwezi kuwa sawa you know it ! Kwa hiyo sikupotosha wala sina tabia hiyo ya kupotosha mambo, kama sijui, nina tabia ya kujifunza na kufanya utafiti.

Asante kwa wana JF mliolizungumzia hili, positively!
 
Kwa mtu kama huyu ataanzaje mkuu
1. Amemaliza form six na yupo chuoni
2. Hana mkopo
3. Anategemea akimaliza chuo ndo aajiriwe

Sasa kwa mtu kama huyu je aanzeje katika kujiajiri. Je mshahara wake wa kwanza akiajiriwa ndo iwe njia au vip..
 
kwa wafugaji wa kuku hapa jf..nahitaji mbolea ya kuku kwa ajili ya kilimo cha matikiti,nipo dar ila shamba lipo mkuranga,naanza mwezi ujao,na ni kwa mara ya kwanza!kama kuna mtu anaweza nisaidia kwa gharama nafuu ili nisafirishe!nahitaji almst 800kg!thanx in advnc
 
Mkuu kichwa yale mayai ya kreki baadhi yametotolewa so majaribio yameonyesha mafanikio
 
Back
Top Bottom