Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Wana-jamvi mimi nina kitabu, cha kufuga kuku wa kienyeji, nimeshindwa kukiweka hapa, mwenye haja ani PM, tafadhali , espescially wewe FIRST LADY, wataka kufuga wa kienyeji!!!!!!
Habari yako mkuu,

Tafadhali ninaomba uni-PM kitabu cha ufugaji wa kuku wa kienyeji maana mie nae ni mfugaji ila napata changamoto sana juu ya hili

Nashukuru sana na ubarikiwe...
 
Ndugu wana jamii forum,ifike wakati tuache kulalamika, tujitume kwa bidii kufanya kazi .Vijana graduates kutoka vyuo mbalimbali tuwaze zaidi kwenye kujiajiri kuliko kuajiriwa,kuajiriwa ni utumwa pia ni hasara kama utapiga vizuri hesabu zako.Kwa wastaafu pia wana fursa ya kutumia mafao yao vyema kwenye miradi ya ufugaji.

Kwa kuanzia tu naruhusu kuulizwa maswali kutoka kwa wale wote wanaojihusisha na ufugaji wa kuku, kama kuna jambo lolote linasumbua na kutaka kupata ufafanuzi .Pia kwa wanaohitaji kuanzisha mradi wa ufugaji wa kuku,utotoreshaji wa vifaranga,biashara ya uchanganyaji na uuzaji wa vyakula vya kuku nk ,kama watanzania tunaweza kusaidiana ili hatimae tuondokane na umasikini.Kila mtu awe msaada kwa watu wengine kwa fani aliyesomea.

Karibuni kwa mjadala.

nimepitia mjadala mwanzo mwsho na nimeupitia muda muafka kwani niko katika maandalizi ya kuanzisha mradi wa kuku wa nyama
 
Tunaendelee kuandika na kuwatumia watu mbalimbali nchini na hata nje ya nchi maandiko ya miradi (Business write up) pamoja na mipango ya biashara (Business Plan),kwa yeyote anayehitaji tuwasiliane.Maandiko yetu ni bora sana na unaweza kutumia hata kuomba mkopo benk na ukapata,wengi wamenufaika.Karibuni sana.
 
Zantsan.. Asante sana mkuu kwa uzi huu ambao ni shule nzuri sana. Asante pia kwa wachangiaji wote. Nimesoma thread yote kwa kweli nimevutiwa sana na elimu niliyoipata kutoka humu. Nashukuru pia kwasababu nimeipata muda ambao naplan ya kufuga kuku and I thank God eneo ninalo.

Kwanza Ntakutafuta mkuu mwisho wa mwezi huu, kwa kupata kitabu, then mdogo mdogo tutakuja kwenye business plan na kuendelea.....
 
Nakupongeza sana kwa kupitia uzi wote,pia hongera kwa hamasa uliyopata.Hakuna sababu ya watanzania kulia umasikini,fursa nyingi tunazo,ni sisi tu kuamua kuzitumia.Karibu sana kwa sasa naona mjadala umedoda kidogo nahisi wengi wamesatisfy na majibu yaliyojibiwa kwa maswali yaliyoulizwa .
 
Mh Kingdom,
Asante kwa kufuatilia mada zangu na hongera kwa kujihusisha na ufugaji wa kuku,hatua uliyofikia ni kubwa sana.Kuku elfu moja wa mayai kama umewatunza vyema tosha kabisa kabisa kukupa faida kubwa na kukuwezsha kujikwamua kiuchumi.

Hiyo kazi yako ya kufanya feasibility study pamoja na Business Plan ziko ndani ya uwezo wetu,wengi tumewfanyia na zimewasaidia sana. Binafsi Shahada yangu ya kwanza nimechukua Bsc.Agricultural economics and Agribusiness,mambo hayo ya kufanya Feasibility study, business plan pamoja na pamoja na project write up,ni miongoni mwa mambo niliyosomea na kuyafanyia kazi kwa undani sana.
Namba zangu nimekutumia,tuwasiliane kwa msaada zaidi.

Mkuu naomba unitumie na mimi izo zako!
 
Mbona unakwepa baadhi ya maswal ndugu, hehehehehe ila asante kwa kutusaide
 
Mbona hujamjibu huyo alietaka hesabu za makadirio kwa kuku wa nyama 300,
 
Mbona unakwepa baadhi ya maswal ndugu, hehehehehe ila asante kwa kutusaide
Hakuna swali ninalokwepa,maswali yote ya kuku yako kwenye uwezo wangu mimi binafsi pamoja na wenzangu.Ila mtu anayehitaji gharama za mradi kwa mfano ufugaji wa kuku 300, nimeshawasiliana naye kupitia pm ,na nimwambia kuwa anatakiwa apate Business plan ambayo itahusisha pia gharama za mradi huo,na business plan tunazitengeza kwa pesa,wengi tu wametoa oda na wengine tayari tumeshawakabidhi kazi zao.
 
asante kaka, mie nishaanza michakato ya utengenezaji wa banda na maandalizi madogo madogo, nia yangu ni kua na mradi wa kuku wa nyama
 
Muda si mrefu nitaanza kutupia gharama mbalimbali za uanzishaji miradi ya kuku,nitaweka gharama za kuku 100,200,300 na kuendelea kadri nafasi itakavyopatikana.
 
Asante sana kwa nafasii hii...Mimi ni mfugaji wa kuku na ninashamba though sina experience sana kwani nimetake ova from family...nina layers.broilers na chotara pia na sasa wanataga.Swali langu ni muda gani natakiwa kutunza mayai kabla sijayapeleka kwa incubator? Na je mayai ya chotara yanavalue sawa na ya kienyeji?
 
Ndaha,
Hongera kwa kujihusisha na ufugaji wa kuku,biashara inayolipa sana ikifanywa kwa kufuata kanuni na misingi ya ufugaji bora wa kuku.
Kwa mayai ya kutotolesha inashauriwa yasikae zaidi ya siku 10,ingawa yanaweza kufika hadi siku 14,ila uwezo wa utotolewaji wa mayai hayo unakuwa umepungua sana.

Kwa ushauri wangu,kama unajishughulisha na utotoleshaji wa vifaranga,ni vizuri ukakusanya mayai kwa siku saba na ile siku ya nane yaingize mayai kwenye machine.Mayai yaliyohifadhiwa kwa siku 7 na kisha kuingizwa kwenye mashine uwezo wake wa kutotolewa unakuwa ni mkubwa sana.

Kuku gani unawatumia kama kuku wazazi wa kukupatia mayai ya kutotolesha,ni hao chotara au,maana ninachojua mimi kuku wa mayai wa kawaida huwezi ukayatumia mayai yake kwenye mchakato wa utotoleshaji.
 
Back
Top Bottom