Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndaha,Asante sana kwa nafasii hii...Mimi ni mfugaji wa kuku na ninashamba though sina experience sana kwani nimetake ova from family...nina layers.broilers na chotara pia na sasa wanataga.Swali langu ni muda gani natakiwa kutunza mayai kabla sijayapeleka kwa incubator? Na je mayai ya chotara yanavalue sawa na ya kienyeji?
Mkuu jifunze kujieleza vizuri ili usaidiwe vizuri, mfano,unataka kuanza na kuku wangapi, je una eneo la kufugia maana kutaja pesa tu hakusaidii kwa kuwa sio wote wanajua mazingira yakonahitaji kupata mchanganuo wa ufugaji wa kuku wa mayai na wa nyama ikiwa ndio nahitaji kuanza mladi huo maana nimeshawishika kufanya biashara hyo nikiwa na mtaji wa milioni moja na nusu 1.5. Nisaidieni ndugu zang
Hapo juu ni cover pages ya moja ya Business plan niliyomtengenezea mmoja wa wateja wangu ambaye anahiatji kuanza mradi wa ufugaji wa kuku wa mayai 5000. Kwa sasa kazi yake imeisha kabisa,nasubiri nimkabidhi ili aweze kuanza mradi wake.I am serious in serving others.
Mheshimiwa Coturnix,mkuu Zanstan,
Kwanza heshima kwako na pongezi nyingi sana kwa jitihada na msaada kwenye jukwaa hili katika sector hii ya ufugaji (poultry farming) , hii sector ni muhimu na inamanufaa makubwa kiuchumi
Naomba msaada kadhaa, moja; ninaweza kupata wapi mbegu ya majani ya Lucerne/alfalfa (lusseni) kwa ajili ya malisho ya kuku, mbili; je ninaweza kupata wapi mayai kwa ajili ya utotoleshaji wa kuku wa nyama na mayai, tatu; ninaweza kupata wapi kuku wazazi (breeders) vifaranga wa nyama na mayai?
Natanguliza shukurani
Ndugu asante sana kwa maelezo safi.Mimi nina layers 1000 sasa na wamenza kutaga lakini speed yao sio nzuri kwani wana miezi 5 na siku kumi kwa siku sasa naoata trey 4..je hii ni kawaida?.Mayai ninayotegemea kutotolesha ni ya chotara ambao ninao kama 200 hivi.
Mheshimiwa Coturnix,
Nakushukuru sana kwa pongezi zako.
Mbegu za majani aina ya Lucerne zinapatikana zaidi nchini kenya kama una mtu kule unafahamiana naye unaweza kumwagiza.Hapa nchini hazipatikani kwa wingi zaidi nenda kaulize kwenye vyuo vya mifugo huwa wanakuwa na hizo mbegu huwa wanaotesha kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi.Mimi binafsu niliwahi kuziona Sumbawanga bwana mmoja mtaalam wa mifugo alikuwa ameotesha shambani kwake na ilikuwa imestawi vizuri sana.Nilimuuliza yeye mbegu kazipata wapi,aliniambia kazitoa kutoka nchini Kenya.
Kuhusu mayai ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai utayapata wapi,kwa kweli hayapatikani kirahisi,serikali kupitia wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi wamekataza uuingizaji wa mayai kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuzuia uenezaji wa magonjwa.Wazalishaji wa vifaranga hapa nchini kwa kiasi kidogo sana huuza mayai kwa ajili ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai lakini mara nyingi inakuwa ni ile ziada na hivyo sio chanzo kizuri sana cha kuaminika cha upataji wa mayai hayo ya kuku wazazi.
Kuku wazazi wa mayai tunawaagiza kutoka uholanzi na kuku wazazi wa nyama tunawaagiza kutoka nchini Kenya wanazalishwa na kampuni ya kutoka nchini Marekani ambao wamefungua tawi lao kenya kwa ajili ya kuhudumia nchi za afrika mashiriki na kati.
Asante sana.
Asante mkuu,mkuu Zantsan, asante sana kwa maelezo na ushauri wa kina
Ningependa kujua kama kuna utaalam au njia yeyote ile artificial au organic ambayo ninaweza kuzalisha wadudu wanaotambaa kama vile sisimizi, mchwa na siafu kwa ajili ya kulisha na kuongeza protein kwa kuku wa kienyeji
Je protein ya aina gani pia inafaa kuwa supplement kwa kuku wa kienyeji?
Natanguliza shukurani
Asante mkuu,
Njia ambayo naifahamu na wengi wanatumia ni ya kutengeneza mchwa na funza kwa kutumia kinyenyesi cha Ng'ombe. Kinyesi hicho humwagiwa maji na kuwekwa kwenye mtungi na kufunikwa kwa masaa 24, baada ya hapo utatakiwa funua mtundi huo,mchwa na funza watakuwa wamejitengeneza, hivyo kuku wanaweza kuruhusiwa kula.