Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko

Asante sana kwa nafasii hii...Mimi ni mfugaji wa kuku na ninashamba though sina experience sana kwani nimetake ova from family...nina layers.broilers na chotara pia na sasa wanataga.Swali langu ni muda gani natakiwa kutunza mayai kabla sijayapeleka kwa incubator? Na je mayai ya chotara yanavalue sawa na ya kienyeji?
Ndaha,
Hongera kwa kujihusisha na ufugaji wa kuku,biashara inayolipa sana ikifanywa kwa kufuata kanuni za ufugaji bora wa kuku.
Kwa mayai ya kutotolewa inashauriwa yasikae zaidi ya siku 10,ingawa yanaweza kufika hadi siku 14,ila uwezo wa utotolewaji wa mayai hayo unakuwa umepungua sana.

Kwa ushauri wangu,kama unajishughulisha na utotoleshaji wa vifaranga,ni vizuri ukakusanya mayai kwa siku saba na ile siku ya nane yaingize mayai kwenye machine.Mayai yaliyohifadhiwa kwa siku 7 na kisha kuingizwa kwenye mashine uwezo wake wa kutotolewa unakuwa ni mkubwa sana.

Kuku gani unawatumia kama kuku wazazi wa kukupatia mayai ya kutotolesha,ni hao chotara au,maana ninachojua mimi kuku wa mayai wa kawaida huwezi ukayatumia mayai yake kwenye mchakato wa utotoleshaji.
 
Attachments

  • front page.jpg
    front page.jpg
    210.1 KB · Views: 193
  • Back page Bp.jpg
    Back page Bp.jpg
    78.8 KB · Views: 180
Hapo juu ni cover pages ya moja ya Business plan niliyomtengenezea mmoja wa wateja wangu ambaye anahiatji kuanza mradi wa ufugaji wa kuku wa mayai 5000. Kwa sasa kazi yake imeisha kabisa,nasubiri nimkabidhi ili aweze kuanza mradi wake.I am serious in serving others.
 
nahitaji kupata mchanganuo wa ufugaji wa kuku wa mayai na wa nyama ikiwa ndio nahitaji kuanza mladi huo maana nimeshawishika kufanya biashara hyo nikiwa na mtaji wa milioni moja na nusu 1.5. Nisaidieni ndugu zang
 
Mkuu jifunze kujieleza vizuri ili usaidiwe vizuri, mfano,unataka kuanza na kuku wangapi, je una eneo la kufugia maana kutaja pesa tu hakusaidii kwa kuwa sio wote wanajua mazingira yako
 
habari waungwana... Mimi ni mjajisiliamali mpya ninayehitaji kuanza kufuga kuku wa mayai nimesoma topics zote zinazohusu ufugaji wa kuku hawa wa kisasa lakini cjapata mchanguno halisi nina mtaji wa kutosha kama 1.5m kwaajili ya kuanza shughuli hyo naomba msaada wenu...
 
habari mzee makaruta, hv hapo mikocheni B wanakiingilio ama ni bule na kama kuna kiingilio ni kiasi gani?
 
Hapo juu ni cover pages ya moja ya Business plan niliyomtengenezea mmoja wa wateja wangu ambaye anahiatji kuanza mradi wa ufugaji wa kuku wa mayai 5000. Kwa sasa kazi yake imeisha kabisa,nasubiri nimkabidhi ili aweze kuanza mradi wake.I am serious in serving others.

mkuu Zanstan,

Kwanza heshima kwako na pongezi nyingi sana kwa jitihada na msaada kwenye jukwaa hili katika sector hii ya ufugaji (poultry farming) , hii sector ni muhimu na inamanufaa makubwa kiuchumi

Naomba msaada kadhaa, moja; ninaweza kupata wapi mbegu ya majani ya Lucerne/alfalfa (lusseni) kwa ajili ya malisho ya kuku, mbili; je ninaweza kupata wapi mayai kwa ajili ya utotoleshaji wa kuku wa nyama na mayai, tatu; ninaweza kupata wapi kuku wazazi (breeders) vifaranga wa nyama na mayai?

Natanguliza shukurani
 
------- wewe.....mpaka leo hujui kujieleza?haya nijibu.una ardh?nyumba ya kuku au banda?eneo lako kuna wafugaj wa kuku?
 
ahsanteni sana kwa kunifunza kujieleza wanandugu...
Ni hivi, eneo la kufugia/banda la kuwekea kuku hao lipo la kutosha ila kikubwa ninachokihitaji ni kupata mchanganuo wa kuku wa mayai na wanyama na kujua kati ya wale wa mayai na wale wa nyama wapi wanafaida watakaonifanya nifaidike maana naona soko la kuku ni kubwa sana nami nahitaji kuwekeza katika biashara hyo ili kujikwamua.. Natumai nimejieleza vyema... DANCAN and Tizo 1
 
Kimsingi kuku wa nyama ni wazuri kufuga kama una weza kumudu mambo yafuatayo BILA KUKOSEA HATA KIDOGO.
1.KWANZA KUPATA SOKO LA UHAKIKA BAADA YA KUKU KUFIKISHA WIKI NNE MPAKA TANO.HATA ZIKIZIDI SIKU MBILI HAUJAUZA NI HASARA SANA.
2.KUKU WA NYAMA WANAHITAJI SANA MATUNZO NA DAWA PASIPO UJANJA UJANJA.
3.KIFARANGA KINAKUWA BAADA YA WIKI NNE HADI TANO NA KUWA KUKU KAMILI..MUDA HUWA NI MFUPI SANA KWA KUPATA SOKO ZURI.UKIKOSA SOKO HASARA YAKE YAWEZA UKALA MPAKA MTAJI.

KUKU WA MAYAI NA FAIDA ZAKE.
1.WANAANZA KUTAGA WAKIWA NA MIEZI 5 HADI SITA,KUTOKANA NA UBORA WA CHAKULA ULICHOWAPA.
2.WAKIANZA KUTAGA NI MIAKA MIWILI MPAKA MIWILI NA NUSU....
3.HAWA NI WAZURI SANA KWA MFUGAJI ANAEANZA KAMA WEWE KWANI MAYAI YANAWEZA KUVUMILIA UKIKOSA WATEJA.
4.WAKIFIKISHA MIEZI MIWILI NA KUENDELEA MATUNZO YANAKUWA RAHISI SANA.UNAWEZA UKAFANYA KAZI NYINGINE KAMA ZIPO.
Ushauri wangu ufuge kuku wa mayai ni wazuri sana kwa kipato.kuku wa nyama wanakula sanaaa.hivyo ukikosa soko utalia.miongozo ya kufugia kuku ninayo katika hard copy..
 
mkuu Zanstan,

Kwanza heshima kwako na pongezi nyingi sana kwa jitihada na msaada kwenye jukwaa hili katika sector hii ya ufugaji (poultry farming) , hii sector ni muhimu na inamanufaa makubwa kiuchumi

Naomba msaada kadhaa, moja; ninaweza kupata wapi mbegu ya majani ya Lucerne/alfalfa (lusseni) kwa ajili ya malisho ya kuku, mbili; je ninaweza kupata wapi mayai kwa ajili ya utotoleshaji wa kuku wa nyama na mayai, tatu; ninaweza kupata wapi kuku wazazi (breeders) vifaranga wa nyama na mayai?

Natanguliza shukurani
Mheshimiwa Coturnix,
Nakushukuru sana kwa pongezi zako.
Mbegu za majani aina ya Lucerne zinapatikana zaidi nchini kenya kama una mtu kule unafahamiana naye unaweza kumwagiza.Hapa nchini hazipatikani kwa wingi zaidi nenda kaulize kwenye vyuo vya mifugo huwa wanakuwa na hizo mbegu huwa wanaotesha kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi.Mimi binafsu niliwahi kuziona Sumbawanga bwana mmoja mtaalam wa mifugo alikuwa ameotesha shambani kwake na ilikuwa imestawi vizuri sana.Nilimuuliza yeye mbegu kazipata wapi,aliniambia kazitoa kutoka nchini Kenya.

Kuhusu mayai ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai utayapata wapi,kwa kweli hayapatikani kirahisi,serikali kupitia wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi wamekataza uuingizaji wa mayai kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuzuia uenezaji wa magonjwa.Wazalishaji wa vifaranga hapa nchini kwa kiasi kidogo sana huuza mayai kwa ajili ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai lakini mara nyingi inakuwa ni ile ziada na hivyo sio chanzo kizuri sana cha kuaminika cha upataji wa mayai hayo ya kuku wazazi.

Kuku wazazi wa mayai tunawaagiza kutoka uholanzi na kuku wazazi wa nyama tunawaagiza kutoka nchini Kenya wanazalishwa na kampuni ya kutoka nchini Marekani ambao wamefungua tawi lao kenya kwa ajili ya kuhudumia nchi za afrika mashiriki na kati.
Asante sana.
 
nawezaje kupata mawasiliano yako na hatimae kuonana na wewe ndugu ili kuweza kupata somo zaidi na hyo hard copy itakayoweza kuniongoza kufikia malengo tarajiwa na endelevu? Tizo 1
 
Last edited by a moderator:
Ndugu asante sana kwa maelezo safi.Mimi nina layers 1000 sasa na wamenza kutaga lakini speed yao sio nzuri kwani wana miezi 5 na siku kumi kwa siku sasa naoata trey 4..je hii ni kawaida?.Mayai ninayotegemea kutotolesha ni ya chotara ambao ninao kama 200 hivi.
 
Ndaha, unaenda vizuri ingawa uko nyuma kwa nusu trey.
 
Mheshimiwa Coturnix,
Nakushukuru sana kwa pongezi zako.
Mbegu za majani aina ya Lucerne zinapatikana zaidi nchini kenya kama una mtu kule unafahamiana naye unaweza kumwagiza.Hapa nchini hazipatikani kwa wingi zaidi nenda kaulize kwenye vyuo vya mifugo huwa wanakuwa na hizo mbegu huwa wanaotesha kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi.Mimi binafsu niliwahi kuziona Sumbawanga bwana mmoja mtaalam wa mifugo alikuwa ameotesha shambani kwake na ilikuwa imestawi vizuri sana.Nilimuuliza yeye mbegu kazipata wapi,aliniambia kazitoa kutoka nchini Kenya.

Kuhusu mayai ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai utayapata wapi,kwa kweli hayapatikani kirahisi,serikali kupitia wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi wamekataza uuingizaji wa mayai kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuzuia uenezaji wa magonjwa.Wazalishaji wa vifaranga hapa nchini kwa kiasi kidogo sana huuza mayai kwa ajili ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai lakini mara nyingi inakuwa ni ile ziada na hivyo sio chanzo kizuri sana cha kuaminika cha upataji wa mayai hayo ya kuku wazazi.

Kuku wazazi wa mayai tunawaagiza kutoka uholanzi na kuku wazazi wa nyama tunawaagiza kutoka nchini Kenya wanazalishwa na kampuni ya kutoka nchini Marekani ambao wamefungua tawi lao kenya kwa ajili ya kuhudumia nchi za afrika mashiriki na kati.
Asante sana.

mkuu Zantsan, asante sana kwa maelezo na ushauri wa kina

Ningependa kujua kama kuna utaalam au njia yeyote ile artificial au organic ambayo ninaweza kuzalisha wadudu wanaotambaa kama vile sisimizi, mchwa na siafu kwa ajili ya kulisha na kuongeza protein kwa kuku wa kienyeji

Je protein ya aina gani pia inafaa kuwa supplement kwa kuku wa kienyeji?

Asante mkuu,
Njia ambayo naifahamu na wengi wanatumia ni ya kutengeneza mchwa na funza kwa kutumia kinyenyesi cha Ng'ombe. Kinyesi hicho humwagiwa maji na kuwekwa kwenye mtungi na kufunikwa kwa masaa 24, baada ya hapo utatakiwa funua mtundi huo,mchwa na funza watakuwa wamejitengeneza, hivyo kuku wanaweza kuruhusiwa kula.
 
mkuu, nakushukuru sana sana
 
Mheshimiwa Coturnix,
Nakushukuru sana kwa pongezi zako.
Mbegu za majani aina ya Lucerne zinapatikana zaidi nchini kenya kama una mtu kule unafahamiana naye unaweza kumwagiza.Hapa nchini hazipatikani kwa wingi zaidi nenda kaulize kwenye vyuo vya mifugo huwa wanakuwa na hizo mbegu huwa wanaotesha kwa ajili ya mafunzo kwa wanafunzi.Mimi binafsu niliwahi kuziona Sumbawanga bwana mmoja mtaalam wa mifugo alikuwa ameotesha shambani kwake na ilikuwa imestawi vizuri sana.Nilimuuliza yeye mbegu kazipata wapi,aliniambia kazitoa kutoka nchini Kenya.

Kuhusu mayai ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai utayapata wapi,kwa kweli hayapatikani kirahisi,serikali kupitia wizara ya maendeleo ya mifugo na uvuvi wamekataza uuingizaji wa mayai kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuzuia uenezaji wa magonjwa.Wazalishaji wa vifaranga hapa nchini kwa kiasi kidogo sana huuza mayai kwa ajili ya utotoleshaji wa vifaranga wa nyama na mayai lakini mara nyingi inakuwa ni ile ziada na hivyo sio chanzo kizuri sana cha kuaminika cha upataji wa mayai hayo ya kuku wazazi.

Kuku wazazi wa mayai tunawaagiza kutoka uholanzi na kuku wazazi wa nyama tunawaagiza kutoka nchini Kenya wanazalishwa na kampuni ya kutoka nchini Marekani ambao wamefungua tawi lao kenya kwa ajili ya kuhudumia nchi za afrika mashiriki na kati.
Asante sana.

huku Kibaha kuna mtu namjua anayo hii Lucerne
 
Back
Top Bottom