Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Ukiwa na huyo inabidi ujiandae na majike wakutosha maana hao Galla sifaya yao madume ni uwezo wa kupanda na kupigana bila ya kuchoka ka Boer, Hapa nyumbani kapiga Dume alilo likuta hapa li mekuwa bwege kabisa sasahivi
 
upande wa chanjo za msingi ikoje
 
upande wa chanjo za msingi ikoje
Kwakweli swala la chanjo nilakushirikisha Vet maana unaweza ukafanya chanjo kumbe hujafanya kwa wakati muafaka au ukawa umetoa dozi ndogo au umetumia chanjo isiyo stahiki nisinge penda kutoa ushauri usio wakitaalamu isije kuleta madhara kwenye zizi lako.
Nasisitiza tumia Vet mwenye kuelewa na atakupa elimu nzuri ya chanjo kuliko mfugaji mwenzako.
 
Sorry mdau hv utamjuaje kua huyu ni GALLA? Liko vzr sana!! Sema bei imechangamka sio poa
Galla ana njia kuu za kumtambua. 1, uso wake sio mrefu kama Mbuzi wa kawaida.
2,sehemu zake za siri chini ya mkia ni nyeusi.
3,sehemu za mdomo wake lips ni nyeusi.
4,Ngozi yake juu ikiwa nyeupe chini ya manyoya atakuwa mweusi.
5,Dume la Galla/Isiolo huwa ni kati ya madume yenye nguvu sana ya kupanda bila kuchoka.
6, Chini ya shingo yake baada ya kidevu kuna nyama inashuka hapo kama baadhi ya picha zilivyojionyesha nilizo zituma.
7,Miili yao mikubwa naimejaa nyama sana.
Nafikiri hapo umenielewa ndugu karibu sana tujifunze pamoja.
 
Asante kiongozi!! Mpaka hapo nimekuelewa!! Vp jike lake GALLA linaweza kuzaa watoto mapacha?
 
Asante kiongozi!! Mpaka hapo nimekuelewa!! Vp jike lake GALLA linaweza kuzaa watoto mapacha?
Kwakweli wapo ila mimi bado sijabahatika kuwa nao ila kuna mahala nime agizia ni nunuwe mama pamoja na watoto wake wote
 
Nipo Dar ndugu wanapatikana bila shida wewe upo mkoa gani

nipo dar mzee natamani kuja kuona na kujifunza kwako
Ndugu karibu sana hili ni zawadi yetu sote kwa Mungu njoo chemba tupeane mawasiliano, niko all weekend karibu sana.
 
Niseme kitu kimoja jamani tuliopo kwenye ajira tuanze sasa kutayarisha mashamba yetu kwa anae weza mifugo na kilimo na aliyepo na nafasi ayaendeleze pale alipo fikia kuna maisha ya baadae yanayo tuhitaji hasa sisi waajiriwa baada ya ajira.
 
Tena Sana mkuu hili me nmeliona mapema sana
Niseme kitu kimoja jamani tuliopo kwenye ajira tuanze sasa kutayarisha mashamba yetu kwa anae weza mifugo na kilimo na aliyepo na nafasi ayaendeleze pale alipo fikia kuna maisha ya baadae yanayo tuhitaji hasa sisi waajiriwa baada ya ajira.
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu, poleni na maombelezo ya Rais wetu, lakini tukumbuke Mazizi ya mfugo wetu mpendwa Mbuzi yanatuhitaji, kumekuchaje huko?
 
Mungu ni mwema mkuu harakati zinaendelea vyema
Nawasalimuni kwa jina la Mungu, poleni na maombelezo ya Rais wetu, lakini tukumbuke Mazizi ya mfugo wetu mpendwa Mbuzi yanatuhitaji, kumekuchaje huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…