Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Tumeanza taratibu sasa, nawasalimuni nyote kwa jina la Mungu. Isiolo/Galla wameanza kutupatia wajukuu taratibu, tunamshukuru Mungu kwa kila jambo.

20211205_072316.jpg


20211205_072325.jpg


20211205_072330.jpg


20211205_072338.jpg
 
Mbuzi wangu wamegoma kabisa kulamba hili jiwe . Kwako mfugaji uliwezaje kuwazoesha mbuzi wako jiwe hili
Liache humo kwenye banda lao watalilamba tu kuna wakati wanakuwa kama wanakiburi na pia jitahidi uwe unawapatia chumvi kwenye chakula chao hasa pumba pindi uwapatiapo.
 
..labda kwasababu hukuwaanzisha kulamba hilo jiwe tangu wakiwa wadogo.
Nayo pia inaweza kuwa sababu lakini watalizoe tu kuna Mbuzi kwangu alikuwa hali maganda ya ndizi nilikuwa nampatia kila mara baada ya miezi 2 aliyatafuna mweneyewe😂😂
 
wakuu nawashukuruni sana kwa michango yenu na kututia moyo sisi tunaotaka kuanza ufugaji..

mimi nataka kununua shamba nijenge mabanda kwaajili ya mbuzi mnanishauri nini!? zaidi nauliza hidroponic fodder na azolla zinawafaa hawa viumbe kwaajili ya kupunguza gharama ya chakula!?..

nawashukuru sana in advance..

wakaliwetu Manchid JokaKuu na wengineo..
@Kazakh destroyer yes hydroponic fodder zinafaa kulisha.
Swali ni je unajua kuotesha?
 
Bei ya mbuzi mwenye mimba ina kwendaje?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Habari za leo ndugu kwaupande wangu sijawahi kuuza hivyo lakini naamini itategemeana na maeneo husika na mahitaji ya muuzaji, maana kuuza mwenye Mimba lazima mfugaji atakuwa amebanwa na hana njia mbadala lazima amtoe mwenye Mimba.
 
Nahitaji kununua mbuzi wa kufuga tafadhali je wapi naweza kuwapata wa kununua hata majike 5 na madume wawili tafadhali.....
 
Back
Top Bottom