Naomba kujua kama inawezekana kumpandisha nguruwe / artificial insemination kama vile wanafanya kwenye ngombe???? Mwenye kujua hii nahitaji msaada wako
Kujua mlipo haisaidii sana,tunachotaka twambie bei zenu na wa mikoani mnasafirisha?Jamani ckuwa hewani kwa muda bt kifupi ni kwamba tuko kisenvule karibu na kiwanda cha rhino cement wilaya ya mkuranga
Wana jamvi,katika pita pita zangu mitaani,na kwenye mitandao ya kijamii nimegundua njia pekee itakayonipa ajira ni kujikita katika ufugaji wa Nguruwe kitaalam na kibiashara zaidi ikizingatiwa ndo kwanza nimehitimu elimu yangu ya Chuo kikuu..Nna shamba la ukubwa wa ekari 5 huko kijijini kwetu,maji yapo ya kutosha.Swali ni je shilingi milioni kumi (10,000,000) zinatosha kuanza kufuga nguruwe wangapi tangu wakiwa watoto hadi umri wa kuwauza? Naomba mnisaidie wadau
Naona umeingia choo cha kike mzee, pole sana. Ila kama umetukana basi matusi hayo yakurudie mwenyewe. laiza.
Inawezekana sana tena ni rahisisana,unakuwa na dume moja tu unalikamua mbegu likikojoa mbegu mala moja hizo mbegu unapandishia majike 14,
bigurube hiki sio choo cha kike. nimekupa mawaidha tu na busara ingekutuma uombe tafsiri..kukusaidia tu..."imeharamishwa kwenu damu, na maiti na nyama ya nguruwe" hiyo ndio tafsiri yake
Pitia huu uzi utafaidikaHabari za leo wadau. Naomba kuuliza eti Nguruwe hula maboga pekee na akila mboga ya maboga anakufa? Maana nimeanza ufugaji wa Nguruwe na jirani yangu amenambia hivyo, Je ni kweli?
Nguruwe toka azaliwe mpaka afae kuvunwa ni miezi sita mpaka saba lakini kuna mambo ya kuzingatia mpaka uweze kumvuna kwa umri huo
,Aina ya nguruwe
2,Aina ya chakula unachomlisha
3,Hali ya hewa pamoja na mabanda yako.
Aina ya nguruwe huwa ina impact kubwa mno kwenye ukuaji mfano nguruwe wanaitwa Duroc wanakuwa haraka mno na wana uzito mkubwa kulinganisha na yorkshore au Landrace,ukimlisha vzuri kumkuta na kg80 ndani ya miez saba c kitu cha kusadikika na wana mafuta machache kwenye ngozi
Aina ya chakula kama utamlisha nguruwe majani au mboga mboga kwa wingi bila nafaka zilizochanganywa na vitu vingine kwa uwiano sahihii basi jua kwamba nguruwe utamfuga mwaka na hato faa kuvunwa hata kama ni mbegu nzuri vp
Mwisho kabsa hali ha hewa japo c sana ila inahusika