Ramea
JF-Expert Member
- Mar 19, 2015
- 2,146
- 4,084
Huyo kwenye Avatar ni mbegu bora baada ya kushauriwa na wataalamu ni kaenda Misheni ya jirani, wao wanauza nguruwe mzima kwa kumpima kwenye mizani. Mwenye mimba anauzwa kg1 kwa 4500 na hasiyepandishwa kg1 tsh 4000. Wapo midume wenye kilo zaid ya 220...lakini Mimi nilimchukuwa jike ambaye kilo zake nililipa karibu 600,000/-.Tafuta mbegu bora.... epuka na inbreeding(mbegu nyingi zilizopo sokoni zimeshachakachuliwa sana na inbreeding hivyo wanakula tuu hawaongezeki uzito inavyopaswa)
Nipo kwenye mgrupu ya whasap wafuga nguruwe mengi na tunashea mengi lakini tunafarijiana tu, hii ni biashara kichaa. Haina faida, ni ngumu. Nina experience had ya kuchoma sindano mwenyewe kwa jinsi nilivyoiva kiufugaji, lakini tusidanganyane, mfugo mgumu sana.