Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

mkuu umeniinspire sana ,,lazima nijipange kufanya hii kitu
 
Kwa anayefahamu kuhusu nguruwe jike mwenye mimba anieleze sababu zinazopelekea nguruwe jike kuzaa watoto chini ya watano na tumbo bado kuonekana lina watoto ndani na zipi process inabidi zifwate.
 
Naamini wote mnaendelea vzuri na pia ambao hawajisikii vizuri Mungu awawekee mkono wake,,ndugu zangu mm nataka nianzee kufuga nguruwe na nna mtaji wa laki 800000.swali la kwanza je unatosha kwa gharama za kununulia piglets na gharama zote za vyakula?? Na pia gunia la pumba Na mashudu ntapata wap kwa bei ya chini na soko pia lamaana maana huwezi kufanya Biashara bila soko ,,,Nawatakia kheri ya Christmas na mwaka mpya (samahani kwa watu wa imani za kiislamu kwa hili)
 
Naamini wote mnaendelea vzuri na pia ambao hawajisikii vizuri Mungu awawekee mkono wake,,ndugu zangu mm nataka nianzee kufuga nguruwe na nna mtaji wa laki 800000.swali la kwanza je unatosha kwa gharama za kununulia piglets na gharama zote za vyakula?? Na pia gunia la pumba Na mashudu ntapata wap kwa bei ya chini na soko pia lamaana maana huwezi kufanya Biashara bila soko ,,,Nawatakia kheri ya Christmas na mwaka mpya (samahani kwa watu wa imani za kiislamu kwa hili)
 
Hiyo ni mradi mzuri cha msingi fanya utafiti wapi utapata mbegu nzuri za nguruwe wanao kua haraka na kula kidogo wasiliana na tapifa
 
==========

USHUHUDA

======================================================[/QUOTE]
Banda 300,000
Piglets 80,000
Mpagazi 40,000 per month
Umebaki na 80,000

Nguruwe ni atleast afikishe miezi 6 au 7 ili uweze kuuza na wewe umemnunua akiwa na miezi miwili so inakupa muda wa miezi 4 ili apandishwe na mimba ya nguruwe ni miezi 3 wiki3 na siku 3 pia usishau kuwa itabidi anyonyeshe kwa muda wa miezi miwili thus unahitaji kulisha nguruwe huyo jike kwa jumla ya miezi isiyopungua (4+4+2)=10.

Now kwa jike ni miezi 10 ina siku 300
Assume anakula kilo 2-3+maji+majani= Tzs. 600

Then gharama ya chakula ni 600x300= Tzs. 180,000
gharama ya mpagazi ni 20,000x10=Tzs.200,000
gharama ya dawa ni =Tzs. 50,000
Jumla 330,000 kwa jike NB: Bei ya kuuza jike ni 200,000- 300,000

kwa dume atahitaji miezi 4 hadi 5 toka uipo mnunua ambazo assume ni siku 130
Then
gharama ya chakula ni 600x130= Tzs. 78,000
gharama ya mpagazi ni 20,000x5= Tzs.100,000
gharama ya dawa ni = Tzs. 20,000
Jumla = 198,000 kwa dume remind you bei kuuza dume max, ni 200,000

Thus 528,000+420,000= 968,000.



Ushauri ni kwamba gharama za uendeshaji ni kubwa (528,000) kuliko hela uliyobaki nayo (80,000) tafuta njia za kupunguza gharama za uendeshaji wa mradi ili kuweza kupata faida. Pia mbegu nzuri ya nguruwe ndio issue.
Pia nguruwe wanavyozidi kuongezeka na gharama za uendeshi nazo huongezeka sambamba
 
1.mtaji
2.changamoto zake
3.profit and loss calculation
4.market
5.any other advice
Karibuni wajuzi
 
changamoto kubwaa ni garama ya chakula-hasa kama unafugia mjini,,
 
Kuhusu mtaji sifahamu sehemu kama dar kwa nguruwe mkubwa unaetaka kumkuza anauzwa sh ngapi kwa sababu hujaweka bayana kama unaanza na watoto au wakubwa wa kukuza haraka. ila kwa range ya watoto mpaka mkubwa sina uhakika kama itavuka hii range 60,000 - 230,000/= Tsh hapo ondoa gharama ya nyumba kabisa na usafiri na nyingine ndogondogo mpaka wanafika nyumbani.

Hakikisha utafute mbegu nzuri wale warefu kabisa japo wana gharama ila ukiweza kuwatunza watakulipa.

Changamoto zake
hawa wanyama wanakula sana narudia tena wanakula sana, kwa hiyo kama utaamua kuwalisha polard na mashudu ya alizeti peke yake utakula hasara sana. Inakubidi utafute mabaki ya vyakula na matunda mfano buguruni matunda ni mengi na masokoni kama unaweza upate cha kutosha wakaanga chips chukua mabaki ya maganda ya viazi. Pia unaweza kwenda pale kiwanda cha bia ukawaomba kimea cha bia maana wale huwa wanaenda kukitupa ni kizuri huwa wanakuwa haraka sana.Take it from me kama ukiwapunguzia chakula wakawa hawali na kushiba basi kuwa na uhakika watachelewa kukua watachelewa kukupa matokeo unayotaka. Magonjwa ni kawaida uwe karibu na daktari wa mifugo hapa hakuna gharama kubwa sana. Kikubwa zaidi ni gharama ya chakula.

Profit and loss calculation.
Kikubwa zaidi kila unapoenda kuchukua chakula cha nguruwe andika, usafiri n.k pesa inayotoka mfukoni weka pale na pia usiweke siku unazofanya kazi nao. nikisema nikuambie ni magunia mangapi watakula mpaka umeuza kweli hapo sijui. Kama wanakula vizuri miezi 8-9 unaweza kuuza. Tena sehemu kama dar unaweza kuchinja na kuuza kama nyama na utapata hela nzuri.

Market.
Kwa sehemu kama dar silijui soko lake sana ila ukienda maeneo ya tabata na kimara utakutana na sehemu nyingi sana wanauza kitimoto ya kupikwa hao wanaweza kuwa wateja wako.

hayo ndo nayoyajua kutokana na uzoefu wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…