Habarini wana jamvi,mimi ni kijana mwenye umri kati ya 30-40,naishi Dar es Salaam,ni nimuajiriwa.
Nina wazo ningependa kuwashirikisha,natamani tupatikane vijana 10 wenye kupenda maendeleo na kujituma,na angalao wasiwe wote waajiriwa wengine wawe ni watu waliojiajiri na awe na uwezo wa kuwa na mtaji wa milioni mbili,huu mtaji usiwe ndo utegemee kula yako na nauli hapana ni project ya muda mrefu,faida ni baada ya mwaka au miaka miwili.
Tukiziunganisha watu kumi tutapata 20milion ambayo cha kwanza tupate ardhi ekar 10,na kila ekar itamilikishwa mtu mmoja.Kwa mfano maeneo ya chanika au kisarawe ambayo bei ya ekari moja kwa maeneo haya inacost kati ya laki mbili mpaka milion moja na nusu inategemea na umbali!then tuanze na nguruwe wachache ambao tutawamudu kwa hela itakayobaki baada ya kununua shamba.
Na project iwe ni ya mipango ya muda mrefu.long term plan project)tusitegemee faida ya mda mfupi.
Au tukatafuta maeneo ambayo maji ya Dawasco yamefika bei ya haya maeneo imechangamka kidogo bei inaanzia milioni moja na nusu mpaka kumi kwa ekari(maeneo njia ya moro-dar)huku tukipata hata ekar tano kwa milioni mbilimbili ambayo jumla itakua ni milion kumi kwa ekar tano,then utaratibu utakua uleule tutagawa nusu ekar equal,after that tutaanza project kwa pamoja.
Mwenye mawazo mengine,ushauri,nyongeza namkaribisha
Sent using
Jamii Forums mobile app