Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ufugaji wa samaki kama ilivyo shughuli nyingine yoyote ya kiuchumi inahitaji usimamizi mzuri ili uweze kuwa na faida. Mbali na hilo, mfugaji wa samaki anatakiwa kuzingatia vigezo vingi kabla ya kuanza ufugaji. Moja ya vigezo hivyo ni soko. Si jambo la busara kuanza shughuli yoyote kabla haujafanya uchunguzi na kujua kama kuna mahitaji ya bidhaa unayokusudia kuzalisha. Wafugaji wengi wameanzisha ufugaji wa samaki lakini wakaishia kupata hasara kutokana na ukosefu wa soko. Na wengine wameanguka kutokana na utunzaji mbovu wa mabwawa ya samaki.
-
*Maji*
Upatikanaji wa maji na ubora wake ni kigezo muhimu katika ufugaji wa samaki. Mtiririko wa maji ni njia rahisi kwa mfugaji. Maji machafu hayatakiwi kwa ufugaji wa samaki. Wafugaji ni lazima wasaidiwe na maafisa kilimo katika eneo lao kama maji yanayopatika yana ubora kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Kwa wakazi wa Dar es Salaam, inawezekana pia kufuga samaki kwenye bwawa, endapo maji yana chumvi ya wastani, na kwa kiwango kinachoshauriwa kitaalamu, basi samaki wanaweza kustahimili, na kukua vizuri.
-
*Bwawa*
Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.
-
Utengenezaji wa bwawa la samaki kwa maeneo yenye udongo wa kichanga kama Dar es Salaam, mfugaji atalazimika kuchimba na kuweka karatasi ya nailoni. Hii, itasaidia kuzuia upotevu wa maji pamoja na kuzuia bwawa kuporomoka.
-
Ni vyema upande mmoja wa bwawa ukawa na kina kirefu kuliko mwingine. Upande mmoja unaweza kuwa na kina cha mita moja na nusu, na mwingine mita moja. Hii itamsaidia mfugaji kuweza kulihudumia bwawa vizuri, hata kama ni kuingia na kufanya usafi.
-
*Utunzaji wa bwawa*
Inashauriwa kufanyia bwawa usafi mara kwa mara, hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Pia ukiacha mimea bwawani itatumia virutubisho kwa kiasi kikubwa na kuondoa hewa ya oxijeni.
Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.
-
*Ulishaji*
Wafugaji walio wengi, wamekuwa hawazingatii kanuni za ulishaji wa samaki. Kwa kawaida inatakiwa kuwalisha samaki mara mbili hadi mara tatu kwa siku.
-
*Aina ya chakula*
Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa. Haishauriwi kulisha chakula kilichoko kwenye mfumo wa vumbi, bali kiwe mabonge madogo madogo, kwa wastani wa tambi.
-
*Magonjwa*
Kwa kawaida samaki hawana magonjwa mengi sana yanayowashambulia, ila kuna baadhi ya yaliyozoeleka kama vile magonjwa ya ukungu (fangasi), magonjwa yatokanayo na virusi, pamoja na minyoo.
-
Samaki wanaposhambuliwa na fangasi, huonekana kwa macho kwa kuwa huwa na madoa madoa. Samaki aina ya kambale hushambuliwa zaidi kuliko perege.
-
Pia unaweza kutambua kuwa samaki ni mgonjwa kwa kuwa huzubaa sehemu moja kwa muda mrefu. Magonjwa kwa samaki pia yanaweza kutokana na mrundikano kwenye bwawa. Hivyo, ni muhimu kuwapunguza kila wanapoongezeka.
-
*Tiba*
Tiba iliyozoeleka kwa samaki ni kwa kuweka chumvi kwenye maji, kasha kuwatumbukiza samaki unaowaona kuwa ni wagonjwa, kisha kuwatoa na
kuwarudisha bwawani.
-
*Upatikanaji*

Unaweza kupata vifaranga wa samaki kutoka katika kituo cha kuzalisha na kufuga samaki Kingolwira Morogoro. Bei ya kifaranga cha Perege ni shilingi 50, na Kambale ni shilingi 150.....
 
Nami nimenufaika sana kwa michango ya wadau wa hili jukwaa, hakika JF ingekuwa hivi kila siku hakuna ambaye angebaki nyuma kimaendeleo. Nami napenda kuongezea nondo zifatazo kwajili ya ufugaji samaki.

1.Namna ya kuzalishaji wa vifaranga bora wa SAMAKI

i.Chagua samaki wazazi wazuri kulingana na umbile lao kama rangi, ukubwa, afya na sura zao. Samaki hawa watengwe na wale wasio na sifa hizo na wasiruhusiwe kuzaliana nao. Mfugaji anaweza kununua wazazi hawa kutoka katika chanzo kinachofahamika kuwa kina samaki bora.

ii.Dhibiti ubora wa samaki hawa wazazi kwa kutoruhusu miingiliano na samaki wenye ubora hafifu. Chuja vema maji yanayoingia bwawa. Ikiwezekana, tumia samaki wenye ukubwa wa zaidi ya gramu 100. Hii itakuwezesha kutenganisha wazazi kutoka kwa vifaranga kila baada ya kuzaliwa (reproduction cycle).

.Endelea kuwatumia wazazi hawa kila unapohitaji vifaranga kutegemeana na jinsi wanavyoendelea kuzaa vifaranga bora. Pamoja na ubora wa wazazi hawa, kuna umuhimu wa kuchagua na kuwaondoa vifaranga wasio kuwa na ubora unaohitajika au ambao ubora wao unatiliwa mashaka (culling).

iii.Ni muhimu mfugaji afahamu uzuri wa kutumia vifaranga bora. Kausha bwawa kabisa angalau mara moja kila baada ya miezi sita hadi nane ili kuondokana na samaki wasio na ubora unao hitajika, kuua maadui wa samaki na kuondokana na hali ya kuwa na samaki wengi kwenye bwawa zaidi ya kiwango kinachotakiwa na pia hali ya samaki kuzaliana kinasaba “inbreeding”. “Culling na grading” ni muhimu kuanza baada ya siku 30 hadi 45 baada ya samaki wakubwa kuwa wamewekwa kwenye bwawa na hufanyika kwa kutumia kawavu kadogo ambacho kina matundu madogo.
Endelea kufanya kazi hii kila baada ya wiki mbili hadi nne.

2.URUTUBISHAJI WA BWAWA NA ULISHAJI WA SAMAKI

i.Mfugaji anashauriwa kuweka mbolea ya asili kama Mboji na samadi kwenye maji kabla ya kupandikiza samaki. Hii ni muhimu kwani samaki watakaopandikizwa, watahitaji chakula siku hiyo hiyo na chakula chao cha awali huwa ni vijimea na vijidudu vilivyomo ndani ya maji. Vyote hivi huwepo kwa wingi kwenye maji yenye rutuba.

ii.Iwapo maji yatakuwa yamerutubishwa vema, chakula cha ziada huhitajika kwa kiasi kidogo sana, kama (2-3%) ya uzito wa samaki husika kwa siku. Ni vema samaki wakalishwa angalau mara mbili, kiasi kidogo asubuhi ya kati ya saa tatu na nne na jioni kati ya saa 10 na 11. Pia ni vema kama eneo la kulishia ikawa ni sehemu moja ili kuwazoesha samaki kuja eneo hilo muda wa kulisha na kuwawezesha kula sehemu kubwa ya chakula watakachopewa.

3.KUZALIANA KWA WINGI NDANI YA BWAWA NA NJIA ZA KUDHIBITI

KUWEPO KWA SAMAKI WENGI KULIKO IDADI INAYOTAKIWA NDANI YA BWAWA (OVERPOPULATION IN PONDS)
1.Kwa kawaida, samaki jamii ya perege wako katika makundi mawili kutegemeana na wanavyo tunza mayai/watoto wao wakati wa kuzaliana. Perege jamii ya Oreochromis aureus, O. mossambicus na O. niloticus hutaga kwenye viota lakini hutunza mayai/vifaranga vyao midomoni kwa ajili ya kuyalinda dhidi ya maadui.
2.Perege wa jamii ya T. rendalli na T. zilli hutaga na kutunza mayai/vifaranga vyao kwenye viota vinavyochimbwa na dume na jike kwa pamoja. Hulinda mayai/vifaranga vyao wakiwa kwenye viota na si kuwatunza kwenye midomo mdomoni panapotokea hatari.
3.Urahisi wa jinsi wanavyo zaliana ni moja ya sababu inayofanya perege afae kwa ajili ya kufugwa kirahisi. Lakini, tabia hii pia husababisha matatizo. Uwezekano wa kukuza vifaranga wengi ni mkubwa na husababisha kuwepo samaki wengi kwenye bwawa kuliko uwezo wa bwawa. Matokeo yake samaki hudumaa kutokana na uhaba wa chakula, hewa na hata sehemu za mapumziko. Katika hali hii, kuna uwezekano mkubwa kukuta samaki zaidi ya asilimia 75% wakiwa na ukubwa wa chini ya uzito wa gramu 100. Kwa maeneo ambayo samaki wadogo huliwa, hili linawezekana lisiwe tatizo, lakini kama lengo ni kuuza na kujipatia fedha, samaki wa ukubwa huu huuzika kwa taabu au kwa hasara. Katika kuzuia hali hiyo ya kudumaa samaki isitokee, yafuatayo huweza kufanyika:


NJIA ZA KUWEZA KUDHIBITI UWINGI WA PEREGE KUTOKEA KWENYE BWAWA
1.Uvunaji wa mara kwa mara wa vifaranga kwa kutumia wavu. Njia hii hufaa kwenye bwawa dogo, ina shuruba na haihitaji uzoefu ili vifaranga wasife kutokana na majeraha watakaopata wakati wa kuwavua.
2.
Kutenganisha jinsia baada ya vifaranga kuwa na ukubwa wa kuweza kutenganishwa (monosex culture
3.Kwa kawaida, madume hukua haraka kuliko majike. Hivyo, wengi hupendelea kufuga madume
4.Kazi ya kutenganisha huweza kufanywa na mfugaji yeyote baada ya kuonyeshwa tofauti iliyopo kati ya jinsia moja na nyinge. Mkulima anashauriwa amuone mtaalam wa uvuvi aliye karibu naye kwa maelekezo.
5.Katika mchakato wa kuwatenganisha, makosa huweza kufanyika na kusababisha baadhi ya jinsia tofauti kutotenganishwa, mkulima asikate tamaa kwani idadi itakayokuwa imetenganishwa bado itatoa tija nzuri.
6.Kupandikiza vifaranga machotara (stocking hybrid "all-male" fingerlings: Madume hukua haraka kuliko majike
7.Utahitaji samaki wazazi waliohakikiwa ubora wake (requires pure strains of broodstock.
8.Utahitaji sehemu maalum ya kuzalishia na mtaalam aliyefuzu.
9.Ili kukidhi mahitaji ya vifaranga wa perege kwa wafugaji, kuna umuhimu wa wafugaji binafsi kuanzisha “hatcheries” kwa ajili ya kuzalisha vifaranga bora na kuwauzia wengine wenye kuhitaji. Japo kuwa kwa sasa baadhi ya wafugaji huzalisha vifaranga na kuwauzia au kuwagawia wenzi wao, wafugaji hazalisha vifaranga hao kama sehemu ya uzalishaji wa samaki wa kawaida kwenye bwawa. Kwa kadiri shughuli hii inavyokuwa, wafugaji wengi hupendelea kupata vifaranga bora. Na kwa jinsi hii, “hatchery” itakayokuwa ikizalisha vifaranga bora itapata soko zuri la vifaranga wake.
UZALISHAJI WA VIFARANGA


Uchaguzi wa mbegu bora (wazazi)
Samaki aina ya perege huzaliana wakati wote wa mwaka. Wana tabia ya kuzaa vifaranga wengi. Samaki
wazazi huweza kufugwa kwenye mabwawa au matanki wakiwa wanasubiri kuzaliana. Idadi ya mayai
yatakayotagwa na perege jike hutegemea ukubwa wa kimaumbile wa samaki jike. Kwa kawaida majike
wadogo hutaga mayai machache wakati wale wakubwa hutaga mayai mengi. Hii hutokana na uwezo wa
tumbo kuweza kubeba idadi ya mayai.

Inawezekana kutofautisha perege dume na jike kwa urahisi wanapokuwa na uzito wa gramu 15. Perege
jike ana tundu moja katikati ya mapezi matatu yaliyo karibu na mwisho wa mkia eneo la tumboni. Kwa
upande wa dume eneo hilo hilo kuna mrija uliojitokeza kwa nje.

UZALIANAJI WA PEREGE

Kama ilivyokwisha elezwa hapo juu, perege ni moja ya aina ya samaki ambao huweza kuzaliana kwenye
maji yaliyozingirwa (captivity) kama vile bwawa la kuchimbwa na hata tenki.

Ili mfugaji atape mbegu bora, ni vema akaanda mazingira mazuri yatakayopelekea kupatikana kwa
mbegu (vifaranga) bora. Hatua zifuatazo ni muhimu:

1.Chagua samaki wazazi na kuwaweka kwenye bwawa au tenki uliloliandaa kwa kuzalishia vifaranga. Uwiano unaopendekezwa ni wa samaki majike 2 kwa dume 1. Huyo dume mmoja ana uwezo wa kurutubisha mayai ya majike hayo2. Ukiweka madume wengi, watakuwa wakigombana wao kwa wao badala ya kuzaliana. Chagua samaki wenye ukubwa na umbo linalofaa na linalopendeza.
2.Mara tu baada ya vifaranga kuanguliwa huweza kuogelea wakiwa wamejichukulia kiini cha yai (yolk sack) ambacho hutumika kama chakula kwa muda wa siku 2 –3. Baada ya hapo, vifaranga uanza kujilisha vimelea (planktons) vitakavyokuwa vikipatikana ndani ya maji. Baada ya muda, vifaranga hao watakuwa na uwezo wa kuendelea kula vimelea hivyo, vijidudu na hata chakula cha ziada kama pumba za mahindi, za mpunga kama watapewa kama chakula cha ziada. Waachwe wakue kwa muda wa wiki tatu au zaidi kabla ya kuwahamisha kwenda kwenye bwawa la kukuzia. Kwa kuwa vifaranga hawa watakuwa na umri mmoja (ni wa rika moja), ukubwa sawa na ni wachanga, watakuwa na uwezo mkubwa wa kukua kwa ubora zaidi.

UHIFADHI WA MBEGU KWA AJILI YA MZUNGOKO MWINGINE WA UPANDAJI SAMAKI BWAWANI NA MATATIZO KATIKA UFUGAJI SAMAKI..

Unapovuna samaki, hakikisha kuwa vifaranga au samaki wazazi utakaokuwa umewachagua wanawekwa katika kijibwawa kingine (kinachojulikana kama nursery pond) kabla ya kuwarudisha bwawa la kukuzia (production pond). Ni muhimu kufanyia bwawa matengenezo na kulijaza maji kabla ya kuweka samaki tena. Hili ni muhimu kwa mfugaji kwani kinamhakikishia mfugaji kujua kuwa anapanda mbegu changa na ambao hawajadumaa. Pia humhakikishia kujua kuwa samaki waliopandwa wanalingana na ujazo wa bwawa, yaani vifaranga viwili kwa kila mita moja ya mraba na pia hurahisisha maji ya bwawa kurutubika kirahisi.

MATATIZO YA UFUGAJI SAMAKI
Ingawa ufugaji wa samaki si kazi ngumu sana, kuna matatizo mbali mbali ambayo mfugaji anaweza
kukumbana nayo. Lakini, matatizo mengi yanaweza kuepukika kama mfugaji ataweza kufuata kikamilifu
maelekezo ya ujengaji na utunzaji wa bwawa.
1.Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Iwapo utakumbana na tatizo hili, muone afisa uvuvi aliye karibu nawe upate ushauri.
2.Tatizo la maadui wa samaki kama vile ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Kwa kiasi kikubwa tatizo hili huambatana na ujengaji bwawa mbali na nyumbani na bwawa kuwa na nyasi nyingi (halifyekewi). Suluhisho ni kufweka nyasi kila mara, kujenga uzio kwa kutumia matete na hata nyaya za seny’enge, kuwinda ndege na kuharibu mazalia/maskani yao, bwawa kuwa karibu na maskani ya watu.
3.Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa. Tatizo hili hutokana na kutokukaushwa bwawa kwa kipindi kirefu. Utatuzi huweza kuwa; kukausha bwawa kila baada ya miezi 6 hadi 9
4.Ugumu wa kukausha maji bwawani. Husababishwa na bwawa kujenjwa kwenye eneo la tambarare kiasi kuwa hakuna uwezekano wa kutumia bomba au kukata kuta za bwawa kuondoa maji. Utatuzi; chimba bwawa kwenye eneo lenye mteremko wa wastani
5.Bwawa lisilo kaushika huwa mazalia ya Mbu wakati linapokuwa halina samaki ndani yake na kusaidia kuenea kwa malaria. Konokono wenye mabuu ya kichocho huzaliana kwenye mabwawa yenye kina kifupi au yenye majani mengi. Ni vema kuwa na bwawa yenye kina cha kutosha, lisilo na nyasi au majani ndani yake na linaloweza kukaushika kirahisi ili kuondokana na matatizo haya.
Matunzo, uvunaji wa samaki na zana ziazotumika kuvulia samaki

MATUNZO YA SAMAKI BWAWANI.

Ili bwawa liweze kutoa samaki wazuri muda wote yafaa bwawa la samaki lihudumiwe kwa kufuata
maelekezo yafuatayo;
1.Angalia samaki wanavyoogelea na kula wakati unapowalisha. Kama hawana matatizo, watajitokeza juu kwa wingi na kula vizuri kwa furaha.
2.Ondoa magugu na mimea katika bwawa.
3.Fyeka majani kando kando ya bwawa.
4.Angalia kila siku kiasi cha maji kama yananywea au hayanywei, yanatosha au hayatoshi.
5.
Angalia rangi ya maji ili ujue kama unahitaji kuongeza mbolea.
6.Chunguza kama kuna ndege na wanyama waharibifu na ukiwabaini, wadhibiti mapema.


UVUNAJI WA SAMAKI.

Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea wanavyokula, wingi wao bwawani na joto la maji. Samaki wanakuwa haraka kwenye maji ya joto kuliko kwenye maji ya baridi. Pia mfugaji mwenye bidii ya kulisha na kutunza bwawa, samaki wake watakua haraka. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 9.
Ni ukweli usiopingika kuwa; kwa kadiri juhudi na maarifa yanavyoongezwa katika bwawa, ndivyo kiasi cha samaki kitakachovunwa kitakavyoongezeka.

ZANA ZITUMIKAZO KATIKA UVUNAJI SAMAKI

Kwa kawaida, kuna makusudi mawili ya kuvuna samaki waliofugwa bwawani:
1.Kwa ajili ya kitoweo au kiasi kidogo kwa ajili ya kuuza.
2.Uvunaji wa samaki wote ili kuhitimisha msimu mmoja wa ufugaji samaki.
Kwa samaki wachache wa mboga au kuuza, unaweza kutumia kipande cha nyavu, mitego ya asili (migono), ndoano na hata kipande cha nguo. Kwa uvunaji wa samaki wote ili kuhitimisha msimu wa ufugaji, njia nzuri ni kuondoa maji yote kutoka katika bwawa na kukamata samaki wote mara moja. Unaweza kuondoa maji kwa namna mbili:
•Kukata ukuta ulio upande wa kina kirefu, weka chujio ili kuzuia samaki kutoka halafu ruhusu maji kutoka.
•Kutumia bomba la kuondolea maji kwa kufunikwa na kipande cha nyavu au kitu cho chote kisichoruhusu samaki kutoka bwawani isipokuwa maji.
Njia hii ni muhimu kwani isipofanyika kwa kipindi kirefu, samaki watakuwa wengi mno bwawani na kusababisha wengi kudumaa na kuwa na umbo dogo.
Samaki wanaofugwa bwawani huweza kuliwa wabichi baada ya kupikwa, kuchomwa, kukaangwa au kuuzwa kwa wanaohitaji.
Mfugaji pia anaweza kuuza samaki wachanga (vifaranga) kwa watu wenye kuhitaji mbegu za kupanda.
Baadhi ya samaki wakubwa wanaweza kukaushwa kwa moto, moshi, jua au kutiwa chumvi ili wasiharibike au kuoza upesi. Hii ni katika kuwahifadhi.

URUTUBISHAJI WA BWAWA LA SAMAKI KWA MBOLEA NA (MAJIVU) PAMOJA NA USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI.

1.Kutegemea aina ya udongo, majivu ya moto huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuingiza maji ili kupunguza Tindikali ya udongo na kuua baadhi ya wadudu walio maadui wa samaki waliopo katika eneo la bwawa.
2.Mbolea huweza kutawanywa bwawani kabla ya kuweka maji ili kusaidia kujenga mazingira ya maji kutuama (yaani Kushikamanisha udongo).
3.Vinginevyo, mbolea huwekwa eneo maalum (Uzio) mara baada ya maji kuingizwa bwawani ili kulirutubisha na Kuliwezesha liwe na vijimea na vijidudu vidogo vidogo vitakavyokuwa chakula cha awali cha samaki.
4.Dalili za kuwepo kwa vijimelea hivyo bwawani ni kugeuka rangi ya maji na kuwa ya kijani.
5.Aina ya mbolea hutegemea upatikanaji wake. Samadi ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na hata Majani mabichi yaozayo kirahisi na yasiyo sumu kwa wanyama na binadamu huweza kutumika.
6.Kiasi cha kuweka mbolea hutegemea sana ukubwa wa bwawa, aina ya samadi na idadi ya samaki waliomo.
7.Kipimo kizuri cha kiasi kinachotosha ni kuingiza mkono ndani ya maji hadi kufikia kwenye kiwiko, na usipoona Kiganja chako, basi simamisha uwekaji wa mbolea kwani vijimelea na vijidudu waliomo wanatosha kulisha samaki Waliomo kwenye bwawa kwa muda wa siku kadhaa.
8.Ukizidisha mbolea ni hatari kwa samaki, kwani wanaweza kufa kwa kukosa hewa ya oksijeni, hasa nyakati za usiku.



USAFIRISHAJI, UPANDAJI NA ULISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI

USAFIRISHAJI WA VIFARANGA WA SAMAKI
Upatapo vifaranga, visafirishe wakati wa asubuhi kwa kutumia ndoo ya plastiki, chungu, maplastiki makubwa.

Weka kiasi cha vifaranga 200 katika ndoo moja. Ni vema mkulima kuwa na tabia ya kupunguza maji
kwenye ndoo yenye samaki na kuweka mengine afikapo eneo lenye maji.

Ufikapo bwawani
, inamisha ndoo ili maji ya kwenye ndoo yaingiliane na yale ya bwawani.
Hii ni kuruhusu joto la maji na mazingira ya maji yaingiliane na kuwa sawa.

Waruhusu samaki watoke bwawani wenyewe bila ya kuwamwaga. Itachukuwa muda kabla ya vifaranga wote kuingia bwawani. Kwa kufanya hivyo, samaki hawatapata mshituko ambao wanaweza kupata kama
watamwagwa. Mshituko wa ghafla huweza kusababisha vifo.


UPANDAJI WA VIFARANGA VYA SAMAKI.
Ubora wa samaki utakao wafuga utategemea sana ubora wa vifaranga utakaokuwa umepanda bwawani.

Chanzo chako cha vifaranga ni bora kiwe na vifaranga wenye umri mdogo na ambao hawajadumaa.

Kwa samaki aina ya Perege, panda vifaranga viwili (2) hadi watatu (3) kwa kila mita moja ya mraba.

Kwa sasa, samaki aina ya Perege ndio wanaoshauriwa kufugwa na wafugaji wa maji baridi hapa nchini.

Kambale huweza kufugwa na mkulima mzoefu kwani huduma yake huitaji mtaji mkubwa katika
kuwalisha na Utaalam katika kuzalisha vifaranga vyake.


ULISHAJI WA SAMAKI.

1.Samaki, Kama walivyo wanyama wengine, wanahitaji kula.
2.Chakula cha samaki huweza kugawanywa katika makundi mawili:-
3.Cha asili kipatikanacho ndani ya bwawa kama vile vijimea, vijidudu na samaki wadogo.
4.Cha ziada ambacho huongezwa bwawani na mkulima.
5.Ili chakula cha asili kipatikane bwawani, ni vema bwawa liwe limerutubishwa vizuri, kwani vijimea vinavyotarajiwa humea palipo na rutuba.
6.Chakula za ziada huwekwa bwawani na mkulima mwenyewe. Aina ya chakula cha ziada hutegemea upatikanaji wake, gharama na aina na ukubwa wa samaki. Baadhi ya chakula cha ziada ni kama: pumba za mahindi, za mpunga, mashudu ya pamba na karanga, machicha ya pombe, ugali na masazo ya jikoni, baadhi ya majani pori, majani yatokayo bustanini.
7.Inashauriwa mfugaji alishe kila siku, kwa muda ule ule, saa ile ile na sehemu ile ile. Tabia hii hujenga mazoea ya samaki kula zaidi na kupunguza wingi wa chakula kinachopotea.
8.Usilishe chakula kingi zaidi ya mahitaji ya samaki kwa siku hiyo. Mfano, usiweke debe zima la pumba kwa mara moja na kuacha kulisha kwa wiki nzima! Sehemu ya chakula kitakachosalia, kitaoza na baadhi ya siku samaki hawatakuwa na chakula, watashinda na kulala njaa!




PART II

UFUGAJI WA SAMAKI: MABWAWA YA KUFUGIA SAMAKI


Hili ni bwawa la kuchimbwa chini, lipo katika kituo cha ufugaji wa samaki cha serikali kilchopo Kingolwira mjini Morogoro. Yapo na mabwa mengine mengi kama yanavyoonekana pembeni mwa bwawa hili.


Hii ni aina nyingine ya bwawa lililochimbwa na kujengwa kwa simenti na kulifanya liwe imara zaidi. Nalo lipo katika kituo cha ufugaji wa samaki Kingolwira mjini Morogoro.

Bwawa hili limejengwa pia kwa simenti kutoka usawa wa ardhi kwenda juu, ni la mduara kama linavyoonekana kwenye picha hii. Yapo mabwawa mengi ya aina hii katka kituo cha kufugia samaki Kingolwira mjini Morogoro.

Ufugaji wa samaki unamanufaa sana kwa mfugaji kwani unaweza kumuondolea Mtanzania umaskini huku akiendelea kujipatia kitoweo. Soma zaidi HAPA kuhusu jinsi ya kuanza kufuga samaki na ufugaji wenyewe.

VIDEO ZINAZOHUSU SAMAKI TANZANIA
Video hii inaonyesha baadhi ya wanachi wa mkoa wa Kagera walioamua kunzisha miradi ya ufugaji wa samaki. Wameamua kufuga samaki baada ya kuona upatikanaji wa samaki Toka ziwa Victoria umekuwa mgumu sana na uhitaji wa samaki ni mkubwa sana. Waliamua kuanza kidokidogo na hatimaye miradi yao kuendelea kukua kadri siku zinavyoendelea.
Kuna uhaba mkubwa sana wa samaki Tanzania, ukipita katika masoko ya samaki hasa asubuhi utaona wafanyabiashara wanavyogombania samaki. Hii inaonyesha msisitizo kuwa uhitaji wa samaki Tanzania ni mkubwa na watu wengi wanahitajika kuingia katika ufugaji wa samaki. Itawasaidia kujikwamua kimaisha lakini pia kuwafanya Watanzania wengi wapate kitoweo cha samaki. Tazama video hii hapa chini inayoonyesha uhaba wa samaki Tanzania hadi kulazimika kuagiza nje ya nje ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani.




PART 3

UFUGAJI WA SAMAKI KWENYE BWAWA

“NINA SHAMBA MAENEO YA BUNJU DAR ES SALAAM. NINGEPENDA KUFUGA SAMAKI KIBIASHARA. MAJI YA UHAKIKA NI YA KISIMA NA YANA CHUMVI KIASI. NAPENDA KUPATA MAELEZO ZAIDI YATAKAYONIWEZESHA KUANZA UFUGAJI HUU.”

Wakulima wanaweza kuongeza kipato kutokana na ufugaji wa samaki katika maeneo yao
UFUGAJI WA SAMAKI KAMA ILIVYO SHUGHULI NYINGINE YOYOTE YA KIUCHUMI INAHITAJI USIMAMIZI MZURI ILI UWEZE KUWA NA FAIDA. MBALI NA HILO, MFUGAJI WA SAMAKI ANATAKIWA KUZINGATIA VIGEZO VINGI KABLA YA KUANZA UFUGAJI. MOJA YA VIGEZO HIVYO NI SOKO. SI JAMBO LA BUSARA KUANZA SHUGHULI YOYOTE KABLA HAUJAFANYA UCHUNGUZI NA KUJUA KAMA KUNA MAHITAJI YA BIDHAA UNAYOKUSUDIA KUZALISHA. WAFUGAJI WENGI WAMEANZISHA UFUGAJI WA SAMAKI LAKINI WAKAISHIA KUPATA HASARA KUTOKANA NA UKOSEFU WA SOKO. NA WENGINE WAMEANGUKA KUTOKANA NA UTUNZAJI MBOVU WA MABWAWA YA SAMAKI.

MAJI
UPATIKANAJI WA MAJI NA UBORA WAKE NI KIGEZO MUHIMU KATIKA UFUGAJI WA SAMAKI. MTIRIRIKO WA MAJI NI NJIA RAHISI KWA MFUGAJI. MAJI MACHAFU HAYATAKIWI KWA UFUGAJI WA SAMAKI. WAFUGAJI NI LAZIMA WASAIDIWE NA MAAFISA KILIMO KATIKA ENEO LAO KAMA MAJI YANAYOPATIKA YANA UBORA KWA AJILI YA UFUGAJI WA SAMAKI. KWA WAKAZI WA DAR ES
SALAAM, INAWEZEKANA PIA KUFUGA SAMAKI KWENYE BWAWA, ENDAPO MAJI YANA CHUMVI YA WASTANI, NA KWA KIWANGO KINACHOSHAURIWA KITAALAMU, BASI SAMAKI WANAWEZA KUSTAHIMILI, NA KUKUA VIZURI.

BWAWA

BWAWA LA SAMAKI LINAHITAJI NAFASI KUBWA YA ARDHI, YENYE MWINUKO PAMOJA NA ENEO LA SAMAKI KUKIMBILIA. HII NI NJIA RAHISI YA UFUGAJI ENDAPO ARDHI NA MAJI HAVINA GHARAMA KUBWA. ENEO KUBWA ZAIDI LINARUHUSU UZALISHAJI USIOHITAJI NGUVU YA ZIADA NA WENYE TIJA.

UTENGENEZAJI WA BWAWA LA SAMAKI KWA MAENEO YENYE UDONGO WA KICHANGA KAMA DAR ES SALAAM, MFUGAJI ATALAZIMIKA KUCHIMBA NA KUWEKA KARATASI YA NAILONI. HII, ITASAIDIA KUZUIA UPOTEVU WA MAJI PAMOJA NA KUZUIA BWAWA KUPOROMOKA.

NI VYEMA UPANDE MMOJA WA BWAWA UKAWA NA KINA KIREFU KULIKO MWINGINE. UPANDE MMOJA UNAWEZA KUWA NA KINA CHA MITA MOJA NA NUSU, NA MWINGINE MITA MOJA. HII ITAMSAIDIA MFUGAJI KUWEZA KULIHUDUMIA BWAWA VIZURI, HATA KAMA NI KUINGIA NA KUFANYA USAFI.

UTUNZAJI WA BWAWA

INASHAURIWA KUFANYIA BWAWA USAFI MARA KWA MARA, HASA KWA KUONDOA MAJANI ILI KUEPUSHA WADUDU KUFANYA MAKAZI NA HATIMAYE WAKAWADHURU SAMAKI. PIA UKIACHA MIMEA BWAWANI ITATUMIA VIRUTUBISHO KWA KIASI KIKUBWA NA KUONDOA HEWA YA OXIJENI.
HIVYO, KILA UNAPOONA UCHAFU, SAFISHA MARA MOJA.

ULISHAJI

WAFUGAJI WALIO WENGI, WAMEKUWA HAWAZINGATII KANUNI ZA ULISHAJI WA SAMAKI. KWA KAWAIDA INATAKIWA KUWALISHA SAMAKI MARA MBILI HADI MARA TATU KWA SIKU.

AINA YA CHAKULA

SAMAKI WANAWEZA KULISHWA KWA KUTUMIA PUMBA YA MAHINDI, MASHUDU YA PAMBA NA ALIZETI, SOYA, MABAKI YA DAGAA. HAISHAURIWI KULISHA CHAKULA KILICHOKO KWENYE MFUMO WA VUMBI, BALI KIWE MABONGE MADOGO MADOGO, KWA WASTANI WA TAMBI.

MAGONJWA

KWA KAWAIDA SAMAKI HAWANA MAGONJWA MENGI SANA YANAYOWASHAMBULIA, ILA KUNA BAADHI YA YALIYOZOELEKA KAMA VILE MAGONJWA YA UKUNGU (FANGASI), MAGONJWA YATOKANAYO NA VIRUSI, PAMOJA NA MINYOO.

SAMAKI WANAPOSHAMBULIWA NA FANGASI, HUONEKANA KWA MACHO KWA KUWA HUWA NA MADOA MADOA. SAMAKI AINA YA KAMBALE HUSHAMBULIWA ZAIDI KULIKO PEREGE.

PIA UNAWEZA KUTAMBUA KUWA SAMAKI NI MGONJWA KWA KUWA HUZUBAA SEHEMU MOJA KWA MUDA MREFU. MAGONJWA KWA SAMAKI PIA YANAWEZA KUTOKANA NA MRUNDIKANO KWENYE BWAWA. HIVYO, NI MUHIMU KUWAPUNGUZA KILA WANAPOONGEZEKA.

TIBA

TIBA ILIYOZOELEKA KWA SAMAKI NI KWA KUWEKA CHUMVI KWENYE MAJI, KASHA KUWATUMBUKIZA SAMAKI UNAOWAONA KUWA NI WAGONJWA, KISHA KUWATOA NA
KUWARUDISHA BWAWANI.

UPATIKANAJI


UNAWEZA KUPATA VIFARANGA WA SAMAKI KUTOKA KATIKA KITUO CHA KUZALISHA NA KUFUGA SAMAKI KINGOLWIRA MOROGORO. BEI YA KIFARANGA CHA PEREGE NI SHILINGI 50, NA KAMBALE NI SHILINGI 150

Umejitaid kutoa maelezo ila ayajajitosheleza.
 
suala kwamba chakula kisichokuwa ktk pellets format kinaisha au kuoza sio issue kwani unashauriwa kuweka mara tatu kwa siku cha kuwatosha muda huo tu na pia unachagua eneo maalum la kusimama na kuwamwagia.

Kwa maelezo yako kilo kumi kwa siku utazigawa mara tatu na kuwamwagia wanakula chote.
 
Habari.

Kupitia jukwaa hili tumekua tukijifunza vitu tofouti juu ya namna ya kujiendeleza kiuchumi ili kujikwamua kutoka katika hali tulizonazo. shukrani kwa wale walionitafuta na wakapata ushauri, nadhani bado tupo pamoja na mtafanikiwa.

Bado nasisitiza uchaguaji wa eneo na uchimbaji wa bwawa unahitajika umakini kwani ndipo ambapo utakua unafanya mladi hivo ikiwa kama initial stage ,inabidi umakini,hivo ujumuisha, uwepo wa maji safi kwa kiasi kikubwa, na uwezekeno wa kupata chakula cha samaki wako.

Mahitaji ni makubwa kulinganisha na wataalamu tuliopo, ivo tuendelee kuwasiliana kwa ajili ya kupeana ujuzi na ushauri, fuga samaki mana ni biashara inayolipa sana. kwa maelezo zaid wasiliana nami 0717451771.
 
Kumekua na shida jinsi ya kuchimba mambwa ya samaki na ufugaji wake kwa ujumla,,hivyo kama unaitaji hiyo project wasiliana nami,0717451771
 
Samaki mpaka anavunwa, sema miezi 3; gharama zake ni kiasi gani na wanakuwa na uzito kiasi gani?
habari.kupitia jukwaa hili tumekua tukijifunza vitu tofout juu ya namna ya kujiendeleza kiuchumi ili kujikwamua kutoka katika hali tulizonazo. shukrani kwa wale walionitafuta na wakapata ushauri, nadhani bado tupo pamoja na mtafanikiwa..bado nasisitiz uchaguaji wa eneo na uchimbaji wa bwawa unahitajika umakini kwani ndipo ambapo utakua unafanya mladi hivo ikiwa kama initial stage ,inabidi umakini,hivo ujumuisha,,uwepo wa maji safi na kiasi kikubwa,na uwezekeno wa kupata chakula cha samaki wako,..mahitaji ni makubwa kulinganisha na wataalamu tuliopo,ivo tuendelee kuwasiliana kwa ajili ya kupeana ujuzi na ushauri,fuga samaki mana ni biashara inayolipa sana.kwa maelezo zaid wasiliana nami 0717451771,
 
Nitakutafuta kwa maelezo ya ziada ila bajeti ya project hiyo ni sh ngapi?
 
Pia kwa wafugaji wa samaki waliopo DSM mkihitaji chakula cha samaki, kinapatikana maeneo ya karibu na mlimani city. Ukihitaji naweza kukuelekeza kwa kiwango unachohitaji.
 
Kumekua na uhangaiko wa wataalamu wa maswala ya ufugaj wa samaki...na kilimo cha majini kwa ujumla..hivo kama una mradi wako au unamfahamu mtu mwenye mradi au anaehitaji kuanzisha mradi basi anitafute...tunaweza kusaidiana kwa gharama nafuu tuu.071745771 .
 
mimi ni mfugaji samaki ili akue anaitaji maji safi na chakula bora nakalibisha maswali
 
Unahitaji bwawa la ukubwa gani kwa ajili ya samaki ili upate faida nzuri na lichukue angalau samaki wangapi?

Linaweza gharimu kiasi gani kulitengeneza? Na linatengenezwaje hilo bwawa la samaki.

Linaweza chukua samaki wangapi?

Hadi samaki kukomaa wanahitaji muda gani?

Malisho ya samaki unayapata wapi? Na yanagharimu kiasi gani?

Kuna madawa utahitaji wakati wa kuwatunza samaki? Kuna magonjwa ya samaki?

Maji gani unatakiwa utumie kwa samaki? Ya bomba au kisima yanafaaa?

Unatakiwa uwe unabadilisha maji? Kama unatakiwa kila baada ya muda gani?
 
Back
Top Bottom