Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ndugu kwa idadi iyo inabd upate tang lenye kama eneo la mita za mraba 170 hivi..
 
Mwenye utalaamu wa ufugaji wa Samaki anifahamishe.. Ni zao ninalolifikiria sana kulianza muda si mrefu.
 
Habari za leo wadau?

Mimi kuhusu ufugaji samaki nimehamasika ila napenda niwafahamu ma kuwatembelea wafugaji samaki waliofanikiwa. Hapa nina maanisha walioweza kuuza samaki wakiwa na miezi sita kwa uzito mzuri.

Hii imetokana na kwamba ktk hii biashara tunaenda kinadharia mno. Uzalishaji unaoongelewa siyo ambao unapatikana kihalisia labda mimi huwa nakutana na waliofeli tu.

Maana huwa wanakalamika samaki wanadumaa. Wadau niunganisheni na waliofanikiwa.
 
Habar wadau jaman mm.nahitaj mambo ya msing na ya kuzngatia katka ufugaj wa nguruwe kibiashar zaid
 
Tuendelee kujuzana kwani nami nipo kwenye kuchimba bwawa la samaki lenye ukubwa 70mx70m ni ekari 5 nataka nichimbe lote mabwawa ila itakuwa kwa awamu.

Watu ninaowajua wanapiga hela ya maana huku.
 
Tuendelee kujuzana kwani nami nipo kwenye kuchimba bwawa la samaki lenye ukubwa 70mx70m ni ekari 5 nataka nichimbe lote mabwawa ila itakuwa kwa awamu.

Watu ninaowajua wanapiga hela ya maana huku.

Upo wapi mkuu?...Sorry sijaelewa hapo kwenye uchimbaji...Unataka kuchimba lenye ukubwa wa 70m×70m au nime elewa vibaya mkuu?
 
Upo wapi mkuu?...Sorry sijaelewa hapo kwenye uchimbaji...Unataka kuchimba lenye ukubwa wa 70m×70m au nime elewa vibaya mkuu?
ntera tunakusubili huku uzi hauendi kabisa, tujuze huko kwa waliofanikiwa
 
Ufugaji samaki ni tasnia inayokua kwa kasi duniani hata hapa nchini ni kweli inakua. Hali halisi ya kijiografia hapa nchini ni chachu ya maendeleo ya ufugaji samaki.

Kwa wakulima waliokwishaanza naombeni majibu yenu kwa maswali yangu haya.

1. Je! kuna yeyote ambaye amevuna samaki aina ya sato wenye nusu au kilo moja ndani ya miezi kuanzia sita, tisa na mwaka mmoja ?

2. kuna yeyote ambaye amefuga madume tu? (sato) na vipi ukuaji wake upoje ?

3. Kwa mtazamo wako we unaonaje kati ya kufuga samaki mchanganyiko jinsia zote au jinsia moja, upi kwako umeona ni bora.

4. Changamoto ya chakula unaionaje ?

ANGALIZO: Usitumie majibu ya kugoogle au kufundishwa darasani. Majibu yalenge hali halisi ya kijiografia Tanzania
 
Jamani maswali yaufugaji iwe nyuki samaki ama sungura jitahidini kuuliza mchana, usiku ni muda wa kutafuta watoto na kujitafutia heshima ya ndoa!
 
Mimi swali langu ni soko
likoje?
wanunuzi wanapatikana wapi?
wanakufuata kwenye mabwawa au unawapelekea?
bei ikoje?
 
Mimi swali langu ni soko
likoje?
wanunuzi wanapatikana wapi?
wanakufuata kwenye mabwawa au unawapelekea?
bei ikoje?
wanunuzi kuna ambao wanakufata hadi kwenye mabwawa wakanunua kwa jumla na ukiamua wewe mwenyewe unaweza fungua duka la samaki ukauza reja reja. bei kwa kilo ni kuanzia elfu saba
 
Bandugu,

Hakika Elimu Bahari. Kwa muda mrefu nimekuwa na hamu ya kufahamu mengi juu ya UFUGAJI WA SAMAKAI kibiashara na kwa ajili ya kitoweo (maana kwa kweli nakipenda sana kitoweo hiki).

Leo nimepata mwanga baada ya kuutembelea uzi huu. tafadhali Bw Ha Muji naomba contacts zako tuwasiliane zaidi.

TCHAO!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…