Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki


= Aquaponic
 
Dah.. iko poa sana nina pesa kidogo naisi nitaiweka huko
 
Ningeomab kuzua ziada zifuatazo.

a)ukitaka kufuga Samaki kwenye Shamba lako Mwenye lazima uombe Kibali ?
Maana TFDA na TBS wengine hata mipaka ya maeneo yako yakazi hatuyajui.

b)Je kwenye kuuza Samaki je Kodi unalipa?TRA,maana tunasikia kwenye un processed bidhaa hakuna kodi
 
La Zida ni kwamba.
Nimeona wafugaji wengi wa Ng`ombe wanafanikiwa saana wakiwa karibu na Madktari wa Mifugo hiyo na changamoto kuwa ndogo kwao.Hasa pale wanapokuwa katika hatua za Mwanzo.Kipindi cha mpito kama miaka miwili hivi.Then muda unavyokwenda Mfugaji anakuwa anaongeza uwezo na kupunguza kumuita Dokta kira mara.

Sasa hembi nijuzeni kwenye ufugaji wa Samaki.
Ningependa kujua wapi Unaweza kupata Dokta/mtaalam wa Upande wa Ufugaji wa Samaki,na je mfano kama je inawezekana kuingianae mkataba wa kumlipa kwa mwezi Mshahara na allowance ya mafuta ili kila wiki kwa uchache awe anakuja site.
Kwa wazoefu inawezaku cost kiasi gani?

Maana mie kwa muono wangu,naona hii ndio move nzuri kwangu kuanza nayo.Ili nikianza nianze kwa mfumo wa kuwa karibu sana na Mtaalam.

Wadau naomba mchanganuo hapo na njia nyepesi,Manual readings ninazo nyingi ila kuwa na trainer on site ni bora zaidi pia
 
kwa wale wanao hitaji huduma ya
kuchimbiwa mabwawa
kujengewa ya sement
kuwekewa yale movable
mantank
huduma zetu ni nafuu sana pia kutafutiwa wanunuzi wa samaki tuwasliane pm(kwa wa kazi wa dar) nitatoa no.
 

Bonge la elimu mkuu, sijawahi kufikilia kufuga samaki lakini naona sasa napata ushawishi.
 
Bonge la elimu mkuu, sijawahi kufikilia kufuga samaki lakini naona sasa napata ushawishi.

Usiende mbio, anza na elimu ya ufugaji kwa kuipata kwa watalaam wa serikali walio ktk vituo vya serikali ili usifanye makosa.
 
Humu ndani pana majibu ya kila swali linalosumbua akili yangu, asante sana wana JF kwa kutoa bila choyo
 
Usiende mbio, anza na elimu ya ufugaji kwa kuipata kwa watalaam wa serikali walio ktk vituo vya serikali ili usifanye makosa.

Kaka Malila Mungu akuzidishie jamaangu, idea nilikuwa nayo muda na nilishafanya utafiti kwa kutembelea baadhi ya mabwawa hapa kwetu manispaa ya bukoba na nikahamasika sana, nakushukuru pia vitabu vyote ni vizuri na vina miongozo mizuri sana, kimsingi mm na rafikiangu mmoja ufugaji wa samaki ni moja kati ya miradi tunayokwenda kuifanya soon.

Pia asante kwa ushauri wa kwenda kumuona mtaalamu toka halmashauri na ikiwezekana twende nae site akatupe maujuzi ya ziada.

Kama hutojari waweza nicheck kupitia 0765829256.

Asante sana
 
Huyu malila kwakweli Mungu amzidishie mema maana jamaa ni mtaalam hlf anapenda kusaidia sana bila kinyongo
 
 
Habari ndugu,ninafuatilia kwa karibu sana kuhusu ufugaji hasa huu wa samaki,naomba kujua nitapata wapi mbegu au vifaranga wazuri wa sato,nipo kigamboni dar es salaam
 
Heshima mbele JF member, kwa upande wangu kuhusu ufugaji wa samaki nilipenda kutoa tu tahalifa juu ya chakula cha samaki, ni kwamba kwa mtu au company yeyote ambayo itahitaji cassava cripts au chips kwa ajili ya kutegenezea fish meel binders tunao mzigo wa kutosha hata hivyo tuna stock ya mapumba ya muhogo na chips zake, kama kutakuwa na mahitaji ya chakula aina hiyo nyooote mnakaribishwa
 
[Hello JF members yeyote atakayehitaji chakula cha samaki aina ya cassava chips au casssava cripts tunaomba aweze ku tu PM, tunazo aina zoote ya cassava chips na mapumba yake ambayo hutumika kwa ajili kutegeneza chakula cha kukuQUOTE=Malila;816346]Wana JF

Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vya maji ya asili ikiwemo mito, mabwawa, maziwa, bahari, chemchem nk. Kutokana na vyanzo hivi tunapata samaki wa aina mbalimbali wakiwemo perege/sato, kambale, kambamiti (prawns), vibua, changu, kaa n.k.

Samaki ni chanzo cha lishe, kipato na ajira, tunaweza tukatengeneza vito kutokana na lulu wa chaza. Nimejaribu kuzungukia katika soko letu la fery pale nikagundua akina mama na wadau wengi wanafaidika sana na biashara ya samaki nadhani tunawaona mitaani kwetu lakini wanalalamika bei imekuwa juu na upatikanaji wake ni wa shida sana kulingana na msimu.

Nilijaribu kufuatilia kwa undani suala hili kwa wizara husika nikaelezwa ni kweli bei ya samaki iko juu na upatikanaji wake ni mgumu kutokana na samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa na wanapungua kwa kasi ya ajabu...Hali hii inatokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uharibifu wa mazingira, nguvu kubwa ya uvuvi iliyopo kwa mfano samaki sangara kutoka ziwa victoria wamepungua sana na wanaopatikana kwa sasa ni wadogo. Pia wizara ililazimika kufunga uvuvi wa prawns kwa meli kubwa kubwa kutokana na hali kuwa mbaya. Hata perege wanaopatikana ni wadogo na kwa uchache.

Ili kuokoa suala hili, njia pekee ni kuhamasisha UFUGAJI WA SAMAKI kwa ajili ya kipato, ajira na chakula. Nimevutiwa na suala hili nikaona niwashirikishe wana JF. Nchi za asia china, ufilipino, japan, indonesia fani hii imekuwa sana na wananchi wanajikwamua kiuchumi kutokana na ufugaji wa samaki.

Bado ninafanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu suala hili la ufugaji samaki na jinsi tunavyoweza kufaidika nalo. Ninaamini tunaweza kufuga na kupata faida kubwa pia tukatunza mazingira yetu ya asili.

Wakati naendelea kufuatilia suala hili naomba mwenye taarifa basi tushirikiane hapa JF. Nitarudi tena kwa maada hii mara nitakapokusanya taarifa ndani ya siku chache.

Nawasilisha kwa michango yenu.

Nteko Vano Maputo

Penye nia pana njia

--------------------------




-----------------------------






*Nakala na vitabu juu ya Ufugaji wa Samaki DOWNLOAD Attachments[/QUOTE]
 
Hello ndugu zangu. Hili suala la kufuga samaki ni wazo zuri na likifanyika kwa umakini litaweza kutukwamua. Mimi nafuga kuku wa kienyeji hapa kwangu Mapinga Bagamoyo nahitaji pia kufuga samani. Nahitaji partner tuanze mradi aliyetayari, sehemu ipo ya kutosha ninayo namiliki mwenyewe. Pia mtu awe serious tuwasiliane maana foundation nimeiweka tayari tuanze kazi.
 
Sangas naomba mchanganuo wa kuchimba kisima tafadhali. Maana hii huduma naihitaji sana!
 
Natengeneza raised ponds kwa kutumia liners na ma banzi...hii njia n8 cheap na hauhitaji kuchimba chini ardhi yako. Karibu nikufanyie kazi nzuri....0768520042
 
abbadjr nipigie 0768520042 ni kutengenezee ponds za bei rahisi
 
Habari ndugu,ninafuatilia kwa karibu sana kuhusu ufugaji hasa huu wa samaki,naomba kujua nitapata wapi mbegu au vifaranga wazuri wa sato,nipo kigamboni dar es salaam

Hali yako, mimi nimfugaji wa samaki aina ya sato na kambale. Nina zalisha vifaranga wa sato na unaweza kututembelea ili upate kujionea mwenyewe tupo Cheka njia ya kwenda Kimbiji.

Kwa mawasiliano piga namba hii 0717314500 Abdul.
 
funzadume hongera kumbe umeenea sehemu zote;
naomba chapisho, nitumie kwa lyimo2@yahoocom
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…