Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Iwe hasara afu watu waendelee kufuga? Nenda ucheki calculations zako vzr
 
Lazima ununue chakula?unaweza kutengeneza mwenyewe kuna mashine zipo.
Tatizo siyo mashine mkuu, tatizo ni ingredients (malighafi za kutengeneza hicho chakula), upatikanaji wake na gharama zake.
 

Acha Bangi na Uongo
Kama hujatembelea wafugai uwe mpooole,sio kukaa unadanganywa na wahindi.

We muhindi gani akakupa siri ya biashara yake zaidi ya kukutisha,halafu nyie mnaokatisha watu tamaa kwa kuona watu waoote maboze humu au hatujui wafugaji.

Au ndio unataka tujue na wewe ulienda Israel,Sifa mbaya,kabla ya kupost ujue kwamba kinachoongelewa ni kitu gani.

Matajiri wangapi walianza na laki moja, na leo wangapi wanatusua maisha kwa mitaji midogo.

We Jiuliza, maeneo ya yard za magari Dar yalivyo na kila ukipita mwezi mzima unakuta karibia gari zote zipo au zimetoka mbili tu, wakati mtu ameinvest karibia Billion kwenye Yard, at the same time kuna mtu anamiliki Dalala 10 tu anaingiza pesa kuliko yeye.

Maisha usilazimishe unavyotaka wewe, utajiri unaanzia kwenye moja. Tembelea vijijini uone watu wanavyofuga kwenye mabwaya ya asili karibia ya mito au maeneo yenye chemchem uone wanavyopiga hela, wanamiliki majumba na magari kwa biashara hiyo
 
***Planktons(phytoplanktons-mimea midogo sana, zooplanktons-wadudu wadogowadogo), Hivyo Mkuu (microorganisms) sioni kama litakuwa neno sahihi hapo juu kwa maana halisi ya Micro-organisms.
Nilikisudia kuandika kwa urahisi na kueleweka kwa kila mtu.
 
Reactions: Luo
Ungemuuliza huyo mhindi kwao wanafugaje? Kama yeye mtaalam amekuja bongo kufanya nini?. Halafu na wewe ukiambiwa changanya na zako. Wabongo bwana yaani akisema mhindi sawa, akisema Bukoba boy no.

Turudi katika mada sasa- Hiyo teknolojia ya kuzungusha maji wanaganya kwasababu wana uhaba wa maji na ardhi kwahyo eneo dogo linatumika intensivelly. Ni gharama sana hiyo yeknolojia.

Tuishie hapo ila nikutaarifu tu Tanzania ina hazina kubwa ya wataalam wa samaki. Vile vile ina fursa nyingi. Hivyo huu mradi unalipa. Siku nyingine omba msaada wa kuelewa haya mambo.
 
Mkuu chakula cha samaki ni kipi? Na je wakati wa kuwavuna wanavunwaje bila kuwabakisha kwenye bwawa lako la kutengeneza?
Kwanza unatakiwa upate formula ya chakula chako. Lishe yake haina tofauti na kuku isipokuwa viwango vya protin, wanga, mafuta hutofautiana. Pia fomu maana chakula cha samaki kinaingia kwenye maji.

Hivyo lazima kiwe binded na unga wa mhogo au ngano na kitengenezwa kama pellet kwa samaki wakubwa. Vile vile kama ni sato ni vema kikawa cha kuelea. Tembelea Wizara husika kwa msaada.
 
Ni ule upumbavu wa kuamini kila kitu kinachosemwa ukitoa wanavosema watanzania.
 
***Planktons(phytoplanktons-mimea midogo sana, zooplanktons-wadudu wadogowadogo), Hivyo Mkuu (microorganisms) sioni kama litakuwa neno sahihi hapo juu kwa maana halisi ya Micro-organisms.
Neno sahihi ni phytoplankton yaani mimea ya katika maji na zooplankton yaani wadudu-wanyama katika maji kwa pamoja huitwa plankton
 
Kuchimba bwawa lenye ukubwa wa robo heka kwa kutumia mashine inaweza kugharibu kiasi gani cha pesa?
 
Kuchimba bwawa lenye ukubwa wa robo heka kwa kutumia mashine inaweza kugharibu kiasi gani cha pesa?
Robo heka ni bwawa lenye ukubwa wa sqm 2500. Mashine itachimba kwa siku 2-3 kulingana na eneo na uwezo wa operator. Kwa masaa 8 kukodi mashine ni laki 6-8. Operator kwa kawaida 100,000 kwa masaa 8. Mafuta ni kama lita 250-300.

Inawezekana ukamlipa hela ya ziada operator akufanyie kazi kwa zaidi ya masaa 8 ili umalize mapema. Pia kuna gharama ya usafiri wa kubeba mashine kama ni ile ya chain (1ml-2ml)
 
Kwahiyo kwa kukadilia unaona ni shilingi ngapi?
 

uNGEMUOMBA HUYO MUHINDI AKUFUNDISHE ILI NA WEWE UKAFUGE.
 

Kwahiyo gharama ya kubeba hiyo mashine ni juu ya mteja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…