Ufugaji wa Samaki: Pata ushauri, mawazo na michango kuhusu ufugaji samaki. Jifunze changamoto, utaalamu na masoko ya Samaki

Ok basi naweza kufanya mautundu Kutengeneza la simtank.. Nitakata hata mara bili.....!
Inawezekana pia, au waweza chimba kibwawa chako ukubwa unaotaka, badala ya kusakafia unatumia zile plastic liner ili kutoruhusu maji kunyonywa na udongo.

Hizi karatasi za plastic waweza zipata kwa urahisi zipo maduka mengi mjini
 
Nimesikia ufugaji wa Samaki kwa kutumia bwawa dogo la plastiki nyumbani ni mkombozi tosha wa Maisha. Nahitaji msaada wenu wadau. Je bwawa hilo la plastic liwe na vipimo gani? Hayo maplastic yanauzwa bei gani?

Ni kweli samaki wanafugika kwenye tank za plastic; ila plastic pekee halitoshi, maana hewa iliyomo kwenye maji inakwisha kadri samaki wanavyoinyonya kama sehemu ya upumuaji.

Pia maji ya kwenye tank yatachafuliwa taratibu kwa kinyesi cha hao samaki.
Utahitajika ama uwe unabadili maji mara kwa mara ili ipatikane hewa mpya kwenye maji hayo mapya ambayo pia yatakuwa hayana kinyesi cha samaki.

Kuna utaratibu wa aina mbili wa kutumia maji hayo hayo (na nyongeza kidogo nadhani---bado najifunza kwa kusoma tu). Utaratibu huu unatoa uchafu wa kinyesi na unarudisha hewa safi kwenye maji.

Ingia Youtube, halafu tafuta 1. RAS---Recirculating Aquaculture System na 2. Aquaponic System.
Ni mafunzo marefu na nadhani magumu kwa sisi ambao ndio kwanza tunawaza kuingia katika ufugaji wa samaki kwa njia ya ma-tank. Lakini hakuna wepesi pale unapotaka kujiletea maendeleo, lazima kupambana.
 
Mkuu mleta mada naomba kujua kwanini vifaranga vya kambare vinabei kubwa yaani 500?wakati sato ni 300?
 
Ati sehemu kama Mbeya Kwenye Baridi baridi waeza funga samaki aina ya Sato.!?
 
Ati sehemu kama Mbeya Kwenye Baridi baridi waeza funga samaki aina ya Sato.!?
NDIO UNAFUGA VIZURI TU, NIMEONA KWA MACHO YANGU KAMBALE PALE TUKUYU MWAKA JANA, WAKATI ZAMANI NILIAMINI KUWA KAMBALE NI WA MAJI JOTO.
 
natamani sana kufuga samaki,je maeneo ya rufiji yanafaa?na upatikanaji wa maji vibali naazaje?na mtaji wa wastani sh ngapi ili uweze uza kwa faida angalau?
 
  • gharama kwa ujumla kama mimi nataka kufuga kulimo cha biashara . gharama average(general) zinakuwaje?
  • na sehemu ninapoweza pata hao samaki wa kuanzia? nipo morogoro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…