Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,308
Njiwa hawa ndiyo nawaota kila siku.nitawapata wapi Kama hawa?:help:
Hawa njiwa mimi ninao kama unawataka itakubidi usubiri nizalishe ndio niuze maana hawapatikani hapa nimeagizia kutoka Dubai na wengine "crested helmet" wametoka Australia. Hawana bei kubwa kwa nje ila gharama ni kuwasafirisha vibali na kuwatoa.
Ninawataka na Niko tayari kusubiri uwazalishe.nitakupm kwa mawasiliano zaidi kaka yangu.ahsante sanaHawa njiwa mimi ninao kama unawataka itakubidi usubiri nizalishe ndio niuze maana hawapatikani hapa nimeagizia kutoka Dubai na wengine "crested helmet" wametoka Australia. Hawana bei kubwa kwa nje ila gharama ni kuwasafirisha vibali na kuwatoa.
Narubongo nashukuru sana kwa maelezo yako.je sungura wako ni wa kienyeji au wakisasa?na vp naweza kupata mbegu kubwa kwako?
Nashukuru sana kwa kujali shida yangu.naomba ukipata mtu mwenye hawa sungura uniunganishe nae.biashara itafanyika tuMama timmy samahani kwa kuchelewa kujibu ..msimu wa kilimo huu nimekimbia mjini, ninao sungura chotara wachache na wanatunza watoto vizuri tu kwasababu nimewaweka shambani kwenye mazingira yao ya asili(wanachimba mashimo).. ila maumbo yao kwakweli ni madogo sana (kg 1.5-3) ukimchuna ngozi na kuondoa matumbo ndio kabisa.. na mimi pia nawafuga kwa hobby kama wewe lakini mpango wa kuanza kuwafuga kibiashara upo na kuhusu soko Malila aliniahidi kwa wajuba.. pimbi nao nimewaweka kiasi... sungura kibiashara wana faida kubwa sana.. kwasasa akiwa hai ni kati ya 10-20,000/=.
Kuhusu kupata mbegu bora ya kibiashara unaweza kubahatisha kwenye maonesho ya kilimo kama yale ya nane nane au kenya.. nikibahatisha jinsi ya kuwapata nitawataarifu
Mama timmy samahani kwa kuchelewa kujibu ..msimu wa kilimo huu nimekimbia mjini, ninao sungura chotara wachache na wanatunza watoto vizuri tu kwasababu nimewaweka shambani kwenye mazingira yao ya asili(wanachimba mashimo).. ila maumbo yao kwakweli ni madogo sana (kg 1.5-3) ukimchuna ngozi na kuondoa matumbo ndio kabisa.. na mimi pia nawafuga kwa hobby kama wewe lakini mpango wa kuanza kuwafuga kibiashara upo na kuhusu soko Malila aliniahidi kwa wajuba.. pimbi nao nimewaweka kiasi... sungura kibiashara wana faida kubwa sana.. kwasasa akiwa hai ni kati ya 10-20,000/=.
Kuhusu kupata mbegu bora ya kibiashara unaweza kubahatisha kwenye maonesho ya kilimo kama yale ya nane nane au kenya.. nikibahatisha jinsi ya kuwapata nitawataarifu
Nakuaminia Malila kaka yangu.leo nimepata nafasi ya kumtembelea Mohammed shossi na njiwa wake! ulisema michango ya send off ndo utaikata?ni waziri zaidi ya namna wanavyoonekana kwenye picha.ufugaji lazima ufanyike na soko litapatikana tuu kaka yangu.Niko na mkulima mmoja mkubwa na mfugaji mzuri wa wanyama. Tukishaweka mambo sawa nitaweka kila jambo hadharani.
Niko na mkulima mmoja mkubwa na mfugaji mzuri wa wanyama. Tukishaweka mambo sawa nitaweka kila jambo hadharani.
Nakuaminia Malila kaka yangu.leo nimepata nafasi ya kumtembelea Mohammed shossi na njiwa wake! ulisema michango ya send off ndo utaikata?ni waziri zaidi ya namna wanavyoonekana kwenye picha.ufugaji lazima ufanyike na soko litapatikana tuu kaka yangu.
Pamoja sana kaka yangu.mimi nikipata nitawajulisha hapaha jamvininamimi nipo interested sana na sungura. Naomba mkipata mbegu mnijulishe na mimi
Mama timmy samahani kwa kuchelewa kujibu ..msimu wa kilimo huu nimekimbia mjini, ninao sungura chotara wachache na wanatunza watoto vizuri tu kwasababu nimewaweka shambani kwenye mazingira yao ya asili(wanachimba mashimo).. ila maumbo yao kwakweli ni madogo sana (kg 1.5-3) ukimchuna ngozi na kuondoa matumbo ndio kabisa.. na mimi pia nawafuga kwa hobby kama wewe lakini mpango wa kuanza kuwafuga kibiashara upo na kuhusu soko Malila aliniahidi kwa wajuba.. pimbi nao nimewaweka kiasi... sungura kibiashara wana faida kubwa sana.. kwasasa akiwa hai ni kati ya 10-20,000/=.
Kuhusu kupata mbegu bora ya kibiashara unaweza kubahatisha kwenye maonesho ya kilimo kama yale ya nane nane au kenya.. nikibahatisha jinsi ya kuwapata nitawataarifu
Kivipi?naomba ufafanue ndugu yangu.Hao wako ni maalumu kwa ngozi
Kivipi?naomba ufafanue ndugu yangu.Hao wako ni maalumu kwa ngozi
nimekuelewa sana ndugu yangu.nashukuru sana na tena saaana.nitayafanyia kazi yote hayaUTANGULIZI
Kabla hujaamua kufuga
sungura hakikisha ya
kwamba umejitoa na una
muda wa kuwahudumia
wanyama waha, ufugaji wao si rahisi kama vile ukifuga paka au mbwa, sungura Wanahitaji uangalizi na hasa kwenye usafi kwa sababu ni rahisi kwao kupata maradhi yatokanayo na mazingira
mabaya na machafu
AINA ZA SUNGURA
Kuna aina mbali mbali wa
sungura lakini
wanagawanywa mara mbili
kwa matumizi. Moja ni kwa
matumizi ya ngozi yake kwa
kutengeza kofia, mifuko, na mishipi na pili kuna aina ya
sungura ambao hufugwa kwa
kuzalisha nyama. Mfano wa
aina ya sungura wa ngozi ni
"Angora" ambaye manyoa
yake ni marefu. Na kwa sungura wanaofugwa kwa
nyama ni aina ya sungura
ambao hukua haraka, uzito wa
sungura wa nyama ni kutoka
kilo mbili hadi kilo tano. Bw.
Wachira anafuga sungura anina ya Califonia White na
Newzealand White, Chinchila
Flemish Giant ambaye ni
mkubwa, an pia hufuga
sungura aina ya Flemish
Fender
MABANDA
Kuna aina mbili za mabanda ya kufugia kwanza ni yale yakuwafungia ndani muda
wote bila kutoka nje na ya
pili ni ile ya pili ni nusu nusu
yaani wanakuwa na mabanda na wanaweza
kutoka nje kwenye ua
maalum, katika aina zote
mbili ni muhimu kuhakikisha
hakuna upenyo wa kuruhusu
panya kupita kwa sababu huwa wanakula watoto wa
sungura.
UFUGAJI WA NDANI
1 - Usitumie banda la kioo (aquarium) kwa sababu
halina hewa ya kutosha na ni vigumu kusafisha
2 - Sakafu ya nyavu za waya ni nzuri zaidi ila hakikisha
hakuna sehemu zenye ncha
kali inayoweza kuwaumiza
sungura, kwani wakumia ni
mpaka wapone wenyewe au
umchinje kwa sababu ukitumia dawa za antibiotic
sungura hana uwezo wa
kuzimeng'enya na kuisha
mwilini mwake, siku
ukimchinja atabakia na dawa na hata ukinusa nyama yake utahisi harufu ya dawa
3 - Ukubwa wa banda usipungue mita 4 * 2 kwa kila sungura mmoja, likiwa
kubwa zaidi ni vizuri
4 - Chini kuwekewe matandazio kama nyasi kavu au maranda ya mbao, lakini maranda yatokanbayo na miti yenye mafuta kama mi-pine na mikaratusi hayafai,
wawekee kipande cha blanket au taulokwa ajili ya kulalia na kujifungulia hasa kwa wazazi
5 - Ni muhimu kuwawekea sehemu ya kujificha mara
wanapohisi hatari, unaweza
kutumia mbao, box gumu au
plastiki
UFUGAJI WA NJE
1 - Sehemu yote izungushiwe wavu wa kuku kuzuia panya kuingia na wanyama wengine kama paka, mbwa, mwewe nk
2 - Upande mmoja uwe na mabanda, sehemu ya chakula na maji pamoja na kivuli kwa ajili ya sungura kupumzika
3 - Futi moja chini ya udongo kuwe na zege kuzuia sungura kuchimba na kwenda mbali
4 - Eneo la wazi liwe huru na hatari zote za sumu kama dawa za kuulia wadudu au mbolea, pia majani yaliyoota yasiwe ni yale yenye sumu
(waone wataalamu
wakushauri au ng'oa yote)
MAJI
Tumia mabakuli ya kigae,
plastiki au jengea kwa saruji, maji yabadilishwe kila siku na vyombo visafishwe kila siku
CHAKULA
Wapewe majani, mabaki ya
mboga za jikoni baada ya
kuchambuliwa, pia unaweza
kuwawekea pumba au chakula cha kuku (growers
mash) kwenye vyombo maalum kama chakula chenye virutubisho (concentrates)
USAFI
Kila siku jaribu kuondoa
uchafu kama vyakula vilivyo
mwagika, na kinyesi
kilichoganda kwenya
matandazio, fagia na kubadili matandazio angalau mara moja kwa wiki, manyoya ya
sungura mzazi yasiondolewe
hii huonyesha kwamba
anakaribia kujifungua watoto
MENO
Wakati mwingine meno ya
mbele hukua sana na
kumsababishia usumbufu
wakati wa kula, waone
wataalam ukiona ni marefu
zaidi na yanahitaji kupunguzwa, dalili kuu ni
sungura kushindwa kula kwa zaidi ya masaa 12
MIGUU
Miguu ya sungura si kama ya
wanyama wengine, nyayo
zake zimefunikwa kwa
manyoya, angalia ukiona
yananyonyoka kuna tatizo
chunguza, kucha zake nazi huhitaji kupunguzwa zikikua sana
UBEBAJI
Usimbebe kwa kutumia
masiki yake huwa wanaumia
sana, shika ngozi nyuma ya
shingo kama paka ukitaka
kumbeba
DAWA
Wapewe dawa ya minyoo
kama piperazine kila baada
ya miezi mitatu, dawa za
wadudu kama akheri
powdeer zinyunyuziwe
kwenya mabanda yao kuzuia viroboto, usiwape dawa nyingine bila ushauri wa kitaalamu, antibiotics ndio usijaribu kabisa kama
nilivyosema mwanzo
NB:Epuka kuzaana ndugu kwa ndugu (inbreeding) kwani pia hujenga tabia hii kwa majike, itabidi ubadili majike na baada ya vizazi kadhaa utabadili pia madume ili yasizae na watoto wao
Aksante
Bluetooth vp tena?wiki imeisha tena ndugu yangu.nina moto wa kufuga usiniache mpaka nipoe.nasubiri kusikia kwakoMama timmy
nina vitabu vidogo viwili raising and keeping rabbits part 1&2 ... nilipewa na mtu mmoja wa FAO telefood program .... maelezo yote from A to Z utayapata in very simple and understanding language
kama unahitaji do not hesitate to contact by pm ...
available free of charge