Hapa nina fikra tofauti kidogo na wewe kufuga paka, mbwa au njiwa unaweza kunufaika kiuchumi. kwa mfano ukiwa unazalisha mmbwa kwa ajili ya kuuza ni biashara nzuri sana na ina fedha nyingi sana.
Kwa taarifa yao na wengi sungura hasa hybrid mbegu ya California white, Newzealand na German giant wana soko kubwa ..... kit mmoja wa umri wa mwezi mmoja anauzwa Tsh 20,000 na sungura mkubwa (matured/adult) anauzwa Tsh 30,000 ..... ukienda SUA order ya sungura hawa ina foleni ya kusubiri miezi minne
Nyama ya sungura ni white meat, very delicious,very nutriteous, tender meat and haina uric acids wala na mafuta yake hayana colesteral .... kuna sehemu inaitwa Oceanic Resort ipo Mbweni wanabanika sungura na wanauza sana hawa sungura
Sungura hupevuka ndani ya miezi minne tangu kuzaliwa ..... sungura hujifungua siku ya 32 tangu apate mimba, sungura muda wote huwa mbegu zake za kike zipo tayari kupokea mbegu za kiume tofauti na wanyama wengine ambao huingia kwenye joto kwanza mara moja kwa mwezi, sungura anauwezo wa kuzaa mpaka mara 10 kwa mwaka na huzaa mpaka watoto kumi kwa mzao mmoja
Malisho mazuri ya sungura ni majani (legumes,hay and vegetables)
cereals, proteins, minerals and vitamins .... kama unamjua agent wa chakula cha mifugo cha Hill basi Dairy Pellet Meal ndiyo chakula bora kabisa kwa kulisha sungura wakawa bora
Sungura huchomwa sindano ya minyoo (Bamectin injectible-subcatenoaus) kama kinga na salphurdimadine-intramascular kama kinga ya magonjwa yatokanayo na bacteria kama coccidiossis
Nashauri watu wajikite kwenye ufugaji huu usio na usumbufu na ni rahisi