Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

inasemekana kuwa vijana wenye hasira kali walimtandika vibao Marine Hassan Marine baada ya kuona kusikia kuwa TBC wamekatisha kurusha mkutano.Nilikuwa jukwaani hivyo sikuona tukio hili.
 
Ingalikuwa vyema iwapo Chadema itakuwa imenunua muda kwa hivi vituo vyetu vya TV kwa ajili ya sisi tuliokuwa mbali kushuhudia tukio hilo muhimu. Ila sidhani kama kuna Kituo cha TV kitadiriki kurusha matangazo hayo jinsi walivyo waoga!

tbc walikuwa wanarusha bana ila huku kwetu umeme ulikuwa umekatika nikawa nasikiliza kwenye redio ya simu alipoanza kuonge mabere arando wakakatisha matangazo kwasababu za kiufundi ila wali inyima mengi nilipokatiza maeneo ya tauni nikakuta watu wanaendelea kuangalia kwenye tv wakati huo mkuu wa anga ya saba alikuwa anaongea
 
inasemekana kuwa vijana wenye hasira kali walimtandika vibao Marine Hassan Marine baada ya kuona kusikia kuwa TBC wamekatisha kurusha mkutano.Nilikuwa jukwaani hivyo sikuona tukio hili.

Asantea Regia.

Vyovyote ilivyokuwa message imewafikia wahusika. na ufasadi aliousema Marando sasa ni black and white.

Tunasubiri ama wampeleke mahakamani ama watoe maelezo ya kutosha juu ya tuhuma nzito kama hizi za kutingisha dunia.
 
Ni sehemu ya walafi wale wale ambaye anaona kitumbua kinaondoka
 
TBC news ..saaa mbili:

Tido Muhando anakubali kuwa ni kweli kuwa ni wao waliokata matangazo

WHY?

...eti kulikuwa na matusi ya nguo....

.... Wanasema inawezekana siku zijazo watashindwa kurusha matangazo ya kampeni za CHADEMA...

.... anaogea na vituvingine visivyoeleweka... lakini kwlei wameigwaya CHADEMA...
 

vitu ambavyo dr slaa atavifanya kwa siku zake 100 za kwanza haviitaji pesa za wahisani au nini, vinahitaji nia na maamuzi....
2010 hatudanganyiki......
 

huyo ni Superman
 
Huyu mgombea udiwani 'anaetafutwa' tukimwona tuwajulishe polisi au?
 
pale mkutanoni tuliambiwa ni itilafu ya mitambo, sasa hivi kwenye taarifa tido anasema kwa ajili ya lugha chafu
alikata pale marando alipokuwa anataka kuanika kila kitu, kwa nini hawakukata wakati ambapo wanasema palikuwa na matusi.
safari watake wasitake mabadiliko yatatokea tuuuu
 
Tunawashukuru wote walioshiriki kutuletea matangazo haya moja kwa moja toka Jangwani. Tunaomba moyo huu uendelee, na mabadiliko ya kweli yaja Tanzania kama kila mmoja wetu atajisikia kuguswa na udhalimu tuliotendewa kwa miaka yote hii toka Uhuru, tuikomboe nchi yetu kutoka mikononi mwa walioteka hatutaki kulipa ransom, ni kura yako na ya jirani zako, ndugu zako na rafiki zako!
Hongera Superman, tunaomba walioweza kuchukua clips watuwekee!!
 

pole mzee
 

Nilikuwa nimesahau.
Shirika la habari la taifa linadanganya umma! Kwa nini walisema ni mitambo hapo uwanjani kama kweli walikatisha kwa haki si wangesema tunakatisha matangazo kutokana na matumizi ya lugha chafu?

Walijua reaction ya wananchi ingekuwaje
 


guilds!

Kifo cha nyani miti huteleza
 
Huyu mtu anaitwa michuzi (MZEE WA LIBENEKE) anazidi kujipotezea umaarufu kwa kutumia blogu yake kuipigia kampeni CCM tu kila kukicha utadhani hakuna vyama vingine!!!. Nilitegemea basi hata aweka japo ka habari kamoja ka CHADEMA leo, lakini badala yake anapiga mapicha ya CCM na akina Mama Rwakatare(maombi ya Kampeni),. Chakusikitisha kote ughaibuni anakoenda anaendela kujifagilia kuwa yeye ndie mwenye "blogu ya jamii"" inayowapasha wanatanzania wote habari bila upendeleo.. Inasikitisha kwa msomi kuwa "bias".

UNCLE MICHUZI Kama hujui mkuu unapoteza, jaribu kwenda na wakati wa kutofungamana na upande wowote, vinginevyo utapoteza wasomaji wa blogu yako kwa itikadi zako za upendeleo, ana utajikuta huna nyimbo pale ambapo wapinzani watachukua inchi !!!. Kama hulipwi na CCM katika safari zako au kuihudumia blogu yako, tafadhari toa nafasi sawa kwa vyama vyote kaka kwani ni vya watanzania!!!
 

idiota
 

.
Kifilie mbali chama cha majambazi.
Unataka darasa la namna ambavyo chadema itafanya kazi na mawaziri 20, na jinsi ya kuzigeuza hali za wafanyakazi kwa siku 100, na mengineyo mengi? Basi njoo chadema usomeshwe ukiwa umetulia chamani.
 

Hivi watanzania mnataka Tanzania ya namna gani? Mbona nchi hii imeshiriki kwenye ukombozi wa nchi jirani lakini kujikomboa bado ni kitendawili? Unapokuwa na mawazo ya kupinga watu wenye mtazamo mbadala (CHADEMA) basi wewe una mawazo mgando. Hebu tuachilie mbali na Ilani ya CHADEMA, na tuzingatie nchi hii, kwa miaka mitano iliyopita, chini ya utawala huu imevuna mambo mangapi?
  • Umaskini unaoongezeka kwa kasi, kuliko Rwanda na Burundi ambao nusu ya wananchi waliteketea
  • Viongozi ambao hata kujua kuwa wako pale sababu ya wapiga kura ni sawa na kuandika Thesis ya PhD
  • Hadhi ya Elimu imekuwa ikishuka kila idadi ya shule/vyuo zinapoongezeka
  • Watawala hawana cha kuwaeleza wapiga kura, bali kutumia takwimu zisizo sahihi, au zisizoendana na hali halisi
  • Mifumuko ya bei na kuporomoka kwa shilingi, inahusishwa na vigezo(indicators) visivyostahili
  • Tofauti za kidini kuonekana ni tija, kuliko maendeleo na umoja wa kitaifa
Nchi hii imegubikwa ulemavu wa kifikra zaidi kuliko ulemavu wa kimwili, na kama kizazi kipya kinaendana na hiyo syndrome basi tumekwisha, na sitashangaa kwa sababu, watawala wanageuza uongozi wa nchi kuwa wa kurithishana na sio wa kuchaguliwa kidemokrasia. Tukae chonjo saa mbaya, fanya maamuzi sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…