Elections 2010 Ufunguzi wa Kampeni ya Chadema Jangwani 2010

Regia:nitafutie mfano wa nchi moja tu duniani ambayo mkulima wake bora kabisa alifanywa kuwa waziri wa kilimo!Lol!Jamvi linavutia sana.
 
Halafu wanajisifu kuwa Wasomi wetu wamegawa vyandarua kibao kwa Watanzania. Na hii wanaweka kama Mafanikio makubwa saaana kwao. Cha kufurahisha ni kuwa miradi yao mingi imeisha hivi:

Chadema wamesema kuwa wao ni chama makini wanafanya tafiti.Dr Shein ana Phd lazima alifanya utafiti kwenye PhD yake. Mgombea wako kakiri kuwa hana elimu wala uzoefu.
 

Nimekupata Mkuu.
 
Kwa vyovyote nadhani kuwa CHADEMA hawakuwa makini sana katika kutafuta mgombea mwenza wao. Najua kuwa pale Zanzibar kuna watu wenye elimu nzuri ambao wangeweza kushawishiwa kuwa wagombea wenza badala ya huyu ambaye hata kama ana uwezo mkubwa kiuongozi, swala la elimu yake linaweza kuwa tatizo sana katika kumnadi.
 
Kuna wengine ni wasomi ila mhhhhh. Reagan si alikuwa Cowboy vile. Ila kusema ukweli heri ya darsa la saba kama Makamu wa Rais kuliko Rais kama huyu na tena anatoka nchi ambayo ni Superpower na vifaa vya Neuclia........... Huyu ndiye alianzia U-Mziray....

http://www.youtube.com/watch?v=xMThTEA4M0o&feature=related

Huyu jamaa alipigana na Wakominist na kuwashinda na yeye pia hata University hakufika......
Mwisho akawa RAIS................
Lech Walesa


Regia:nitafutie mfano wa nchi moja tu duniani ambayo mkulima wake bora kabisa alifanywa kuwa waziri wa kilimo!Lol!Jamvi linavutia sana.
 
Si firiii mbali. Niko na wewe. Maana wewe ndiyo unaelekea kufiria mbali! Sihitaji kuja Chadema. wewe sema ikoje na Slaa wako mtafanya na hao mawaziri wenu 20?
Kumbe JK anapata ushauri kwa watu kama hawa la kuwa ma baraza kubwa la mawaziri na anasahau kuwa mbayuwayu
 
Fisadi utamjua tu. Atatafuta kila njia ya kuhalalisha ufisadi wake, hata kutunga takwimu na habari za uongo. Ronald Reagan ndiye aliyeanzisha aina hii ya ufisadi, inaitwa PLAUSIBLE DENIABILITY. Reagan alikuwa msomi, lakini wakati anaondoka madarakani aliwaacha Wamarekani kwenye hali mbaya ya uchumi, lakini si hali mbaya kama alivyofanya George Bush! Ronald Reagan alianzisha kitu kilichoitwa REAGANOMICS, na Bush alifuata mkondo huo kwa sera zake, zikaitwa BUSHANOMICS!

Sasa hawa ni wasomi, tena waliosababisha mamilioni ya Wamarekani kupoteza ajira zao, huku nyumba zao zikinadiwa, wengi wakijikuta hawana pa kwenda!

Bora huyu mwenzetu wa darasa la saba, ambaye hajui kuiba, atakuwa mwadilifu, atazingatia wajibu na dhamana atakayopewa na wananchi, atawawakilisha, hatawaibia! Elimu nyingi inamfanya mtu kuwa MWEREVU na MJINGA PIA! MWEREVU wa kupanga mipango ya KUIBA, MJINGA kwa kufikiria kwamba wananchi hawatakuja KUMBAINI na KUMCHUKULIA HATUA!

Basi, kwenu CCM, subirini "mwali" wenu atolewe Ikulu, 31 Oktoba 2010, arudishwe nyumbani kwao Msoga! Wananchi watatoa hukumu yao, kwa njia ya kura! Wamechoka KUIBIWA miaka nenda rudi!

CCM, hata mpige kelele zisikike hadi mwezini, 2010 Watanzania hatudanganyiki! Hii si kura ya siri tena, ni KURA YA WAZI, KURA YA HUKUMU!

Tumeshasema, CHADEMA itaingia Ikulu, ni zamu ya Watanzania kufaidi matunda ya Uhuru wao. CCM kwa sasa imetosha! Hatuwapi kura zetu!

Mnalialia nini?

Hahahahaha!

-> Mwana wa Haki

--------
Mpaka Kieleweke! People's Power! CHADEMA! VEMA!
 
Tatizo letu watanzania mpaka tunafisadiwa ni kuabudu vyeti, ilihali tunafahamu kuwa vyeti hutengenezwa, kuchapishwa na kununuliwa mitaani. Hivi hawa waandisi tuliona nao ambao wanasababisha wakazi wa Jiji l;a Dar es Salaam kukaa kwenye foleni masaa mawili hadi matatu kila asubuhi na jioni walisoma na kufaulu au wamenunua shahada zao. Basi shughuli hiyo akipewa kama huyo mgombea mwenza wa CHADEMA amabye hajapitia Chuo kinachotoa Shahada za wizi hapao Mlimani anaweza kumaliza tatizo hili ndani ya siku 30.

Msomi kama Chenge, Maramba. Lowassa, Karamagi, Rostam, Msabaha wa nini. Toka Mwalimu amewasomesha bure hadi ulaya viongozi lukuki walioko CCM wamefanya nini kuleta maendeleo. Ni heri sasa ncghi wapatiwe wa daras la saba na Form Four nakuhakikishieni Tanzania itapata maendeleo na vihiyo wote mtapatiwa mitihani upya chini ya usimamizi wa watu wasio kula rushwa mthibitishe hizo digrii zenu kama ni halali.

Mnajidai mmesoama mna MaDigrii ilihali kuzungumza na kuandika kiingereza hamjui,sasa mtihani ya kiingereza mlifanya vipi?

Licha ya mambo ya Ruge na mamengineyo Mimi nilisikia kuwa Mkataba mbovu uliopelekea watanzania kufukiwa wakiwa hai huko Bulyanhulu ulisainiwa na Jakaya Kikwete.

Wahudhuriaji waliokuwa pale ni wapambanaji, sio kama ule mkutano wenu wa kila mtu kupatiwa elfu tano ili ahudhurie
 
Halafu wanajisifu kuwa Wasomi wetu wamegawa vyandarua kibao kwa Watanzania. Na hii wanaweka kama Mafanikio makubwa saaana kwao. Cha kufurahisha ni kuwa miradi yao mingi imeisha hivi:

Vyandarua viligawiwa kwenye nyumba zenye watoto CHINI YA MIAKA 5! Uamuzi huu ulitokana na UTAFITI uliofanywa na wataalam, WASOMI, walioajiriwa na Serikali ya CCM!

Swali: Malaria INACHAGUA umri wa mtu kabla ya kumdhuru?

Swali: Mbu wanauma USIKU tu? Na mchana, je, hawaumi?

Hahahaha!

-> Mwana wa Haki

----------------
Mpaka Kieleweke! 2010 HATUDANGANYIKI! Peoiple's Power! CHADEMA-VEMA!
 

Mbayuwayu anatoa hela zake mfukoni? Mbayuwayu anashirikiana na fisi?...changanya na zako...
 

Michuzi anasikitisha kwa kweli. Ni blogu yake lakini dahh!! Lakini ndio Watanzania tulivyo. Ni culture yetu.
 
Lets not waste time anymore and get out the votes for dr. Slaa, we can trust this man and one day we shall reflect back and tell our children and children children those are the time when we did it, lets do it................................there is no turning back, not this time, not when we have an economy to transform, and a costitution to reform, not when we have resource to protect and farmers to empower, not now when we have mafisadi to send them away.................
On october 31st lets speak loud and clear 50 years is enough..........................................................................................
Watanzania the stake are to high to stay on the sideline, together lets make history and our children will remember us that we did it, may god bless us and bless our country
 
Sasa kama mnajiamini hivyo kimekuleta nini huku kutujazia upupu wenu?
 


...mara zote umaskini wa watanzania ndio umekuwa mtaji wa kura wa ccm ,ninahisi kuna maeneo ambayo ccm haitaki yapate elimu ya uraia na maendeleo kwa makusudi ili waendelee kuwatumia kama..misukule ya kuwapa kura ukija uchaguzi kwa ujira wa kanga ,kofia na fulana ....yaani kama misukule na pumba.....haingii akilini ccm wanajivunia kura wanazoita za maeneo LOYAL,,...kama kusini[kilwa,lindi,ntwara]..na central wakiamaanisha singida ,dodoma ,tabora ......ni kweli haya maeneo have been voting for ccm overwhelmingly.....lakini yamepata nini...huwezi kulinganisha na mikoa ambayo inapiga kura bila kuzingatia sana chama kama Mara,bukoba,mwanza,shinyanga,kigoma,rukwa,mbeya,iringa,arusha ,kilimanjaro,dar es salaam .....mikoa yote hiyo imepata kuwa na wabunge wa upinzani...nani anaweza kubeza population ya wananchi wa mikoa hiii......

sidhani kama kuna mwanademokrasia atakayeshangilia ushindi wa kina membe na mkono...masha wa kupita bila kupingwa ....demokrasia imebakwa ...nani hajui matukio ya wagombea maskini wa upinzani kupewa mamilioni ili wajitoe??? nani hajui matukio ya wagombea walioporwa fomu wakiwa njiani kurudisha fomu....?...AMABO walikwepa yote hayo walipakaziwa kuwa wao si raia.......je huko ndiko kupita bila kupingwa tunakoweza kujivunia...???? sidhani...sidhani.....nadhani tunatania....
 
What a great day to be remembered! I, myself, was there at Jangwani grounds.

Najua CCM nyuso zimewashuka; na mahasira kibao. Mtajiju.

msisahau wananchi kwa maelefu waliojaa pale jangwani na kufurika ......umati ule ni mkubwa sana...wote wamekuja kwa nauli zao ...wala hawajalipwa pesa .....zaidi ..wamekuja kuchangia pesa ...na hata uchangamfu uliokuwapo ni mkubwa sana....huwezo kulinganisha na umati wa kukodiwa wa ccm....hata kura zao ni za kununua....wao walitumia mamilioni kuwalipa wananchi waliohudhuria pale pesa ...[kama hukupata kwamdai balozi wako ].....walipeleka mabasi kila kata ....na magari mengine kubeba watu.......ukipanda unapewa kifuta jasho .....ie elfu mbili na fulana .......ndio maana watu waliohudhuria mkutano wa ccm walikuwa hawajachangamka kabisa.......hata pamoja na kuwa na bendi na wasanii wa bongo fleva kama 50 .....mood was too dull..
 
Hivi hawa jamaa hawajui kuwa viongozi wenge ndani ya ccm wamefanya ufisadi hadi wa ku forge elimu zao na jk ni mmoja wao amepewa u dr. Wa nadhalia na ki group cha familia moja ya wazungu wajanja ambao wapo kenya wanatafuta pesa na hicho chuo cha nyumbani kimepata scandal kenya na kimeamua kubadilisha jina kuwa sio chuo kwasababu ya vyombo vya habari kenya kuwaanika kuwa wanauza phd kwa wakuu mbalimbali wa nchi afrika, na chuo chenyewe ni kama richmond kwani hata marekani hakitambuliki. Hebu mtu mwenye mda wa kutosha apost hiyo clip ipo kwenye wall ya mtumishi zito kabwe kwenye facebook, huo ni ufisadi inabidi kuvalia njuga kikwete hana phd amenunua kwenye chuo ambacho nikama richmond, nitaitafuta hiyo clip ya kenya tuwaonesha hawa jamaa, mtu akiwa mkweli tunamshambulia, je hao vihiyo wa ccm, kuna kihiyo mwingine anaitwa athon dialo hana vyeti lakini kadanganya kuwa kasoma harvad, kuna kihiyo mwingine anaitwa richard ndasa..................................
 
Superman, Regia mmefanya kazi kubwa sana kuwahabarisha watu ambau kwa njia moja au nyingine hawakuwaweza kuhudhuria mkutano wa Ufunguzi wa kampeni CHADEMA. We really appreciatea that. Mlivyodondosha nondo hapa, wale ambao hawakuwepo utafikiri walikuwepo couple of metres from Jukwaa kuu.

Mkuu invisible, je kunahitajika video camera kuchukuwa matukio ya kampeni? Ni vema memba tukajua kama kuna mahitaji ambayo twaweza kusaidiana. Tunahitaji kujionea sisi wenyewe haya matukio badala ya kusubiri edited video na propaganda machines. Please let me know how I can help about that.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…