Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo ni kukumbushwa sio kuongea, alikazania mahakama ya kisutu, Ruge na Ufisadi
msisahau wananchi kwa maelefu waliojaa pale jangwani na kufurika ......umati ule ni mkubwa sana...wote wamekuja kwa nauli zao ...wala hawajalipwa pesa .....zaidi ..wamekuja kuchangia pesa ...na hata uchangamfu uliokuwapo ni mkubwa sana....huwezo kulinganisha na umati wa kukodiwa wa ccm....hata kura zao ni za kununua....wao walitumia mamilioni kuwalipa wananchi waliohudhuria pale pesa ...[kama hukupata kwamdai balozi wako ].....walipeleka mabasi kila kata ....na magari mengine kubeba watu.......ukipanda unapewa kifuta jasho .....ie elfu mbili na fulana .......ndio maana watu waliohudhuria mkutano wa ccm walikuwa hawajachangamka kabisa.......hata pamoja na kuwa na bendi na wasanii wa bongo fleva kama 50 .....mood was too dull..
Mimi pia nitachangia,sitaki habari za kuchakachuliwa na akina Marin Hassan,matokeo yake wanaishia kupata vipigo lol!Tuko pamoja Mkuu. asanteni wote.
Regia pia ameonyesha ushirikiano mkubwa sana. Anastahili pongezi.
Mkuu Invisible, in case kutahitajika Video Camera aanytime, na mimi pia naungana na Indume, naweza kutoa yangu pia.
Naamini sana JF inafanya kazi yake vema kipindi hiki.
Nimeisoma ilani ya Chadema na mwanzoni kabisa nimeanza kuona tatizo lile lile ambalo Chadema wanasema wanapingana nalo.Longolongo na kutoweka jambo wazi kwa mapana yake.Sehemu iliyoanza kunipa mashaka kabla hata sijafika mbali ni hii:
Katika sehemu hiyo ni wazi kuwa Chadema wanataka umma uamini kwamba matatizo yote tuliyo nayo yanatoka na utawala!Ufisadi ni nini?
Tunapozungumzia Ufisadi tunazungumzia mfumo na muundo wa utawala ambao umetengeneza utamaduni wa kuishi kiujanja ujanja, matumizi mabaya ya madaraka na vyeo, ufujaji wa mali ya umma, wizi wa fedha za umma, utaratibu wa kubebana na ajira zinazotegemea kujuana, na mahusiano ya watawala na watawaliwa ambayo msingi wake ni woga, vitisho, na kujiona watu wanastahili zaidi kuliko wengine. Ni mfumo uliodidimiza tawala mbalimbali duniani na ambao pasipo kuushughulikia kwa makusudi unasimama kama tishio lilopo na la hatari kwa Tanzania kuliko vita. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alisema kuwa "ufisadi na rushwa ni adui mkubwa zaidi wa maslahi ya wananchi wakati wa amani kuliko vita" (Bungeni, Mei 17, 1960, kikao cha 35 cha bajeti).
Ufisadi ndio kizuizi kikubwa cha kuboresha maisha ya watu wetu; ni kikwazo kikubwa katika kujenga na kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria na haki za raia. Ufisadi ndio kikwazo kikubwa kabisa cha maendeleo ya nchi. Ndio kusema, juhudi zetu za kujiletea maendeleo kama nchi haziwezi kufanikiwa bila kwanza kukomesha ufisadi.
Tumekuwa na miaka takribani 50 ya CCM. Wameahidi kila aina ya ahadi na wamefanya kila makosa, lakini tukawavumilia na tukawapa nafasi nyingine tukiamini kwamba mambo yatabadilika. Kila tulipowapa nafasi, hali ilizidi kuwa mbaya, tukasogea kutoka kubaya kwenda kubaya zaidi. Lengo lao kubwa limekuwa ni kushinda uchaguzi, ili waendelee kutumia madaraka tunayowapa kwa ajili ya kujinufaisha kwa njia ya ufisadi.
Ni wakati wa mabadiliko, na fursa ya kufanya mabadiliko ni huu uchaguzi wa 2010 na siyo 2015. Tukisubiri wakati mwingine tutakuwa tumechelewa sana. Na tukiwapa nafasi nyingine moja CCM ya kututawala tena tutakuwa tumewapa leseni ya kuendelea kutawala wapendavyo na tutakuwa tumejihukumu sisi wenyewe na uzao wetu katika maisha ya umaskini wa kudumu.
Wanataka tuamini hata wale watu wanaotumia vyandarua kufugia kuku badala ya kujikinga na malaria kuwa ni tatizo la watawala.
Wanataka tuamini kuwa serikali inawafuatilia wakwepa kodi sugu kuwa ni unyanyasaji simply kwa sababu JK kapita mahali basi hata kama TRA walitaka kudai kodi basi wasidai tena.
Wanataka tuamini hata kushindwa kwetu kuweka akiba na kujaa kwenye sehemu za starehe siku za kazi,kuchangia mambo ya burudani zaidi kuliko elimu na maendeleo yote hayo kuwa ni tatizo la serikali!!!!!
Ilani haisemi kwamba hakuna chama kinachoweza kuwaondolea watu umasikini kwa asilimia mia. Natumaini Chadema watajipanga zaidi miaka ijayo kuelezea wananchi kwamba elimu ya kujitambua binafsi ni muhimu sana kabla ya lolote.On top of that Chadema inasema kwamba 2010 ndo wakati muafaka!!!
What are the justifications kwa hili??U mean 2010 ndo Chadema imeona nchi inaporomoka au ni ile "I wana be the boss too"!!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Mimi ni fuasi wa Chadema ila kwa hili wameniacha hoi kwa kweli. Sina hamu!!!!!!!!
Wameshasema mbona. Kwami watachelewa. Mfa maji hukamata hata nyasi!!King ebu nyosha maelezo u mean mpaka apo Jangwani hamna mawasiliano,wamekata umeme.
Ebu fafanua pls.
CCM mwaka huu imekula kwao.
Amenifurahisha Marando kuwa vyombo vya habari kesho wasije sema Makani ameanguka kam Kikwete,wajue fika Makani ana 80 something na JK is only 57 so ni kama first born wake
Hebu rudi kwenye shimo ulilotokea haraka!MwanaHaki, ni vizuri kwenye UKWELI kutoongopa, haisaidii kitu kuongopa. Naijua vizuri familia ya kina Halima Mdee, Halima ni MKRISTO, kama alivyo Baba na Mama yake, bali ndugu wengi wa Baba yake ni WAISLAMU. Nikija kwa Anna Komu, alikuwa anaitwa Maulidah kabla ya kubadili dini na kuwa Mkristo. Hivyo Halima Mdee na Maulidah Anna Komu wote ni Wakristo.
Ukiwa katika haki uongo wa nini?.
IBAN/SWIFT codes kwa waliopo nje ya nchi tafadhali.Kushiri SASA kuna Njoia Nne:
1. Muda wa Kutoa Sadaka kwenye Mikutano yote - Sadaka ya Ukombozi
2. Accounti 2 za Benki : CRDB Bank: CHADEMA M4C (Sadaka zinakusanywa)
A/c 01J1080100600; NMB: A/C CHADEMA: No. 2266600140
Katika uzinduzi wa kampeni za chadema jana nilishangazwa na tukio la mgombea urais wa chadema kusahau kuzungumzia uchumi wa taifa. Ambapo ndio kitu muhimu sana. Yeye alijikita na habari za ruge na house of talent, badala ya kujadili issue za kitaifa. Wao ugomvi wa watu wawili wameufanya ndio sera za chama. Akajikita na uendeshaji wa kesi mahakama ya kisutu.
Kama chama chadema kingezungumzia suala za uendeshaji kesi zote yaani mfumo wa sheria nchini, sio kujadili kesi moja au mbili za mahakama ya Kisutu.
Slaa ameshindwa kusema kuwa JK amechagua majaji wangapi kurahisisha mfumo wa sheria.
Nilivunjwa mbavu pale John Shibuda alipompelekea desa bwana slaa kuwa mzee umesahau kuzungumzia uchumi. Slaa kwa ufahamu wake mdogo akatamka hadharani akisema 'nakushukuru ndugu yangu Shibuda kwa kuniletea karatasi kunikumbusha nizungumzie uchumi"
Chama makini kingezungumzia uchumi kutokana na mambo kadhaa yaliyojiri hivi karibuni dunian na hapa nchini mambo kama credit crunch na mengi ya mfano huo. Riba na uchumi wa nchi. Yeye alikuwa busy kuzungumzia neno moja tu ufisadi.
Sasa kama shibuda angekuwa hayupo jana ingekuwaje? Hilo ndio tatizo la chama kuwa na watu wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne kama mbowe na mgombea mwenza wa Slaa.
Mgombea mwenza angekuwa msomi au mwenye uelewa angemsaidia Slaa.
Chadema mshukuruni sana Shibuda kafanya kazi nzuri ingawa hamkumpa nafasi ya kuzungumza.
Kama ule umati wa jana unaitwa "kufunika" na "Jangwani kufurika" basi huo ni ushahidi tosha kuwa hao wanaoripoti hizi habari ni wageni wa mikutano ya kisiasa hapo Jangwani.
Umati wa jana pale Jangwani hauna tofauti na ule wa CUF aliokusanyika kule Kidongo Chekundu juzi. Tofauti ni kuwa CUF hawakujisifia na huo umati kwani walijua kuwa ule umati uliojitokeza kumsindikiza Prof. Lipumba kurudisha fomu ofisi za NEC ulikuwa mara tano mkubwa kuliko huo uliokuwa wakati wa kuzindua kampeni.
Very contradictory!!!Naamini watanzania wana macho na masikio.Kama wapinzani ni wa dizaini hii,CCM itakuwepo for lots of years to come.