Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Hizo story mlizipata wapi jamaa nani alikuepo huko kama sio habari za kutungwa tuu... Et mtu anasimulia mambo ya mbinguni..[emoji23] anasimulia mambo ambayo kabla ya dunia kuumbwaa..

Tuache kutunga
 
Mimi nimesema shetani na malaika wake/majini kifo kimewashinda.

Hao malaika watatu walio mtembelea Adam mimi na sema si malaika ila ni Mungu alimtembelea akiwa katika utatu mtakatifu ambapo kila nafsi yake iliuvaa uwanadamu.

Kwa nini mchukue baadhi tu ya mistari? Nini kiliwatokea hao uliowaita wananchi?


 
Naona wewe ni mgeni wa hili jukwaa. Hapa tunaeleweshana na kushare maarifa hakuna mwenye wafuasi hapa kwakuwa hiki sio chama cha kisiasa, kikundi cha kiimani au group la wasanii... Huku ni intelligence kunakojadiliwa yasiyojadiliwa kwingine

Intelligence ndio imegeuka upotoshaji? Hivi ulitarajia kwingine wajadili huu upuuzi unaouita intelligence.

Hivi Mungu anamuogopa huyu Lilith kiasi gani mpaka afiche ukweli kuhusu yeye kama kweli ali muumba? Au unataka kuniambia wanadamu wanaweza kuficha jambo ambalo Mungu alitaka lijulikane? Oooh mara Biblia imeficha mambo mengine. Manabii wa uongo mpo na bahati nzuri kwetu na mbaya kwenu Mungu alitufundisha jinsi ya kuwa tambua, kwa matendo yenu.

Mungu alivyo na neema kuu bado anawapa pumzi na uzima ili muendeleze haya unayo ya ita intelligence.
 
"Sasa huyu" ujue hii ni demostrative pronoun kimsingi amaonyesha. Swali anamuonyesha nani?. "Bwana akafanyia usingizi, anapozinduka akamuona mwanamke . Hili ni tangazo la kuonyesha kwa Mungu.

Kumbuka gwaride la wanyama lilipita mbele za Adamu akawaita majina huyo maye anampa jina mbele za Bwana
 
Umeelewa swali langu mkuu?? Nmesema kma walikula wakanywa maji na bado walitaka kuingiliwa je hauoni kwa mfumo huo huo wa kuvaa mwili basi na wenyewe wana uwezo wa kumuingilia mtu kma wakitaka

Nmeuliza pia kma maria aliweza kupata mimba kwa uweza wa roho mtakatifu kwanni usiamini pia malaika kma viumbe wa mbinguni wana uwezo wa kutungisha mimba hata bila ya kumuingilia mwanamke???

Tueleweshane taratibu ili tuwe ukurasa mmoja.... Ahsante
 
Kwa imani yangu mimi Yesu ni Mungu na yeye ndiye mwanzo wa yote na alikuwepo kabla ya haya yote uliyo yataja hapa. Kwangu mimi hakuna cha ajabu hapa. Zaidi ya kusema ni uongo wa yule baba wa uongo akitaka kujinasibisha na Mungu ili akupate wewe na wa aina yako.


 
Malaika hawana uwezo kama wa Mungu bali wanapewa uwezo na Mungu akitaka kuwatumia kwa utukufu wake na anafanya mambo yake kwa ukuu na utukufu wake si kwa huu upuuzi unao ongelea hapa. Wala usishangae Mungu kula jaribu kutafiti ni vitu gani Mungu alivyo wahi kutolewa kama sadaka. Mwisho wa siku Mungu ni muweza wa yote.

 
Kwanza hakuna upotoshaji maana lilith kajadiliwa na maprofessor wengi tu na kwa ushahidi wa ancient sumerian texts ndio maana hata kwenye biblia ametajwa...... Kwahiyo anajadili kitu ambacho kipo sio stori za mdomoni kma popobawa!!!

Kingine unadai mwanadamu hawezi kuficha jambo ambalo Mungu anataka lijulikane?? Je unajua mangapi kwenye historia ya imani tumefichwa hata kma ni kwa nia njema

1. Maisha ya Yesu kwenye biblia yapo 10% pekee ila ujana wake wote na maisha binafsi haupo katika biblia hii ya kiprotestant ila vitabu vilvyoandika maisha ya Yesu in details vilitolewa unajua na nani na kwanni??

2. Kuna kitabu kimejadili masuala kabla dunia haijaumbwa wala kuwepo ila kilitolewa je unajua kwanni na nani alikitoa?? Je mshana jr akisema kuna vitu tumefichwa utakataa

3. Hivi unajua paulo aliandika nyaraka takribani 60 ila biblia unayotumia ina barua zake 21 pekee!! Unajua lini zilitolewa na kwanni???

Dah ni mengi mkuu tumefichwa ni vzuri ufanye utafiti kuliko kumkejeli mtoa mada ambaye ana nia nzuri ya kutufikirisha
 
Kwahiyo aliyepigana na Yakobo hakuwa malaika???

Kwahiyo waliokula kwa abraham walikuwa sio malaika??

Nachouliza kma malaika waliweza fanya yote ya mwilini kwanni huamini anaweza lala na mwanamke na kupata mtoto???
 
Kwa staili hii hautawahi ongeza maarifa.... unaposema ni uongo mbona Yesu anaitambua embu soma hapa

Matthew 11:23
"And you, Capernaum, will not be exalted to heaven, will you? You will descend to Hades; for if the miracles had occurred in Sodom which occurred in you, it would have remained to this day.

Na kuna mistari mingine 10 inamtaja huyo hades mtoto wa cronus ambaye alifungwa Tertullus huko chini ya dunia mpaka leo ssa unaposema ni uongo tukueleweje ilihali Yesu alimtambua?? Bado kusahau Matendo 14 utaona zeus na hermes hawa wanatajwa..... Je unaposema ni uongo kivp watambulike na paulo na barnaba???

Mkuu panua ufaham kejeli hazisaidii
 
Kwa lugha yako hii ni ngumu kujadiliana.. Na huna kifua cha mijadala mizito kama huu
 
Mie nasikia tu kwenye vitabu vilivyoachwa na baadhi ya maandiko yaliyotoholewa yalimpa nguvu sana mwanamke
Na ndiyo maana havikuwekwa wazi

Nani alishawahi kukutana na baadhi ya maandiko atupe ukweli!

Pengine na Lilith alikuwepo kweli!
 
Hizo story mlizipata wapi jamaa nani alikuepo huko kama sio habari za kutungwa tuu... Et mtu anasimulia mambo ya mbinguni..[emoji23] anasimulia mambo ambayo kabla ya dunia kuumbwaa..

Tuache kutunga
wewe kama huamini uwepo wa MUNGU achana wanaoamini wajifunze.unaita habari za kweli.kuwa ni story za kutungwa shame on u
toa story za kwel bas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…