Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Nilirejea kuisoma Mwanzo sura 1:26ff na 2 (nzima) na kubaini jambo ambalo limenipa kuuliza swali kwa mleta uzi huu kwamba kama mke 'wa awali' wa Adam alikuwa ni Lilith (Is. 34:14) ni vigezo gani vimetolewa kudhibitisha hilo beyond doubt?
 
Na mimi niko kwenye hilo hojaji lakini kuepuka marudio naomba usome replies za zitto junior zina ufafanuzi mzuri sana
 
Na mimi niko kwenye hilo hojaji lakini kuepuka marudio naomba usome replies za zitto junior zina ufafanuzi mzuri sana
Nimemsoma na tangu Mwanzo wa Uzi huu hata sasa sijaacha kitu hata dot; hata inputs za Zitto jnr nimezihifadhi kabisa; ila bado hajadadavua vya kutosha.

Kwa mfano, ktk Mwanzo 1:27-30 Biblia inazungumzia uumbwaji wa me & ke na umilikishwaji wa raslimali zote; lkn ktk Mwanzo 2:7 tunaona Bwana ANAMFANYA mtu!

Je, na huyo wa mwanzoni kwenye Mwanzo 1:27 ndio nani?
 
Hapa kwenye huu mstari ulio unukuu kilichokuwa kinaongelewa ni ugumu wa mioyo ya hao walio kuwa Kapranaum. Kuwa pamoja na miujiza yote na mambo makuu ya Mungu bado hawakuamini. Miujiza hiyo ingefanyika hata sodoma na gomora wangali badili mioyo ya iliyojaa kutenda uovu na dhambi wakamgeukia Mungu.

Soma Biblia yako vizuri sababu ya Yakobo kupewa jina la Israel iko wazi. Soma pia maongezi ya wale Abraham na wale watu watatu anapo wasihi. Mwanzo 18:3. Watu watatu anawambiaje "Bwana wangu"? Si ange wa ambia bwana zangu.

Mwanzo 18:9 Wakamwambia...
Mwanzo 18:10 Akamwambia... Ukitulia na kutafakari haya maongezi na majibizano utaona ni Mungu katika zile nafsi zake tatu abawasiliana na Ibrahim.

Kwahiyo aliyepigana na Yakobo hakuwa malaika???

Kwahiyo waliokula kwa abraham walikuwa sio malaika??

Nachouliza kma malaika waliweza fanya yote ya mwilini kwanni huamini anaweza lala na mwanamke na kupata mtoto???
 
Kwa lugha yako hii ni ngumu kujadiliana.. Na huna kifua cha mijadala mizito kama huu

Hamna mjadala mzito hapa ila niufinyu wa akili zenu za kibinadamu ambazo mwafikiri kwa kuzitumia hizo bila kuomba msaada wa Mungu mtayaelewa Maandiko Matakatifu bila kuyapotosha.
 
Tanua fikra usiwe kama pakacha unameza tu bila kuchuja ukiambiwa ukweli utakuweka huru tafuta ukweli sio kuamini tu unachohubiriwa jiongezee

Wewe msukule wa shetani utanishauri nini? Maana umepita darja la kuwa mfuasi wa ibilisi wewe ni msukule wa shetani.
 
Hamna mjadala mzito hapa ila niufinyu wa akili zenu za kibinadamu ambazo mwafikiri kwa kuzitumia hizo bila kuomba msaada wa Mungu mtayaelewa Maandiko Matakatifu bila kuyapotosha.
Okay sawa asante kwa kushiriki mjadala... Kwangu mimi kila mchango ni somo bila kujali kama una mtazamo hasi au chanya
 
MWANZO 19
1 Basi, wale malaika wawili wakaja Sodoma jioni; na Lutu alikuwa amekaa mlangoni pa Sodoma. Lutu akawaona akaondoka akaenda kuwalaki, akainama kifudifudi.
2 Akasema, Bwana zangu, karibuni nawasihi mwingie nyumbani mwa mtumwa wenu, mkalale, mkanawe miguu yenu, hata asubuhi mwondoke na mapema mkaende zenu. Wakasema, Sivyo, lakini tutakaa uwanjani usiku kucha.
3 Akawasihi sana, nao wakaja, wakaingia nyumbani mwake. Akawafanyia karamu, akawapikia mikate isiyochachwa nao wakala

Mkuu ukifuatilia mistari hii utagundua malaika walimtembelea lutu na waliweza kufanya mambo yote wanayofanya binadamu

Walikula walikunywa walitaka kulala na walioga pia ssa najiuliza kma walikuwa na ubavu wa kufanya mambo yote ya mwilini kwanni huamini kwamba walikuwa na uwezo wa kufanya ngono???

Kwanni mengine waweze ngono washindwe embu tuanzie hapo
 
Wewe ulisema greek mythology ni stori za kufikirika hiyo mistari inamtaja zeus hades na Hermes sasa ndio nakuuliza kma Yesu aliwataja hao Miungu wa kigiriki kwanni wwe unasema ni story za kufikirika?? Je nikuamini wwe au Yesu
 
Okay sawa asante kwa kushiriki mjadala... Kwangu mimi kila mchango ni somo bila kujali kama una mtazamo hasi au chanya
Mkuu mshana jr we ni mmoja wa viungo muhimu sana huku jukwaa la intelligence kwa thread zako zenye madini.... Huyo hayuko tayari kujifunza ila asikuvunje moyo maana tulio wengi tunakusupport
 
Maelezo marefu eti unajenga hoja. Kabla ya kufanya hivyo unge jiuliza maswali haya, wanyama si nyama na mifupa,? Je nyama na mifupa yao ilitoka kwa Adam? Haikudhaniwa wangempa kampani Adam? Lengo hilo lilifanikiwa/lilitimia? nk nk.

Wewe ulisema greek mythology ni stori za kufikirika hiyo mistari inamtaja zeus hades na Hermes sasa ndio nakuuliza kma Yesu aliwataja hao Miungu wa kigiriki kwanni wwe unasema ni story za kufikirika?? Je nikuamini wwe au Yesu

Niangalie tena vizuri, utakuwa umenifananisha.
 
Mkuu mshana jr we ni mmoja wa viungo muhimu sana huku jukwaa la intelligence kwa thread zako zenye madini.... Huyo hayuko tayari kujifunza ila asikuvunje moyo maana tulio wengi tunakusupport
[emoji120] [emoji120] [emoji120] am humbled.. Nimekualika tayari kwenye mada ya laana naye namualika. Tujifunze pamoja
 
Nilirejea kuisoma Mwanzo sura 1:26ff na 2 (nzima) na kubaini jambo ambalo limenipa kuuliza swali kwa mleta uzi huu kwamba kama mke 'wa awali' wa Adam alikuwa ni Lilith (Is. 34:14) ni vigezo gani vimetolewa kudhibitisha hilo beyond doubt?
Mkuu TRIPLE H hakuna mstari direct kwenye biblia unathibitisha kuwa lilith alikuwa ndie mke wa adam kabla ya Hawa ila nje ya biblia zaidi ya jamii nyingi za kale zilitambua uwepo wa Lilith kuanzia Egyptians Assyrians greeks mpaka sumerians bila kusahau babylon wote wanaitambua hii stori na imeandikwa kwenye vitabu vyao vingi ila kwenye biblia kama nilivyoeleza hapo mwanzoni wanaipa hoja yao mashiko kupitia kulinganisha mwanzo 1 na mwanzo 2

Hivyo basi kwa kuwa wana conclude mwanamke aliyetajwa mwanzo moja ni tofauti na mwanzo 2 basi inatoa fursa kwa hoja ya kwamba lilith kweli alikuwepo Eden sababu kuna ka upenyo kameachwa apo

Na mstari wenyewe ni hapa tu

22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

23 Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume

Hivyo kwa hitimisho lao ni kwamba kama lilith asingetajwa popote basi wasingediriki kusema mwanzo 1 na 2 zinaongelea wanawake 2 tofauti.... Ila kwakuwa kuna story ya jamii karibu zote za mashariki ya kati kuwa lilith alikuwepo eden afu muda huo huo biblia imeacha huo mwanya hivyo walioanzisha nadharia hii wameishia KUCONNECT dots kuwa lilith existed

Cjui inaeleweka ama bado
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…