Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Kumbuka biblia ni compilation tuya vitabu iliyofanywa na wazungu wachache pale constantinople na baadae alexandria yaani katika vitabu 400+ vilichukuliwa 66-72 pekee sasa inakuwaje useme biblia haijaandika??
Mkuu kabla ya mkutano mkuu wa Constantinople kufanyika fahamu kwamba tayari kuna watu walikuwa na vitabu vilivyokubaliwa kama maandiko matakatifu, na ndiyo hiyo tunaiita Biblia leo hii.

Mfano mzuri ni "Polycarp of Smyrna", huyu na kanisa la MUNGU tayari walikuwa na maandiko haya kabla hata ya kanisa la Rumi katika karne ya 1. Polycarp alikuwa ni mwanafunzi wa Yohana yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo. Yohana na Polycarp waliishi pamoja kwa miaka mingi.


Isaiah na kwenye moja ya maono akifananishwa na BUNDI ila king james version original inamuita LILITH..... Hivyo si kweli kuwa kwenye biblia hajatajwa.
Mkuu binafsi nimesoma kitabu chote cha ISAYA na mahali unaposema anamzungumzia Lilith na kumfananisha na Bundi au zimwi siyo kweli kabisa. Pale ISAYA alikuwa anazungumzui kitu kingine tofauti kabisa na wala siyo huyo Lilith mnayemsema ninyi. Isaya 34:14-17, hapa tunaona Isaya anamzungumzia "Satyr". Maana ya Satyr kutoka lugha ya kiingereza ni "mwanaume mwenye matamanio ya kingono" na siyo mwanamke.

Kama nilivyosema hapo mwanzo, shetani amekuwa akitunga mambo mengi sana ya uongo ili kuwapotosha watu. Na maandiko haya yenye kupotosha hayakuandikwa leo, yaliandikwa zamani sana za kale enzi za akina Nuhu hasa baada ya Nimrod kuijenga Babeli. Pale Babeli ndipo maandiko mengi sana ya kipagani yalipoanzia na kuenea dunia nzima. Vitabu hivi au maandiko haya yenye hadithi za uongo kanisa katoliki walitaka kuviweka kwenye BIBLIA, lakini Watakatifu wa wakati ule wakiongozwa na ROHO MTAKATIFU wakakataa kata kata.

Leo hii kanisa katoliki linavyo vitabu hivi(pseudepigrapha) na linavitumia katika mafundisho yake, mfano mzuri ni kitabu cha Injili ya Thomas(gospel of Thomas), Book of the Maccabees n.k.
 
Eti ni kama jina la LUCY nasikia wazungu waliompenda shetani walikuwa wanafupisha jina la lucifer wanawaita watoto wao LUCY nasisi eti tunageza......
Maana hata hawa wanamuziki now bado wanamfupisha wanamuita Lucy kama kendrik lamar ana nyimbo kabisa inaitwa LUCY na anasema maana yake ni lucifer.....Ati ni kweli??
 
Paragraph ya mwisho inaweza kuwa ndio jibu sahihi
 
Kwanza kuna points nyingi muhimu umeziruka inawezekana ni kutokana na uhalisia
Soma tena uone asili ya Lilith/ibilisi..
Pia angalia uone hakuna panaposema ibilisi alikula tunda
Zaidi ni kwamba nimeandika kuwa tayari lilith alishageuka roho ya kuzimu na roho haifi
 
Hayo nimawazo ya watu tena potofu nimesoma PhD ya Theology na nmesoma pia Missiology hamna vitu kama hivyo its better kutoendelea kusambaza uongo huu kwa wengine
Hongera kwa kusoma na kufikia level hizo.. Inategemea na taasisi iliyokupa hizo awards, kama ina mlengo wa kuamini kipi... Inawezekana tunachojadili kikawa kipya huko kwenye PhD na degree za kwenu
 
Umepata wapi hii.?
 
Hongera kwa kusoma na kufikia level hizo.. Inategemea na taasisi iliyokupa hizo awards, kama ina mlengo wa kuamini kipi... Inawezekana tunachojadili kikawa kipya huko kwenye PhD na degree za kwenu
Kuna kitu kinaitwa Missiology sio kila chuo kinatoa hii nminahusu vitu vilivyofichwa kwenye Bible na huwezi kuvipata kwenye Theology ndio maana inaitwa Missiology humo utakutana na kitabu cha Henoch kunamambo mengi mno
 
Kwani ni vigumu sana kuamini Mungu bila kuwa na simulizi kama hizi..!?

Kitabu kinajaribu kueleza kwa wepesi tu tena bila mushkeli na kutanabaisha kufikia mioyo ya Vitoto_katika utambuzi wa nguvu mbili kinzani (yin & yang)

Ili kuwajenga viumbe kuwa na welewa na utambuzi katika utendaji wazo na kuzitumia kufikia ukomavu

Lakini bado madoido ya ushehereshaji hayaishi

Utengenezaji wa taarifa nyingi siku zote huandaa ugumu wa upatikanaji wa taarifa sahihi kwa kizazi kijacho

Nachelea tu msije wataabisha watoto wachanga Mkaja kuvuna hesabu yake_karma haidanganyi
 
Hakuna mahali Lilith anatajwa kwa BiBlia. Its a Demon coupled with a demon akimuacha Adam na hii story haipo kwa Bible.
 
Unaamini kabla ya Adamu kulikuw na watu wanaishi?!

Je waamori walikuwa zama gani kabla ya Adamu au baada ya Adamu?!

Biblia haisemi kila kitu,Biblia ni maungano ya machache kati ya mengi yaliotukia katika ulimwengu huu na bado biblia imetumiwa kubeba matabaka uyaonayo katika ulimwengu huu
Si Quran ama Biblia iliokamilika hivyo maarifa mengine ya kumjua mungu na harakati zake za kuwafanya wanadamu wamjue yakupasa kuyajua mengi ili umfuate yeye alie mkuu achana na propaganda za kuingiza siku za jua katika utawala wa Mungu.

Eg. Christmas,Pasaka,Idd...........
 
Hayo nimawazo ya watu tena potofu nimesoma PhD ya Theology na nmesoma pia Missiology hamna vitu kama hivyo its better kutoendelea kusambaza uongo huu kwa wengine
Kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti kabisa jumlisha uwezo wa kutafsiri na nia ya kutafuta maarifa ya ziada nje ya kile ulichosomea kwa maana ya kufaulu na kupata daraja fulani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…