Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Kumbuka biblia ni compilation tuya vitabu iliyofanywa na wazungu wachache pale constantinople na baadae alexandria yaani katika vitabu 400+ vilichukuliwa 66-72 pekee sasa inakuwaje useme biblia haijaandika??
Mkuu kabla ya mkutano mkuu wa Constantinople kufanyika fahamu kwamba tayari kuna watu walikuwa na vitabu vilivyokubaliwa kama maandiko matakatifu, na ndiyo hiyo tunaiita Biblia leo hii.

Mfano mzuri ni "Polycarp of Smyrna", huyu na kanisa la MUNGU tayari walikuwa na maandiko haya kabla hata ya kanisa la Rumi katika karne ya 1. Polycarp alikuwa ni mwanafunzi wa Yohana yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo. Yohana na Polycarp waliishi pamoja kwa miaka mingi.


Isaiah na kwenye moja ya maono akifananishwa na BUNDI ila king james version original inamuita LILITH..... Hivyo si kweli kuwa kwenye biblia hajatajwa.
Mkuu binafsi nimesoma kitabu chote cha ISAYA na mahali unaposema anamzungumzia Lilith na kumfananisha na Bundi au zimwi siyo kweli kabisa. Pale ISAYA alikuwa anazungumzui kitu kingine tofauti kabisa na wala siyo huyo Lilith mnayemsema ninyi. Isaya 34:14-17, hapa tunaona Isaya anamzungumzia "Satyr". Maana ya Satyr kutoka lugha ya kiingereza ni "mwanaume mwenye matamanio ya kingono" na siyo mwanamke.

Kama nilivyosema hapo mwanzo, shetani amekuwa akitunga mambo mengi sana ya uongo ili kuwapotosha watu. Na maandiko haya yenye kupotosha hayakuandikwa leo, yaliandikwa zamani sana za kale enzi za akina Nuhu hasa baada ya Nimrod kuijenga Babeli. Pale Babeli ndipo maandiko mengi sana ya kipagani yalipoanzia na kuenea dunia nzima. Vitabu hivi au maandiko haya yenye hadithi za uongo kanisa katoliki walitaka kuviweka kwenye BIBLIA, lakini Watakatifu wa wakati ule wakiongozwa na ROHO MTAKATIFU wakakataa kata kata.

Leo hii kanisa katoliki linavyo vitabu hivi(pseudepigrapha) na linavitumia katika mafundisho yake, mfano mzuri ni kitabu cha Injili ya Thomas(gospel of Thomas), Book of the Maccabees n.k.
 
Eti ni kama jina la LUCY nasikia wazungu waliompenda shetani walikuwa wanafupisha jina la lucifer wanawaita watoto wao LUCY nasisi eti tunageza......
Maana hata hawa wanamuziki now bado wanamfupisha wanamuita Lucy kama kendrik lamar ana nyimbo kabisa inaitwa LUCY na anasema maana yake ni lucifer.....Ati ni kweli??
 
SAWA LILITH ALIKUJA KWA UMBO LA NYOKA NA KUMDANGANYA HAWA... HII INAMAANISHA MWANZO HAKUWA KATIKA UMBO LA NYOKA... LAKINI BAADA YA KUSABABISHA USALITI KATI YA MUNGU NA ADAMU AKAPEWA LAANA YA KUTEMBEA KWA TUMBO MAISHA YAKE YOTE...

JE INAMAANA ALISHINDWA KURUDI KATIKA UMBO LAKE LA AWALI KABLA HAJAJA KATIKA UMBO LA NYOKA BAADA YA KUMALIZA KAZI YAKE...???

JE MUNGU NDIYE ALIYEMFANYA KUWA KATIKA UMBO LA NYOKA KWA MAISHA YA KUDUMU BAADA YA KUMKOSEA MUNGU...???
Paragraph ya mwisho inaweza kuwa ndio jibu sahihi
 
Kama lilith waliumbwa siku moja na adamu basi lazima walilingana nguvu na uwezo na pengine adamu akazidi kidogo za lilith maana adamu aliambiwa kuwatawala. Kinachoua hii hoja ni Lilith anatoa wapi uwezo wa kujigeuza nyoka ili hali adamu hana? Lilith ndie ibilisi adamu alikufa lini na lilith bado yupo? sasa hii ina maana gani alieasi wa kwanza anaishi hadi leo aliedanganywa kafa kitambo sana kwanini Mungu amuache huyu muasi aliegoma kuishi na mmewe na badala yake muue mapema aliekosea mara moja tu tena kwa kudanganywa na huyohuyo ibilisi? ok turudi nyuma wote walioumbwa na Mungu wanaambia wakila matunda hakika watakufa kwanini lilith yeye hafi je alimzidi maarifa muumba wake? hii story inakosa uhalisia.
Kwanza kuna points nyingi muhimu umeziruka inawezekana ni kutokana na uhalisia
Soma tena uone asili ya Lilith/ibilisi..
Pia angalia uone hakuna panaposema ibilisi alikula tunda
Zaidi ni kwamba nimeandika kuwa tayari lilith alishageuka roho ya kuzimu na roho haifi
 
Hayo nimawazo ya watu tena potofu nimesoma PhD ya Theology na nmesoma pia Missiology hamna vitu kama hivyo its better kutoendelea kusambaza uongo huu kwa wengine
Hongera kwa kusoma na kufikia level hizo.. Inategemea na taasisi iliyokupa hizo awards, kama ina mlengo wa kuamini kipi... Inawezekana tunachojadili kikawa kipya huko kwenye PhD na degree za kwenu
 
Kitabu gani kimeandika hii kitu ya lol lilith??.. Na sisi tukipitie.....

Nachofahamu Adam alikua first man, na alikua first man sababu alikua mmoja wa Malaika MBINGUNI aliyeongoza mapambano Kati ya lucifer na Mungu kule MBINGUNI tunaiita (Pre-mortal) life... Award yake akapewa aje Duniani aanzishe mankind...... Sasa huyu lilith hata kwenye Pre-mortal life hakuwepo.

Tunajua waliokua kwenye Maisha kabla Dunia haijaumbwa ambao walikua mashuhuri kule kwa kazi zao. Baadhi Yao ni

JESUS CHRIST - JEHOVAH
MICHAEL - ADAM
GABRIEL - NOAH
LUCIFER - SATAN/DEVIL

Na wengine wengi.

Jina la kushoto ni Pre-mortal name, jina la kulia ni Mortal (earth) name.. Mfano YESU KRISTO kwenye pre earth alikua anaitwa JEHOVAH.

Sasa huyu lilith hatujui alikua Nani kule na aliletwa kwa mission gani Dunian maana Adam, eve na wengine walioanzisha Dunia kama viumbe wa kwanza walikua wana kazi ya kufanya.
Umepata wapi hii.?
 
Hongera kwa kusoma na kufikia level hizo.. Inategemea na taasisi iliyokupa hizo awards, kama ina mlengo wa kuamini kipi... Inawezekana tunachojadili kikawa kipya huko kwenye PhD na degree za kwenu
Kuna kitu kinaitwa Missiology sio kila chuo kinatoa hii nminahusu vitu vilivyofichwa kwenye Bible na huwezi kuvipata kwenye Theology ndio maana inaitwa Missiology humo utakutana na kitabu cha Henoch kunamambo mengi mno
 
Kwani ni vigumu sana kuamini Mungu bila kuwa na simulizi kama hizi..!?

Kitabu kinajaribu kueleza kwa wepesi tu tena bila mushkeli na kutanabaisha kufikia mioyo ya Vitoto_katika utambuzi wa nguvu mbili kinzani (yin & yang)

Ili kuwajenga viumbe kuwa na welewa na utambuzi katika utendaji wazo na kuzitumia kufikia ukomavu

Lakini bado madoido ya ushehereshaji hayaishi

Utengenezaji wa taarifa nyingi siku zote huandaa ugumu wa upatikanaji wa taarifa sahihi kwa kizazi kijacho

Nachelea tu msije wataabisha watoto wachanga Mkaja kuvuna hesabu yake_karma haidanganyi
 
Mkuu naheshimu mawazo yako lakini kwanini unaamini kila kitu lazima kiandikwe kwenye biblia ndio kiwe cha kweli?? Kumbuka biblia ni compilation tuya vitabu iliyofanywa na wazungu wachache pale constantinople na baadae alexandria yaani katika vitabu 400+ vilichukuliwa 66-72 pekee sasa inakuwaje useme biblia haijaandika?? Kwanni usiseme biblia iliandika ila watu wachache walivitoa???

Anyway habari za lilith zimeandikwa kwenye pseudipigraphi nyingi tu na kwenye biblia ameandikwa kwenye kitabu cha Isaiah na kwenye moja ya maono akifananishwa na BUNDI ila king james version original inamuita LILITH..... Hivyo si kweli kuwa kwenye biblia hajatajwa.

Ni hayo tu mkuu Karibu for clarification huenda sijakuelewa tu....
Hakuna mahali Lilith anatajwa kwa BiBlia. Its a Demon coupled with a demon akimuacha Adam na hii story haipo kwa Bible.
 
Mkuu hii ni hadithi ya kufikirika tu, kwanza kumbuka Adamu hakuzaliwa bali aliumbwa kutoka kwenye udongo. Kama MUNGU alimuumba huyo Lilith kabla ya Eva, basi ingeandikwa kwenye Biblia wala isingefichwa.

Biblia inasema KWELI na wala haidanganyi. Kilichoandikwa kwenye Biblia ni kweli tupu. Shetani anapenda sana uongo na ndiyo maana amekuwa akija na hadithi nyingi za kutunga za uongo kama hii ya kwako ili awapotoshe Wanadamu wauamini uongo kuliko KWELI ya NENO la MUNGU.
Unaamini kabla ya Adamu kulikuw na watu wanaishi?!

Je waamori walikuwa zama gani kabla ya Adamu au baada ya Adamu?!

Biblia haisemi kila kitu,Biblia ni maungano ya machache kati ya mengi yaliotukia katika ulimwengu huu na bado biblia imetumiwa kubeba matabaka uyaonayo katika ulimwengu huu
Si Quran ama Biblia iliokamilika hivyo maarifa mengine ya kumjua mungu na harakati zake za kuwafanya wanadamu wamjue yakupasa kuyajua mengi ili umfuate yeye alie mkuu achana na propaganda za kuingiza siku za jua katika utawala wa Mungu.

Eg. Christmas,Pasaka,Idd...........
 
Hayo nimawazo ya watu tena potofu nimesoma PhD ya Theology na nmesoma pia Missiology hamna vitu kama hivyo its better kutoendelea kusambaza uongo huu kwa wengine
Kusoma na kuelewa ni vitu viwili tofauti kabisa jumlisha uwezo wa kutafsiri na nia ya kutafuta maarifa ya ziada nje ya kile ulichosomea kwa maana ya kufaulu na kupata daraja fulani
 
Back
Top Bottom