Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Mkuu kabla ya mkutano mkuu wa Constantinople kufanyika fahamu kwamba tayari kuna watu walikuwa na vitabu vilivyokubaliwa kama maandiko matakatifu, na ndiyo hiyo tunaiita Biblia leo hii.Kumbuka biblia ni compilation tuya vitabu iliyofanywa na wazungu wachache pale constantinople na baadae alexandria yaani katika vitabu 400+ vilichukuliwa 66-72 pekee sasa inakuwaje useme biblia haijaandika??
Mfano mzuri ni "Polycarp of Smyrna", huyu na kanisa la MUNGU tayari walikuwa na maandiko haya kabla hata ya kanisa la Rumi katika karne ya 1. Polycarp alikuwa ni mwanafunzi wa Yohana yule aliyeandika kitabu cha Ufunuo. Yohana na Polycarp waliishi pamoja kwa miaka mingi.
Mkuu binafsi nimesoma kitabu chote cha ISAYA na mahali unaposema anamzungumzia Lilith na kumfananisha na Bundi au zimwi siyo kweli kabisa. Pale ISAYA alikuwa anazungumzui kitu kingine tofauti kabisa na wala siyo huyo Lilith mnayemsema ninyi. Isaya 34:14-17, hapa tunaona Isaya anamzungumzia "Satyr". Maana ya Satyr kutoka lugha ya kiingereza ni "mwanaume mwenye matamanio ya kingono" na siyo mwanamke.Isaiah na kwenye moja ya maono akifananishwa na BUNDI ila king james version original inamuita LILITH..... Hivyo si kweli kuwa kwenye biblia hajatajwa.
Kama nilivyosema hapo mwanzo, shetani amekuwa akitunga mambo mengi sana ya uongo ili kuwapotosha watu. Na maandiko haya yenye kupotosha hayakuandikwa leo, yaliandikwa zamani sana za kale enzi za akina Nuhu hasa baada ya Nimrod kuijenga Babeli. Pale Babeli ndipo maandiko mengi sana ya kipagani yalipoanzia na kuenea dunia nzima. Vitabu hivi au maandiko haya yenye hadithi za uongo kanisa katoliki walitaka kuviweka kwenye BIBLIA, lakini Watakatifu wa wakati ule wakiongozwa na ROHO MTAKATIFU wakakataa kata kata.
Leo hii kanisa katoliki linavyo vitabu hivi(pseudepigrapha) na linavitumia katika mafundisho yake, mfano mzuri ni kitabu cha Injili ya Thomas(gospel of Thomas), Book of the Maccabees n.k.