Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

.Malaika ndio hawana Jinsia.hawazaani.na huwa hawali chakula...ila majini yana jinsia ndio maana tunayo jini mahaba.na pia majini hula chakula.ndio maana kafara za damu zipo kwa washirikina.
ila wapo majini wema hilo usisahau..
Uko vizuri
 
Inasikitisha sana...

Kusalitiwa kubaya sana... Unamtolea mtu laana ya vizazi na vizazi...

cc: mahondaw
 
Nadhani kuna maana kamili nyuma ya Biblia takatifu kwa kuchagua vya kuandika
Hapa nakuelewa sana. [Yapo mambo mengi ambayo hayakuandikwa kwenye Biblia kama yangeandikwa kusingetosha kwa wingi wake] unajua mshana jr, haya mambo ya ufukunyuzi yanaleta maswali mengi sana hasa kwa sababu mengi hayatoi habari kamili.

Inahitaji ufahamu wa juu sana kuyachunguza mambo na pia yanahitaji muda mrefu sana kuyang'amua. Yaani ni vizazi na vizazi. Elimu ya kiroho ni pana mno!! Huenda mengine yameondolewa kwa maslahi fulani kama unavyosema sababu mengine hayaonekani kuwa na faida sana kwa mwanadamu ukizingatia hali halisi ya uovu unaoendelea kuongezeka
 
Kunavyo vitabu vingi saana! Zaidi hata ya hivyo 72. Vipo vingi saana! Vingine hata bado hawajaviweka hadharani
 
Inaelekea "kipochi manyoja" kilikua cha ubora wa hali ya juu kabisa... Salaleeee[emoji23] [emoji23]
Suala la kuingiliana kimwili ni zaidi ya hisia na kufurahia tendo kama ilivyo kwa wengi wetu. Kuna maana kubwa sana iliyolengwa katika mkutaniko huo ambayo inahitaji ufahamu wa juu sana kuendelea kutambua mambo yanayohusisha tendo la kujamiiana kwa wanadamu.

Mshana nadhani unanielewa zaidi kwa maelezo haya mafupi.
 
Hapa kuna mkanganyiko sana, japo kuwa huwa najiuliza maswali ya ziada huenda ikawa ni namna tu ya mitindo wa mwandishi.

Maana waandishi wengine cha nyuma anatanguliza mbele au katikati kisha anakielezea kwa ufasaha ili msomaji ujue kwamba hiki ni kisa cha nyuma ila kimewekwa kama kidokezo.
 
Mtaijua Kweli na hiyo Kweli itawaweka huru.
 
.Malaika ndio hawana Jinsia.hawazaani.na huwa hawali chakula...ila majini yana jinsia ndio maana tunayo jini mahaba.na pia majini hula chakula.ndio maana kafara za damu zipo kwa washirikina.
ila wapo majini wema hilo usisahau..
Mhm hapa napo sijaelewa labda, majini wema? Ndiyo kama wepi hao mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…