Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Hahahahaha!! Wanawaseti wafuasi wa baadae.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kwa nyongeza hii... Kuna kitu cha ziada nimeongeza hapa kuhusu huu ufunuo usiosemwa kati ya Lilith na Adam... Kuna sababu za msingi sana pengine ni kwanini Bible haikumtaja huyu bibie... Tuendelee kuchambua tutaipata ukweli hatimaye

Jr[emoji769]
 
The Divine resolution to bestow a companion on Adam met the wishes of man, who had been overcome by a feeling of isolation when the animals came to him in pairs to be named. To banish his loneliness, Lilith was first given to Adam as wife. Like him she had been created out of the dust of the ground. [emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144]

Jr[emoji769]
 
Ni ngumu sana kuielewa dunia kwa sababu siri zipo kwenye maandishi na maandishi yamefichwa
Ni kweli na hasa ukitafuta kwa mwelekeo wa kwenda nje yako. Muda hautoshi na vitu ni vingi sana. Lakini pia wewe Ndio ufunguo wa yote bila uwepo wako hakuna dunia, kila ulionalo ni kimvuli Cha uhalisia ndani yako wewe, badili mwelekeo la sivyo hadithi za vitabuni zitakuchanganya tuu.
 
Ni sawa na wewe jini mahaba akujie usiku umpakue usiku kucha,,utawaambia watu una mke?? Mungu kama ana mpango na wewe ataruhusu jini mchafu alale na wewe umpakue??

Kinachonikera ni wewe Kusema eti shetani mchafu analala na Adam?? Haiwezekani,,,Mungu anaonana na Adam kila jioni aruhusu uchafu mtupu uje kulala na Adam???

Kama kutakuwa na ukweli kwenye hii riwaya nitakuwa na mashaka makubwa na Mungu?? Na ni bora nisiwe na imani?

Wewe una mpango binti yako awe na maisha mazuri ya ndoa,,ukute kuna mtu wake special keshamposa,,,utaruhusu wahuni wamkaribie??

Unapomtaja lilith unaondoa uwezo,uangalizi,,maana na upendo wa Mungu.
Tafuta maarifa uelimike

Jr[emoji769]
 
Maneno ya Mungu yanasema kwakuwa wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.... Hapa wanajumuishwa Adam na hawa pia
 
Hata wa piga punyeto pia Lilith ana fanya yake,
 
Ngoja na mimi nichangie kidogo.
Kwanza hiyo Isaya 34:14 inasema
" Pakamwitu na fisi watakuwa humo, majini yataitana humo, kwao usiku utakuwa mwanga, na humo watapata mahali la kupumzika"

Hapa unaunga unga issue ya huyo lilith kivipi?
 
Lilith anayesemekana ni mke wa kwanza wa Adam... Hatajwi popote kwenye Biblia takatifu zaidi ya kwenye kitabu cha Isaya 34 : 14, na ambapo hata hivyo kutajwa kwake hakuna mahusiano kabisa na Adam

Achilia mbali hiyo Isaya 34:14 ambayo nimeomba unielekeze namna lilith alivyotajwa hapo.
Nini kinakufanya uendelee kuquote mistari ya kwenye biblia wakati unajenga hoja zako za lilith wakati umeishasema hapa kwamba hakuna sehemu ingine kwenye biblia ametajwa zaidi ya kwenye hiyo Isaya 34:14.?
 
Na hapa, wewe mwenyewe unasema huyu lilith habari zake ziko nje ya biblia, sasa narudia swali? ni kwa nini umequote mistari ya kwenye biblia katika ujengaji wa hoja zako?
 
Muanzisha mada amesema nje ya Biblia kwa ujumla, lakini baadae kaanza kuzungumzia biblia za kiebrania, lakini pia amekuwa akitaja juu ya masimulizi ya kiyahudi huku akiquote mistari fulani ambayo kwa sasa ntaiita ya biblia, kama mwanzo 1:27 na mwanzo 2:22

sasa sielewi maana yake ni nini
 
Bwana Mshana Jr naomba nikujirishe kwamba wewe ni mmoja ya watu ambao nawatambua kuwa na huelewa mdogo sana juu ya maandiko ya kwenye Biblia, kuanzia namna biblia imeandikwa mpaka maana ya maandiko yenyewe.

Kwa kuanzia, naomba nikuonyeshe mapungu ya uelewa wako yalivyosababisha kutumia mistari ya mwanzo 1:27 na mwanzo 2:22 kwa namna ulivyoitumia kwenye maelezo yako.

Kwanza, Biblia inajieleza namna ilivyoandikwa, namaanisha, Mungu ameeleza alivyoiandika Biblia. hajaiandika kama vitabu vyetu hivi ambavyo vinalielezea jambo moja kuanzia mwanzo mpaka mwisho, yaani ukichukua chapter ya logarith unaisoma logarith na kupata maelezo yake yote, ukienda chapter ingine unaanza probability. NO.

mambo yote kwenye biblia yameelezewa kwa mafungu mafungu, unakuta kuna kilichoandikwa kwenye kitabu cha mwanzo juu ya jambo fulani ni mwisho wa maelezo wa jimbo hilo, mwanzo wa maelezo uko kitabu cha warumi, na kiunganishi kiko kitabu cha mambo ya walawi.

Ama kwenye sura hiyo hiyo moja, mstari wa 2 unamaelezo ya mwisho, ya mwanzo yako mstari wa 17, n.k hivyo basi, biblia inapozungumzia jambo moja mara nyingi haimaanishi kwamba mambo hayo yanatofauti, kama ulivyoforce wewe kwamba uumbaji wa kwenye mwanzo 1:27 ni tofauti na ule wa kwenye mwanzo 2:22.

maelezo hayo hapo juu, ni tafsiri kutoka hapa ISAYA 28: 9-10
"Atamfundisha nani maarifa? Atamfahamisha nani habari hii? Je! Ni wale walioachishwa maziwa, walioondolewa matitini? Kwa maana ni amri juu ya amri, amri juu ya amri; kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo. "

Katika muktadha huu,
Mwanzo 2: 7 "Mungu anamuumba Mwaadamu
"Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai."

Mwanzo 2: 18 " Mungu anamaanisha katika Mwanzo 2:27 alikuwa amemuumba Adamu tu
"Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Mwanzo 2:21-22 (Inaelezea namna alivyomuumba Hawa)"
Bwana Mungu akamletea Adamu usingizi mzito, naye akalala; kisha akatwaa ubavu wake mmoja, akafunika nyama mahali pake, na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu."

Mwanzo 2:23 Adamu anatambua ujio wa Bi Hawa
Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume.

Mwanzo 1;27 " Inasummarize uumbaji wa Mwanaadamu, adamu ha Hawa.

"Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba."


Natambua kwamba kilichokuchanganya hitimisho la yaliyofanywa kwenye kitabu cha mwanzo 2, kuwekwa kwenye kitabu cha mwanzo 1

Ama sivyo.
Hakuna sehemu Adamu wala Mungu kuwa recorded kuwa uncorfortable na mwanamke yeyote hata kupelekea uumbaji wa Hawa
 
Na hapa, wewe mwenyewe unasema huyu lilith habari zake ziko nje ya biblia, sasa narudia swali? ni kwa nini umequote mistari ya kwenye biblia katika ujengaji wa hoja zako?
Naona una tatizo la kuelewa lugha.. Nimesema kuna SIMULIZI NYINGI sijasema kuna SIMULIZI ZOTE NJE YA BIBLE
 
Nashindwa kukuelewa maana yako fuatilia post yote na replies zangu nimejibu hoja zote to the best of my knowledge
 
Bwana Mshana Jr naomba nikujirishe kwamba wewe ni mmoja ya watu ambao nawatambua kuwa na huelewa mdogo sana juu ya maandiko ya kwenye Biblia, kuanzia namna biblia imeandikwa mpaka maana ya maandiko yenyewe.

Bwana Volatility naomba kwanza rekebisha lugha yako hapo juu
- nikujirishe... Nikujulishe
-huelewa... Uelewa
Huo mtazamo wako mwingine kunihusu mimi na Bible sina tatizo nao kwakuwa ni mtazamo binafsi.. Japo haumaanishi kuwa ndio uhalisia
Kingine ni kwamba ukitaka upanue bongo yako na kupata maarifa mengi zaidi usiishie kusoma Bible tu hasa hizi version tunazoletewa.... Kuna Bible nyingi kwa taarifa yako na zina mambo mengi ambayo hayakuandikwa kwenye Bible hii tunayoitumia sisi
 
Noted. Ila Biblia ni moja tu japo uchakachuaji ni mwingi lakini ni rahisi sana kuchambua pumba na mchele, kama nilivyochambua hapo juu.
 
Noted. Ila Biblia ni moja tu japo uchakachuaji ni mwingi lakini ni rahisi sana kuchambua pumba na mchele, kama nilivyochambua hapo juu.
Sasa nikwambie kitu hii ya sasa ndio imechakachuliwa hasa.. Ngoja kuna moja nitakutafutia edition yake ulingalishe uone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…