I see! Nilikuwa sijawahi ckia hizo habari za shost ake na Hawa... ngoja nami niingie online library nimbukue kidogo!!
Sema dah, mara malkia wa giza, mara malkia wa jehanamu, mara Lilith hivi; mara Lilith vile... yaani makombora yote hayo anayopigwa kisa tu kv kamtema Adam!
Hivi huyu Adam nae si ni miongoni mwa wateule wa Mungu; au?! Kama ndivyo, huku Uswahilini si huwa tunaambiana eti mke mwema hutoka kwa Mungu; au?
Kama ndivyo, how come tena mteule wa Mungu akapata mke asiye na sifa za kutoka kwa Mungu?!
Kama mke mwema hutoka kwa Mungu; mke muovu si itakuwa hutoka kwa shetani; au?
Kama ndivyo, ina maana mteule wa Mungu aliletewa mzigo na shetani?!
Oh! Nasikia Mungu aliumba dunia kwa cku 6 na cku ya 7 akaamua kula good time! Nimepatia?!
Kama ndivyo, au inawezekana Shetani alimlia timing Mungu, na ilipofika cku nyingine Jamaa akawa anakula good time; shetani akaupenyeza mzigo kwa Mwana Mteule!!
Au hii good time alikula mara moja tu?!
Hebu ngoja, kabla sijaendelea!! Hivi ukifukunyua fukunyua mara oh, mbona kama hivi ipo vile, mara oh, kama ndivyo mbona iko hivi... hapa vipi; naweza kupata dhambi?!
Nakumbuka enzi hizo tuko Madras Hidayat Kurasini; Ustaadhi alikuwa anatuambia ukitaka kufahamu balaa la moto wa jahanamu; ziba masikio yote mawili kwa viganja vya mikono usikie moto wa jahanamu unavyounguruma!!
Basi ukitoka hapo, hata ukikutana na braza wa Std VII lazima umpe shikamoo ili usije ukakumbana na lijimoto la jahanamu ambalo umelisikia "Live!"
Mungu anakuona Ustaadhi wangu, yaani bila huruma unavilisha matango pori vitoto vidogo!