Wewe siyo wa kwanza kusema hakuna MUNGU, kabla yako wewe walikuwepo watu wenye nguvu, watu maarufu, wafalme waliotawala dunia kama akina Nebukadreza, ambao walisimama na kutangaza mbele ya maelfu ya watu kuwa hakuna MUNGU. Hivyo siyo ajabu leo hii wewe ukisema hakuna MUNGU sababu huna jipya.
Lakini fahamu kwamba huyu Nebukadreza alipouona "mkono" wa MUNGU, yeye mwenyewe alijirudi na kusema hakika yupo BWANA MUNGU na hakuna wa kufanana na YEYE! Hata wewe ipo siku utauona utukufu wa MUNGU na hapo ndipo utapiga magoti na kusujudu, lakini utakuwa umechelewa sana.