Ugali ni chakula adimu katika sherehe, sababu ni nini?

Ugali ni chakula adimu katika sherehe, sababu ni nini?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Ugali ni chakula tunachokula kila siku, iwe ugali wa mahindi, wa mihogo, mtama au uwezo. Hiki ni chakula tunachokimudu watu wengi, hata ukikosa mboga nyanya, kitunguu, ndimu, pilipili na chumvi kidogo vitakusaidia kumaliza portion ya ugali.

Chakula kinacholiwa na wengi kuadimika katika sherehe, sifahamu inawezekana vipi. Sherehe nyingi unakuta pilau, biriani, ndizi, viazi, pasta nk, lakini si ugali.

Kama ni mechanism ya ulaji wa ugali, tunaweza kuweka huduma ya watu kunawa mikono katika sherehe ili waweze kukata matonge kwa mikono. Kuna wanaoweza kula ugali na kisu na umma.


1638964918508.jpeg
 
Hapa ndio kamati ya vinywaji na chakula zinapofail hasa ukute sherehe ina maji mengi, Mimi personally napenda ugali hasa wenye mchanganyiko wa dona, ngano, mtama na muhogo hapo ni hatari sana kuna mboga mlenda, dagaa au nyama choma.
 
ni kwasababu jamii ya kitz ina amini ugali ni chakula cha watu fukara. hakifai kuwepo kwenye dhifa mbalimbali.

na mimi naungana na wanao amini hivyo.ni ukweli, ugali ni chakula cha mafukara, period
 
ni kwasababu jamii ya kitz ina amini ugali ni chakula cha watu fukara. hakifai kuwepo kwenye dhifa mbalimbali.

na mimi naungana na wanao amini hivyo.ni kweli ugali ni chakula cha mafukara, period
Ninadhani ni kwasababu hatujawahi kukosa kabisa chakula. Kuna watu hawali utumbo kwakua una harufu. Utumbo ukitengenezwa roast kama ile ya maini unapendeza sana.
 
Back
Top Bottom