Ugali ni chakula adimu katika sherehe, sababu ni nini?

Ugali ni chakula adimu katika sherehe, sababu ni nini?

Unaanzaje kusonga ugali wa watu kuanzia 100. Ni kazi sana jamani
 
Unapenda chips kiepe?
Sijamaanisha hivyo mkuu, mbadala was ugari unajulukana kuwa ni ubwabwa so nitakula ubwabwa tu endapo nakula basic food.

Na kipindi nasoma chuo sijawai kununua ugari hata siku moja ilikuwa nikienda chuo kula ugari mpaka likizo.

Pia hizokiepe yai ulichosema nakula sana nisuala la pesa tu nakumbuka first year kipindi Cha ramadhani nilkula daku Chips yai mwezi mzima.

Mimi ni mtu naishi maisha yangu ya moyo wangu na watanzania wanakariri ujinga gani sijui.
 
Ugali ni chakula tunachokula kila siku, iwe ugali wa mahindi, wa mihogo, mtama au uwezo. Hiki ni chakula tunachokimudu watu wengi, hata ukikosa mboga nyanya, kitunguu, ndimu, pilipili na chumvi kidogo vitakusaidia kumaliza portion ya ugali.

Chakula kinacholiwa na wengi kuadimika katika sherehe, sifahamu inawezekana vipi. Sherehe nyingi unakuta pilau, biriani, ndizi, viazi, pasta nk, lakini si ugali.

Kama ni mechanism ya ulaji wa ugali, tunaweza kuweka huduma ya watu kunawa mikono katika sherehe ili waweze kukata matonge kwa mikono. Kuna wanaoweza kula ugali na kisu na umma.


View attachment 2037155
Wameuzoea

FB_IMG_16388205907526573.jpg
 
Ugali umezoeleka ni chakula cha mchana
Sherehe nyingi ni usiku

Ugali pia unachagua mboga...
Usiku ushakuta samaki wa nazi kwenye sherehe?!

Ama unataka ule ugali njegere😀?.
 
Ugali umezoeleka ni chakula cha mchana
Sherehe nyingi ni usiku

Ugali pia unachagua mboga...
Usiku ushakuta samaki wa nazi kwenye sherehe?!

Ama unataka ule ugali njegere😀?.
Kukiwa na ugali tutapika bamia na nyanya chungu, msusa, kisamvu na nkhoko.
 
Kwani shule za bweni tulikuwa tunasongewaje!!!...ugali hata wa watu buku unasongwa tu...suala ni watu wako tayari kula ugali??? Jela ugali unasongwa hata wa watu 2000
Huko jela na shule unasongwa mradi ugali tu, sio ule ugali uliosongwa ukasongeka ugali mzuri usio na mabuja mabuja. Ugali unaupishi wake mkuu .
 
Ugali umezoeleka ni chakula cha mchana
Sherehe nyingi ni usiku

Ugali pia unachagua mboga...
Usiku ushakuta samaki wa nazi kwenye sherehe?!

Ama unataka ule ugali njegere😀?.
Ugali mlenda wa karanga, upate na visamaki na kulumangia na kchumbali hatarii.
 
Back
Top Bottom