Ugali umetukuza usidharauliwe na mtu yeyote

Kula Dona mkuu utanishukuru, sio chakula cha Nguruwe
Dona, mahindi ya kuchemsha, kuchoma, makande yasiyokobolewa ndio chakula cha mahindi kwe mtu mwenye ubongo unaofanya kazi vizuri.
 
ugali ni chakula cha ng'ombe na nguruwe ujuaji wa kiafrika ukatufanya tubadili kua mlo wa binadamu , hapo zamani hakujawahi kuwepo mahindi afrika

KAZI NI KIPIMO CHA UTU
Nguruwe na Ng'ombe wanakula Ndizi, Viazi na Mihogo hapo utasemaje nyinyi mnaokula Ndizi mna utofauti gani na Nguruwe?
 
Wanyakyusa inategemea wa wapi kyela_Wali,Tukuyu, Ndizi na ugali,Busokelo_Ugali,ndizi,wali kwa mbaali,usafwani na wandali,wamalila ugali kwa sana!
 
Kuna Member moja humu kasema kuna Matapeli wengi kuhusu ulaji wa Ugali. Nami nakubaliana naye. Ugali ni step food ya familia nyingi. Pamoja na changamoto zake za vitamins kama zipo tuache huu utapeli wa kwamba siyo chakula.. ni kufuru kwa baadhi ya familia.
 
Ugali ndio chakula chetu,hasa kule boarding school tumekula sana na Maharage,hatukuwahi sikia mtu anautapiamlo!
 
Ukweli nakula ugali, hawo vijana wa Dar es Salaam ndio wana mikele, huku ushirombo ni nguma kwenda mbele
 
Ni kufuru sio kidogo mkuu, watu tumekua na Ugali mtu anakuja anaanza kuukashfu ovyo ovyo na hapo hapo anasema amewahi kuula inamaana huo huo Ugali na yeye umemkuza mpaka alipofikia leo hii kashika tushilling twa kubadirisha mboga basi anaanza kuutusi na kuudharau Ugali, how come?
 
Hayaz na ugali wapi na wapi?Ninyi uji wa ndizi/matoke kwa senene tu.Mkishiba mnacheza chenkura halafu mnatulia mkitafuna buni zilizokaangwa.
Ahaaa ! Mimi nimekula Sana hiyo kitu Mkuu kwakuwa mm Bukoba napotoka ni mjini life is expensive ndizi tulikuwa tunakula mara moja moja Sana bei yake ilikuwa juu by that time.
 
Kwa masikini wengi ugali ni mkombozi, pia mashuleni na magereza ugali ndio chakula kikuu.
 
Dona, mahindi ya kuchemsha, kuchoma, makande yasiyokobolewa ndio chakula cha mahindi kwe mtu mwenye ubongo unaofanya kazi vizuri.
Tatizo kubwa la watu kuona ugali ni chakula cha kimaskini ni kwa sababu sisi waafrika huwa tunataja vyakula kitofauti. Wazungu wanaanza na ''chicken or beef..... nk na wanathamini zaidi ile sisi tunaita ni ''mboga ya kusindikizia''. Sisi utakuta hawa wali unakuwa mwingi na ''kisindikizio (mboga)'' kidogo, wakati wao wali unakuwa kama kisindikizio tu.
 
Kwa Afrika ukisikia nchi yoyote ina njaa maana yake hakuna mahindi ya kutosha na msaada utaletwa mahindi/unga na maharage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…