Kabla sijakuuliza maswali Mengi...
Kwanza Hongera kwa POST NZURI...
Pili..hiyo sumu unajua inakaa muda gani kwenye mahindi?
Tatu Kwani ni mahindi yooote yanawekewa hiyo Dawa,all sources?
Nne yaani hiyo dawa inakaa kwenye Kiini tuuuuu?
Tano Je ni madawa yote kwa mimea ni hatari? mbona binadamu tunatumia "Superflaxon"
Sita...ni Kiwango gani ndo kinadhuru?
Ahsante Mkuu
monaco;
Hujaniuliza mimi maswali yako ila nataka tu kukujibu kwa sababu wengi wamevamia kwa kebehi uzi huu. Kwa sababu wanazo zijua wenyewe, wanataka kujitoa ufahamu. Ati, kwa sababu hatujamwona mtu akifa kwa sababu tu ya kula ugali dona basi hiyo sumu haipo. Naomba niseme yafuatayo:
Sumu hii huingia kwenye mahindi yalio vunda kidogo haswa wakati wa uvunaji. Ukiyahifadhi yakiwa na unyevu usio sahihi. Sasa, kwa kuwa wengi tunakula kwa mama lishe, wale ni watafutaji. Akikuta mahali bei imepungua kwa senti kidogo tu anauchukua kwa wingi ili aongeze faida yake.
Kumbuka, mahindi hayo yakianikwa huondoa ule uvundo na kuwa mazuri tu ila rangi inakuwa ya chungwa (yellow). Ukisaga, tiyari unga unakuwa mweupe. Haya, yalitakiwa yakobolewe kuondoa kile kiini.
Pumba ya mahindi ka hayo, huua mifugo (Kitimoto) haraka kuliko mara moja. Wataalam wa kilimo na mifugo njooni saidia hili.
Hatusemi ni yoote huua ila nikienda kununua pumba, nikiikuta ni yellow huwa naipita kwa mbaali. Si lazima huyo mdudu awepo lakini, mara nyingi sana ndiyo inakuwa hivyo.
Kama ni dona, nakula nilo tengeneza mwenyewe.
Wadudu "scania" alipoingia hapa nchini, watu wengi walitumia sumu mbalimbali kuzuia wadudu wale. Je, ni wangapi waliamini kuwa zile sumu zilileta saratani?? Watz kwa ubishi, hatujambo