Naamini wewe siyo kati ya wale waliohusisha kipindupindu na uchaguzi, ati mbinu za CCM watu wasikusanyike.
Nimezungumzia afya zetu kwa kudokeza uwezekano wa kutumia dona iliyo na sumu. Chakula chochote kisipotayarishwa vizuri kinakuwa sumu. Hatuhitaji takwimu kuthibitisha hilo, ila mfano ni mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kama vile kipindupindu.
Ukweli ni kwamba "fungus" huzalisha hiyo sumu ya "aflatoxin" ambayo huleta kansa. Na Vyakula vya nafaka, na vinginevyo vikivunda ni hazina ya "fungus".
Kwamba umekua ukila ugali wa dona, uendelee kufanya hivyo, ni heri kwako. Kumbuka tu mazingira ya sasa hivi siyo salama kamwe. Nenda Ocean Road Hospital uone wagonjwa wa kansa - aina mbalimbali ikiwamo magonjwa ya ngozi.
TAFAKARI CHUKUA HATUA