Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Vijijini ndo vyakula vyao na wamevitumia enzi na enzi kama ni kweli wengi wangekuwa wameshakufa
 
Tangu enzi na enzi vijijin hakuna kukoboa...wewe acha uzushi wako..kila kitu siku hizi mnatudanganya ooh cancer ooh side effect..aah basi bana wacha tufe..wewe unataka tule machips ili tukose afya tuwe dororo
 
Ni kweli ila ni mahindi yaliooza yenye ukungu Fulani lakini ukichukua mahindi safi hayana shida na sio mahindi mpaka karanga
 
Ni kweli ila ni mahindi yaliooza yenye ukungu Fulani lakini ukichukua mahindi safi hayana shida na sio mahindi mpaka karanga
Ni kweli ukiandaa vizuri mahindi yako uwezekano wa kuondoa chanzo cha "fungus" ni mkubwa. Ila wengi tumevamia ugali wa dona na kununua unga ambao hatujui matayarisho yake.

Vijijini miaka yote wanakula dona iliyotayarisha na wenyewe kwa uangalifu ama kwa kujua au kutokujua. Lakini dona ya biashara, tunayonunua maduksni sina uhakikana usalama wake
 
Devil you are a liar go away from me.
 
Nitaleta mrejesho maana hicho ndio chakula changu.
 
Mie siachi kula dona wala kunywa captain morgan kwa sababu mpk sasa hivi hakuna wataalamu walio thibitisha cancer ina sababishwa na nini hasa.Maana kila kitu utaambiwa kina sababisha cancer.sasa tule nini
 
Vijijini ndo vyakula vyao na wamevitumia enzi na enzi kama ni kweli wengi wangekuwa wameshakufa
Bila shaka ww ni shahidi kwamba magonjwa yanayotusumbua kwa sasa hayakuwepo hapo zamani....chukulia hospital ya ocean road zamani miaka ya 80 pengine ulikua unaweza ukaenda wodini ukakuta vitanda Havina watu..but what about now...maisha yamebadilika sana....na ww unatakiwa kubadilika...maisha ya zamani ni ya zamani....na sasa ni sasa...

zamani watu walikua wanakula vyakula halisi visiyowekwa Madawa what about now...vitu vingi either vimechakachuliwa u vimewekwa Madawa sasa usipokua makini usije sema hukuelimishwa [emoji310] [emoji310]
Na kwa ushauri ata nyanya unazonunua magengeni sasa hivi hakikisha unaziosha kwa sabuni na maji ya kutosha....kwani zinapuliziwa dawa asubuh ww mchana unazinunua vitu ambavyo zamani havikuwepo
 

Ahsante mangatara
Mkuu ungetoa Elimu ya bure pia Jinsi ya Kuandaa Dona kwa njia ya kawaida kabisa isio na Gharama,
ili kuitoa hiyo Sumu kwa Faida ya wanajamvi,Cha Msingi watu watumie Dona kwa Usahihi...ila ukisema watu wasitume,Ohhh obvious utaonekana wewe ni Mfanyabiashara unataka watu waache kutumia Dona...unatakiwa kuboresha Pale a,bapo watu wanakosea
"Dona kwa matumizi ya Nguvu ya Mwili" hhgg
 
Mie siachi kula dona wala kunywa captain morgan kwa sababu mpk sasa hivi hakuna wataalamu walio thibitisha cancer ina sababishwa na nini hasa.Maana kila kitu utaambiwa kina sababisha cancer.sasa tule nini
kisababishi cha kansa siyo kitu kimoja bali ni mrundikano wa mambo yakiwemo hayo ya kula dona zenye sumu kuvu a.k.a aflatoxini pamoja na dona zenye pesticides....
 

We ni jipu tu so kwendraaaaaa!! !
 


Tufwile nyambala Kyala nnunu gwe! Hatufi kirahisi rahisi hivyo wewe njoo na style nyingine boss

Kumbe hata fungus akitokoshwa Kwenye uji hafi anazidi kuwa strong ahahahahahhaha Asante Kwa hii elimu ya fungus hafi Kwenye uji
 
Huyu kama sio fadhaget au Dr mwaka basi atakuwa Ndodi.Tiba mbadala kazini.
 


monaco;
Hatuna mbinu mbadala ya kutengeneza dona. Dona hutokana na mahindi yetu ambayo hayajakobolewa. Yamesafishwa vizuri na kutengenezwa kwa ustadi.
Nimesema, mdudu huyu, huingia au huzalishwa na ile process ya kuvunda mahindi kwa sababu ya mvuke wa joto lile la mahindi. Protein yeyote ikitaka kuoza huwa inatoa mvuke. Sasa, kule kuoza oza, ndo huweza kumzalisha huyo mdudu.
Si lazima atokee ila ikiwa atatokea hukaa penye hivyo viini lishe. (Ni somo refu)
Namna ya kutayarisha dona safi ni wewe kuyasafisha mwenyewe mahindi yako. Wafanyi biashara wengi jamani tunawaona. Kweli wanajitahidi kuandaa bidhaa vyema lakini kwa kuwa ni biashara, siku wakipata mahindi hayo kwa bei ya chini kidogo, kuyachanganyia ndani ya mazuri. kwao hilo ni jambo dogo. Wanajali faida.
Siku ukutane na huyo mdudu, si unakufa tu ka kuku?? Kumbuka, hata ule unga, ukiwekwa vibaya, kama mahindi yalikuwa na unyevu kidogo zaidi ya kiwango, waweza zalisha hii hatari.
Kifupi, nashauri, dona usipende kuila kwenye chakula cha wengi (mama lishe na hoteli) au usipende kununua madukani. Nunueni mahindi, myatengeneze kwa usalama wenyewe.
 
Mzee hiyo sumu hata kama ipo kimsingi imeshathibitika haina madhara yoyote yale kuogopwa. Hicho kimekua chakula kikubwa sana cha wabantu tangu enzi na enzi. Sio ishu. Nimezaliwa mpaka Leo nakula ugali was mahindi. Mababu zetu wamekula. Sio ishu wala nini hiyo nadhani
 
Dr.ndodi anasema panya wana akili kuriko binadamu,wao panya wakula kiini chenye protein wakati binadamu wao watoa kiini..sasa wewe tena unakuja unasema dona ni sumu..sayansi ipo kutishana tuu nakumbuka kuna mtaalam mmoja wa mambo ya hewa alikua anatembea na mtungi wake kajifunga mirija na mask usoni akidai binadamu wengi wanavuta hewa yenye bacteria wengi wasioonekana kwa macho..ipo siku katika tafiti zenu mtakuja kusema kufanya mazoezi kuna madhara sana..
 
Ni kweli aflatoxins inasababisha kansa(ya ini) na matatizo mengine ya ini kwani ni moja kati ya active carcinogenic agent chemicals.

Aflatoxins huzalishwa na moulds(fungi) wanaoitwa,Aspergillus flavus na Aspergillus parasiticus ambao upendelea kuishi na kuzaliana kwenye mbegu na nafaka kama mahindi mtama mihogo mbegu za pamba na hata mbaazi, ikiwa hali ya hewa ni ya unyevunyevu au umajimaji na joto la wastani.

Inashauriwa unapotaka kuhifadhi chakula chako kama mahindi au mihogo uhakikishe vinakaushwa vizuri na havipati unyevunyevu utakaopelekea kuzaliana kwa hao fungi wanaozalisha aflatoxins.

Pia,ijulikane kwamba wahanga wakubwa wa aflatoxins ni watoto wadogo, inawasabibishia kutokua vizuri,magonjwa ya ini na hata kansa ya ini na si watu wazima kwani imegundulika watu mzima utengeneza resistance ndani ya mwili dhidi ya hizi chemicals za aflatoxins na kushindwa kupelekea madhara makubwa ingawa ni vema kuhakikisha unapotunza mahindi na vyakula vingine havipati majimaji kuzuia kukua kwa hawa fungi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…