Ugali wa dona sasa washamiri kwa kasi Dar es Salaam

Kwa ujumla napenda kuwaasa watanzania wezangu tuache kula mavyakula haya yasiyo ya asiri. Alafu haya maepple toka south Africa sio salama
Majuice ya kusindika haya sio salama
Soda hatari
Mayai ya kisasa pia hatari
Hebu tutumie vyakula vya hapa Tanzania vya asili tuvitumie katika uasili wake
 
kwa kifupi TUREJEE EDENI
 
Wanaume wengi wamekuwa wakilalamika kupungua kwa nguvu zao za kiume,hii inatokana na vyakula visivyo na virutubisho ambavyo vimekuwa vikutumika,ukila ugali wa dona basi ujue unapata faida maradufu kuliko kula ugali mweupe maana kile kiini cha njano cheche umuhimu kinakuwa hakipo kwenye ugali mweupe.
Ukijiuliza sana ni kwanini wazee wa zamani walikuwa na nguvu sana hata kwenye majamboz jibu ni vyakula halisi walivyokuwa wanatumia,dume zima unaagiza chipsi mayai unadhani kwenye shughuli utaweza?
 

mbona wazungu wanakula mijunk food na wanagonga k kiuhakika?

utafiti wangu usiyo rasmi nimegunduwa dhiki ndio adui mkuu mtu mpaka yuko na mwanamke faragha bado anawaza kesho akamboom nani pesa ili maisha yaendelee, sasa unategemea hilo boro litapata wapi nguvu wakati short circuit kati ya ubongo, wallet na babu boro young?
 

Nikutahadharishe tu kuwa sio mara zote dona ni nzuri, hasa nchi zetu za kitropiki. Uki-google kidogo tu utaona kuwa zaidi ya 80% ya mahindi yaliyopo sokoni yamekuwa contaminated na fungi ambao hutoa sumu zinazoitwa mycotoxins. Sumu hizi hususani zile za aflatoxins hazina rangi wala harufu, lakini zina madhara makubwa sana hasa kusababisha saratani ya ini. Ingawa madhara ya papo kwa hapo sio mengi (mfano walipokufa watu zaidi ya 150 Kenya mwaka 2004), madhara ya muda mrefu ndio ndio makubwa na hatari.
Zaidi ya kansa ya ini, sumu hizi husababisha kudumaa (kwa watoto), na upungufu wa kinga za mwili unakopelekea mhusika kupata maambukizo ya magonjwa kama malaria, kuharisha, typhoid, mafua na mengine mara kwa mara. Kwa wamama wajawazito kunakuwa na hatari ya kujifungua watoto wenye ulemavu au kuharibika kabisa kwa mimba.
Kwa bahati mbaya, fungi humea zaidi kwenye kiini na ganda la nje la mbegu ya mahindi, hivyo kuwaweka watu wanaokula chakula kinachotokana na mahindi ambayo hayajakobolewa katika hatari kubwa zaidi. Hapo ndipo linapokuwepo tatizo kwa kula dona, kwani imethibitishwa (huko Benin, Kenya na kwingine), kuwa kuosha na kukoboa mahindi kunaweza kupunguza hadi kiasi cha 60% ya mycotoxins zilizopo...

Pamoja na faida ya kuwa na protini na fibre kwenye dona, hasara ya kuwepo kwa mycotoxins inafanya wataalamu washauri watu wale sembe zaidi na kupata protini, vitamini na fibres kwenye vyakula vingine kama maharage, kunde na mboga za majani...

cc MziziMkavu Matola miss neddy Joseph
 
Last edited by a moderator:
asanteeeeeeee
 
Hapo kwenye RED Matola UMEJUAJE?
 
DAH, kama kuna mtaalamu mwingine atiririke hapa tutanue wigo wa uelewa zaidi
 
Sijawahi kusikia majunk food yakimsaidia mtu katika kuuletea mwili nguvu zaidi ya kuuumiza tu,si kwa wazungu au kwa waafrika,msingi hapa ni vyakula vyenye kuuletea mwili nguvu ndio msingi,ukifanya utafiti mdogo tu utagundua kuwa wanaume wengi tena vijana kabisa wameangukia kwenye matumizi ya vega(dawa za kuongeza nguvu za kiume)kitu ambacho ni hatari na kinaonesha ni kwa jinsi gani vyakula hivi vinavyokiharibu kizazi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…